TANZIA Padri Wilfrid Dinho Wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Afariki Dunia

Yule msema uongo wa Serikali haramu amedai kutangaza vifo hairuhusuwi kuna mamlaka husika ya kutangaza vifo. Tujiulize Watanzania ni vifo vingapi vya hii COVID-19 vimeshatangazwa na hii Serikali haramu? Jibu wote tunalijua.

Hahaaaaaa yule msemauongo wao hahaaaaaaaaa , ana PHd ambayo Kafundishwa na Kitima leo anadai Kitima hana Mamlaka , Matumbo haya , sawa bana ngoja tuone watakakoishia maana kwa sasa wako karibu na Mungu wao anayependa kutukuzwa Mungu wa Kabudi
 
Kuna watu bado wanasistiza kuombewa, wana maombi wanapukutika.
Siku moja watalazimika kujiombea wenyewe.

Mungu ampumzishe kwa AMANI Fr Wilfrid
 
Mimi nawashangaa akina Father Kitima, kazi kulaumu serikali tu wakati wao kama kanisa wamechukua hatua gani? wafunge makanisa hadi janga hili lipungue, Italy na Ulaya walifunga. Hapa nini kinashindikana? Kututajia idadi ya mapadre na ma sister wanaokufa sio suluhisho hata kidogo, kanisa wachukue hatua wao, maana jumuia zinaendelea, mikusanyiko makanisani inaendelea, alafu akifa padre lawama kwa serikali, kwani serikali ndio imewaua? kipi kigumu wasisitishe kanisa kwa miezi kadhaa? Au hawaoni Italy etc
Ni nani aliyezuia chanjo ya korona tanzania? Ni kanisa? Ni nani aliye entertain kutokuvaa barakoa? Ni kanisa? Ni nani aliyetangaza kuwa tanzania haina korona? Aliyedai kuwa corona "imekoronea mbari huko" si mkubwa wa nchi? Au ni askofu?
 
Usiishie kumlaumu mtu wakati una nafasi ya kuchukua hatua za kukuponya. Mwaka jana kuna Askofu alisitisha ibada kwenye jimbo lake na Serikali haikumuingilia. Tusilaumu kwa sababu tuna chuki na mtu fulani haitosaidia
Kwenye hili ni tofauti mkuu,leo asubuhi waziri ametoa statement ya serikali kwa msisitizo kuwa ni marufuku kutangaza hata vifo vya wapendwa wetu,huko mwanzo hatukuwahi kuzuiwa kufanya hivyo,zamani ikitokea tatizo la mlipuko wa maradhi serikali ilitoa taarifa na kusisitiza kuwa kila atakayepata ujumbe huu amwarifu na mwenzake,kwenye hili tunaambiwa hata kama una taarifa kaa kimya!! Usimwambie yeyote,zamani kipindupindu kiliitwa kipindupindu hivyohivyo,na mtu akifa kwa kipindupindu tuliambiwa wazi ili wengine tuchukue tahadhari,leo huruhusiwi hata kutamka neno corona mbele ya wenye mamlaka,toka kitambo tuliambiwa kuwa chanjo ni haki ya kila mtu,ila chanjo ya corona imekuwa haramu kwa nchi yetu tu! Tafakari,na ujue si kila hatua una haki ya kuchukua,hasa ukiwa mtanzania
 
Oh apumzike kwa amani baba Dino. Namkumbuka huyu baba enzi za utoto nimetumikia sana misa zake
 
Halafu kuna mtu akisha vembewa anakuja kutuambia kuwa hakuna kutangaza vifo
 
Kwenye hili ni tofauti mkuu,leo asubuhi waziri ametoa statement ya serikali kwa msisitizo kuwa ni marufuku kutangaza hata vifo vya wapendwa wetu,huko mwanzo hatukuwahi kuzuiwa kufanya hivyo,zamani ikitokea tatizo la mlipuko wa maradhi serikali ilitoa taarifa na kusisitiza kuwa kila atakayepata ujumbe huu amwarifu na mwenzake,kwenye hili tunaambiwa hata kama una taarifa kaa kimya!! Usimwambie yeyote,zamani kipindupindu kiliitwa kipindupindu hivyohivyo,na mtu akifa kwa kipindupindu tuliambiwa wazi ili wengine tuchukue tahadhari,leo huruhusiwi hata kutamka neno corona mbele ya wenye mamlaka,toka kitambo tuliambiwa kuwa chanjo ni haki ya kila mtu,ila chanjo ya corona imekuwa haramu kwa nchi yetu tu! Tafakari,na ujue si kila hatua una haki ya kuchukua,hasa ukiwa mtanzania
Tumbo baba
 
Halafu Jana wamekuja na drama kwenye vyombo vya habari kwamba wagonjwa wa changamoto za kupumua wamepungua muhimbili wakati watu wanaendelea kufa.

Yupo rafiki yangu mjomba wake alikufa wiki iliopota hsptl ya mount meru Arusha wakakosa hifadhi pale mochwari kumejaa,wakahangaika kwingineko pale mjini Arusha ikiwemo na hsptl ya seriani nako kumejaa.

Ukweli ni kwamba serikali haijaleta corona lakini msimamo wake usiofaa umekuwa chanzo cha kusambaa corona na kuuwa watu.

Raisi anasifia padre hadharani kwakutovaa barakoa,daladala watu mrundikano,viwanja vya mpira,kumbi za sinema nk.

Ila nahisi Mungu anakusudi fulani ngoja tusubiri.
 

Maneno haya hapa Ni kutoka kwenye fb page ya Askofu Kilaini.

Kwaheri Fr. Wilfrid Dinho. Pole sana Baba Ruzoka na wana Tabora ndugu na jamaa. . Huyu Fr. Dinho ni mmojawapo wa classmates wangu wachache waliokuwa wamebaki.

Tulipanga mwaka kesho tusheherekee pamoja miaka 50 ya upadre. Utuombee huko mbinguni.

Kwaheri rafiki yangu tulicheza pamoja basketball Ntungamo.

Tumwombee Mungu amlaze mahali pema mbinguni amina.
Atawaombeaje mtu akiyekufa,tena marehemu,nyie wazima ndiyo wa kumuombea na matendo yake mema aliyoyaacha duniani
 
Alafu anatokea jamaa mmoja anasema huruhusiwi kutoa taarifa / takwimu...

Hata kama mimi sio Mamlaka ya Hali ya Hewa, kama mvua zimezidi lazima nitaongea kwamba hizi mvua sio za kawaida..., ila kama ni zile za kawaida alafu kila siku natoa taarifa / utabiri hapo unaweza kuhoji authenticity ya taarifa zangu

RIP pia nadhani huyu hayupo kwenye zile namba zilimtisha jamaa hadi akatoa takwimu..., Tuendelee kuhoji ni kwa afya ya Jamii / Taifa letu

RIP
 
R I P,. fr. tutakukumbuka kwa mchango wako katika kuzponya nafsi za watu wa MUNGU.pole kwa wakatolic wote Jimbo kuu tabors
 
Apumzike kwa amani Fr. Wilfrid.

Chanjo ya bure kwenye ule mpango wa COVAX wa WHO ingeweza kumnusuru Padre huyu.

View attachment 1717503

Tuweke kwenye rekodi. Roho nyingine yapotea kizembe.
brazaj umesha hama kwenye Barakoa Sasa uko kwenye kupiga Kampeni ya Chanjo! Usiogope sana kila nafsi lazima itaonja umauti,yote ni Mipango yake Mungu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom