TANZIA Padre Paul Nsekela Sabuni afariki dunia

TANZIA Padre Paul Nsekela Sabuni afariki dunia

Mwizukulu wa Buganda

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2024
Posts
657
Reaction score
1,792
Sabuni.jpg

Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa'ichi OFMCap, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, anasikitika kuwatangazia kwamba leo tarehe 30/01/2026 saa 10.31 alfajiri mpendwa wetu Padre Paul Nsekela Mboje SABUNI, Paroko wa Parokia ya IPTL, ameitwa nyumbani kwa Baba wa Milele akiwa katika matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.

Mazishi yatafanyika siku ya Jumatano tarehe 04.02.2026 katika Makaburi ya Mapadri yaliyopo katika kituo cha hija Pugu. Misa ya Mazishi itaanza saa 3:00 asubuhi.

Habari ziwafikie Maaskofu, Mapadri, Mashemasi, Watawa, Wanafamilia, Waamini wote walei wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote wenye mapenzi mema.

Raha ya Milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie, Apumzike kwa Amani; Amina

Padri.jpg
 
A very humble guy.
 
Apumzike kwa Amani bwana Paulo...

Nilipata kumjua miaka hiyo ya nyuma akiwa hata hana ndoto za kuwa mtumishi...

Alikuwa mtu mmoja mwenye roho nzuri sana
 
Back
Top Bottom