Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, amesema;
"Unaposema tusitetee Uhai wa Mtu, Mdude haonekani mpaka sasa hivi, alikuwa anachambua mambo ya Siasa ya Nchi wengine hawafurahi, sasa unaposema tusimtetee wakati sisi Kazi yetu ni kutetea Uhai wa Mtu, unatuambia tuache Dini, na Kazi yetu ni Kufundisha, Linda Uhai wa Mtu, kama amaekosea tulisha weka utaratibu, Kuna Polisi, kuna Mahakama, kuna Magereza, fuata hivyo?. Kwanini asionekane?."
"Ali Kibao amekamatwa kwenye halaiki mchana, mimi natoa mfano huu mpaka Siku ya mwisho. Soka ameitwa kwenye Kituo cha Polisi haonekani mpaka leo. Sasa unasema tunyamaze? Uovu lazima tuukemee!”
"Sasa kukemea Uovu ni kuingilia mambo ya Watu, tunawaambia wale wanaoyafanya wayaache na tutaendelea kuwaambia, na hatutaacha. Vinginevyo Kazi ya Mungu na Mwanadamu aliyeumbwa na Mungu asipomsikiliza Mungu yeye Mwenyewe atajifanya kuwa Mungu! Na sisi tunamtetea Mungu abaki kuwa Mungu na Mwanadamu abaki kuwa Mtumishi wa Mungu. Ndiyo Kazi ya kila Mtu, kila Mwanadamu anaitwa Mtumishi wa Mungu, kwahi kama unataka Uongozi linda UTU wa Mtu, fanya Watu wafurahie USITAWI wa shughuli zote, wafanye Watu WAJITAWALE, wafanye Watu WASHIKAMANE, leta UPENDO."
"Lakini tuna TUNU ambazo sisi Wakatoliki tunajivunia katika masuala ya SIASA! Ni kusimamia UKWELI ulivyo, hatuangalii umesemwa na nani?......."
Soma, Pia