Padre Mapunda: Dk Slaa mwiba unaowatesa wanasiasa wengine

Padre Mapunda: Dk Slaa mwiba unaowatesa wanasiasa wengine

FreedomTZ

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2012
Posts
1,104
Reaction score
251
Amesema Yesu Kristo aliandamwa na uongozi wa Kiyahudi siyo kwa sababu alikuwa gaidi au jambazi, bali kwa sababu alikuwa ni tishio kwa mamlaka na vyeo vyao. Amesisitiza Dr. Slaa anaandamwa na CCM kwa sababu ni mwiba kwao na vyama vyenye mrengo wa CCM vinavyoamini katika siasa zisizo na faida. Kama kiongozi wa chama cha upinzani (Chadema) Dk Slaa ana mvuto wa pekee kwa Watanzania bila kujali dini, itikadi, kabila, vyeo wala tabaka la watu.
=================
Mapunda+padri.jpg

Saikolojia ya kawaida inatufundisha kwamba ukiona mtu anaandamwa kwa kiwango kikubwa, wakati mwingine ujue ni kwa sababu amegeuka tishio kwa uhai, vyeo na madaraka ya wasiompenda.

Yesu Kristo aliandamwa na uongozi wa Kiyahudi siyo kwa sababu alikuwa gaidi au jambazi, bali kwa sababu alikuwa ni tishio kwa mamlaka na vyeo vyao.

Sitaki kumlinganisha Dk Slaa na Yesu, lakini kama mwanadamu mwenzetu kuna yanayofanana na watu wengine duniani waliofanyiwa, hila kama hizo kwa sababu tu walikuwa tishio kwa watawala.

Dk Slaa kwa sasa siyo padri kama wanasiasa wengi wanavyodanganya umma wa Watanzania kwa sababu aliomba kibali cha kuondolewa mamlaka ya kipadri na alikubaliwa.

Kuendelea kumwita padri ni porojo za kisiasa na alama wazi ya hofu ya wapinzani wake kuelekea uchaguzi ujao na kuwapotosha wananchi wasiojua nini kinaendelea katika nchi yetu.

Ni dhahiri Dk Slaa kwa sasa ni mwiba kwa CCM na vyama vyenye mrengo wa CCM vinavyoamini katika siasa zisizo na faida. Kama kiongozi wa chama cha upinzani (Chadema) Dk Slaa ana mvuto wa pekee kwa Watanzania bila kujali dini, itikadi, kabila, vyeo wala tabaka la watu.

Dk Slaa amejizolea sifa nyingi katika utendaji wake pamoja na kurushiwa madongo mengi kwa lengo la kumchafua, lakini mbinu zote chafu zimeshindikana.

Waswahili hutumia neno ‘jembe' wakimaanisha mtu makini na mtendaji na ndilo jina analositahili Dk Slaa, ni mjenga hoja mzuri. Mtu wa namna hii hata kama utamfanyia fitina, chuki, mizengwe, hujuma ni kama kupoteza muda tu kwa sababu anajifahamu. Kwa mantiki hii, Dk Slaa ni kiongozi mwenye msimamo thabiti na anatetea kile anachokijua kwa nguvu na uwezo wake wote.

DK Slaa aliwahi kudai kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2010, aliporwa ushindi. Kulikuwa na madai kuwa baadhi ya viongozi wa dini walikwenda kumwona ili kumtuliza asiitishe maandamano ya kudai ushindi kama alivyofanya Raila Odinga nchini Kenya mwaka 2007.

Swali, kwa nini Dk Slaa alirudia tamko hilo mbele ya wageni mbalimbali wakiwa mabalozi wa nchi za nje? Alitaka kufikisha ujumbe gani? Watu makini hawakurupuki bali wanapangilia mambo yao.

Kama ni sifa za uongozi, basi Dk Slaa hababaishi. Ni kiongozi mwenye muono, yaani ile hali ya kuweza kuona anakwenda wapi na wengine kumfuata.

Tanzania ya leo imepoteza mwelekeo kiasi cha kulinganisha na meli isiyo na nahodha.

Tanzania ya sasa tunahitaji kiongozi atakayerudisha imani ya wananchi.

Leo Watanzania wengi wamechoka na Utanzania kwa sababu ya mateso, hujuma, unyanyasaji, vitisho, na maovu yanaendelea kutokea kila kukicha.

