Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,552
- 4,169
Padre Dkt. Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), ametoa kauli nzito akisema kuwa viongozi wa dini lazima waonyeshe wazi kwamba aliyehusika katika mauaji ya Ally Mohamed Kibao amefanya kosa kubwa na ni laana kwa Mwenyezi Mungu.
Pia, Soma: Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Padre Kitima alisisitiza kuwa, "Aliyemuua Kibao amefanya kosa baya na ni laana kwa Mwenyezi Mungu. Kama viongozi wa dini, lazima tuseme hili. Tunalaani vikali vitendo vya uhalifu kama hivi."
Aliongeza, "Unafikiri watoto wa Mzee Kibao, aliyeuawa kinyama, wataonana vema na wale wanaohisiwa? Hii imejenga chuki kubwa kati ya familia na jamii. Tunapiga vita, tuna laani, na tunahitaji aliyemuua Kibao atubu kwa Mungu wake au achukuliwe hatua na sheria."
Padre Kitima alisisitiza kuwa, kama viongozi wa dini, ni jukumu lao kutoa ujumbe wa haki na amani, na kuonya dhidi ya vitendo vya kinyama vinavyovuruga jamii na kuleta machafuko.
Soma:

- Familia ya Mzee Ali Kibao yatuma ujumbe kwa Rais Samia, yaomba uchunguzi wa wazi pamoja na kutoa kauli kali dhidi ya wahusika wa utekaji na mauaji
- CHADEMA: Mzee Ali Kibao ametekwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa kwenye basi. Usalama wa Taifa waeleze alipo
- John Mnyika aitwa Polisi kwa uchunguzi mauaji ya Ally Mohamed Kibao