Padre: sio mafisadi ni mafisi- maji

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
253
11
Source: Mwananchi
Tunakoelekea matusi ya nguoni yatawatoka watu. hii inaonyesha jinsi watu walivyochukizwa na suala hiliPadri:
Waliohusika Richmond si mafisadi bali mafisi maji

Na Geofrey Nyang?oro


PADRE Agapit Mhando wa Jimbo la Morogoro, amedai kuwa watu wote waliohusika na kashfa Richmond si mafisadi bali ni mafisi maji.


Akihubiri kwenye misa iliyofanyika kwenye Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Manzese, Kanisa Katolikia Jimbo Kuu la Dar es Salaam jana, alisema viongozi hao wamelisigana Azimio la Arusha wsakaleta Azimio la wala rushwa.


Alisema kitendo chao cha kuipendelea Richmond ambayo haikuwa na sifa wala uwezo ni uhujumu wa uchumi uliokithiri.


"Hao siyo mafisadi bali ni mafisi maji," alisisitiza.


Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Shirika la Undugu Association aliyemaliza muda wake, Padri Baptiste Mapunda ameishauri serikali ikubali Katiba ya Tanzania kuandikwa upya na kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, ili kuharakisha na kuimarisha ujenzi wa demokrasia ya kweli nchini.


Padri Mapunda alisema katiba iliyopo pamoja na kufanyiwa marekebisho ya mara kwa mara, ina upungufu mkubwa usioweza kukidhi mfumo wa siasa za vyama vingi uliopo hivi sasa, kwa kuwa ilitungwa wakati wa mfumo wa chama kimoja cha siasa.


Akizungumzana na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salam jana, alisema wakati umefika kwa serikali ya kuyafanyia kazi kwa vitendo mawazo ya msingi yanayotolewa na wanaharakati, likiwemo la kuandikwa kwa katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi ili kuliepusha Taifa na uwezekano wa kutumbukia kwenye machafuko kama nchi jirani ya Kenya.


?Wakati umefika kwa serikali kuyafanyia kazi mawazo mbali mbali yanayotolewa na wanaharakati, likiwemo hili la katiba ili kuepusha taifa lisije likatumbukia kwenye majanga kama jirani zetu wa Kenya,? alisema.


Alisema kumekuwapo malalamiko kutoka kwa wanaharakati mbalimbali wakiwemo wanasiasa hasa wa kambi ya upinzani, kuhusiana na udhaifu wa katiba, hivyo kushauri kuwa mapendekezo yao yakaheshimwe na kufanyiwa kazi na serikali ili yasije yakatumbukiza kwenye majanga.

a kuimarisha demokrasia hapa nchini bali ni njia pekee ni kwa serikali kuunda Tume Huru ya Uchaguzi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom