Ni kweli maggid uliyaeleza ni sahihii.lakini kichguu hakijai kwa rundo la mchanga.haya ni matikeo ya uhuru wa kusema na kutenda bila mipaka.tumekuwa tukitetea sana watu viongozi wa dini na waandishi wa habari kuongea lolote hata kama kaulizao hatimaye zitakuja kuwa msingi wa chuki baina ya makundi.haya ndio matunda yanayojitokeza tusilalamike tumejijengea misingi mibovu sana.E mungu tuepushe na mabalaa hayaAsante maggid kwa maoni yako, ila bibi yetu Kirobo anaendeleaje na habari za sms?
Hivi Allah gani anayeshabikia kuua binadamu mwenzako? Hebu tujitsfakari
One Does Not Kill A Priest, Not A Sheikh Either!
- Padri hauawi, hata Sheikh pia...
Ndugu zangu,
Nimepokea kwa masikitiko makubwa habari za kuuawa kwa Padri Mushi wa Kanisa la Minara Miwili huko Zanzibar asubuhi ya leo.
Tumelelewa tukiamini, kuwa hakuna atakayethubutu kumpiga risasi Padri au Sheikh.
Kwa nini sasa?
Hakika, sote bila kujali tofauti zetu za kiimani, tuna lazima ya kuukemea uovu huu. Na mamlaka husika zihakikishe hakuna kinachoachwa bila kugeuzwa hadi waovu waliohusika na uovu huu watiwe nguvuni.
Maggid Mjengwa,
Iringa.