Tanzania ya leo inahitaji "Nyerere mpya" au "Mandela mpya" kiongozi mzalendo mwenye kuwapenda Watanzania kwa moyo wote, mwenye kulinda amani na utulivu siyo kwa kutumia bunduki, risasi wala mizinga bali kwa kutumia utawala bora, demokrasia na matumizi bora ya sheria za nchi katika kutenda haki sawa. Wizi wa mali ya umma, wakiwamo tembo na wanyamapori wengine ni lazima walindwe kwa nguvu na uwezo wote.

Je, kiongozi kama huyu atapatikana kweli? Mungu si athumani basi ametuletea Dk Slaa ili aweze kuongoza ukombozi wa pili kwa Watanzania wanaoteseka.

Watanzania mmeshuhudia sasa namna watawala walivyoshindwa kuwaletea Katiba mpya inayotokana na mawazo ya wengi. Wameamua kuchakachua mawazo ya wengi kuwaletea katiba yao.

Hii ni alama wazi ya dharau kwa wananchi na ubabe uliopitiliza na hivi dawa yake ni kuungana na kuipumzisha ili kuwapa nafasi viongozi na chama kitakachoweza kutuletea Katiba Bora.

Mungu wabariki Watanzania. Tutaonane wiki ijayo panapo majaliwa katika tafakari mpya.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu Bwana ni nguzo muhimu sana kwa CHADEMA na UKAWA. Endapo ataidhinishwa kuwania Uraisi mchuano utakua mkubwa sana na MaCCM ambao mpasuko wa wazi unanukia tayari katikati yao, kama hautatokea kabla utatokea baada ya uchaguzi kutokana na uhasama na kutovumiliana kunakokua sana ndani yao (wenye macho wanajua sana hili).

Iwe isiwe tuendendako alama za kuimba nyimbo mpya za ukombozi wa pili zinaonekana kwa uwazi zaidi kuliko kipicho chochote cha awali.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Africa.
 
Huyu padre ni mwiba mkali sana kwa CCM, anatoa elimi nzuri sana ya uraia.

Hongera Father Baptist Mapunda
 
Huyu Padre nasikia atagombea ubunge kupitia Chadema.

Padre Mapunda kwenye makala yake amesema Dr. Slaa alishaondolewa mamlaka ya kipadre na uongozi wa juu wa Kanisa Katoliki baada ya yeye kuomba. Hivyo kwa maoni ya padri Mapunda si sawa kuendelea kumwita Dr Slaa padri;hizo ni propaganda.
 
Siku hizi makanisa yamevamiwa mpaka wahuni wa vijiwenu wanajiita mapadri bure kabisa tutaanza kuwatia bakora wakileta mambo yao ya siasa kwenye nyumba za ibada.

IV UNAJUA MA PADRE WANAVYOPATIKANA AU UNAJISEMEA TU kuna TOFAUTI KUBWA KATIKA KUWAPATA MAPADRE na WACHUNGAJI. USIKURUPUKE
 
Huyu Padre sasa anaenda too far,angepaswa awe tu mpigania haki na usawa katika jamii ila kuingia kabisa hivi anakosea maana Wakatoliki anawasalisha jambo wote wanapaswa wawe na matendo mema na wapiganie usawa na haki lakin wana maono tofauti juu ya viongozi wa siasa.

Hakupaswa kwenda this far
 
Huyu Padre nasikia atagombea ubunge kupitia Chadema.

Ritz,

Usipende sana kujitoa ufahamu.Katika Miaka 15 aliyokua Mbunge ameonyesha kuwa mbunge anapaswa kufanya nini

Tatizo la nchi yetu ni mfumo mbovu wa CCM na tunahitaji overhaul na mtu wa kusimamia hili

Kwa namna ambavyo Dr.Slaa amekua akisimamia maswala ya msingi na kuonyesha weledi wa kiwango cha juu na uzalendo ndiye anayeweza kusimamia haya

Sisemi hivi kwa sababu ni kiongozi wangu kiutendaji isipokua wakati mwingine tuwe realistic

Taifa hili limepoteza mwelekeo kisera na kiitikadi

Yote yaliyosemwa na Father Mapunda ni ukweli mtupu

Na mwaka huu tumejipanga kukabiliana na wale watawala wenye hila katika zoezi zima na kilichotokea kwa wale waliochakachua matokeo ya serikali za mtaa ni rasharasha tu.

Tutawakabili kwa nguvu na kila mbinu ambazo hamjawahi kushuhudia tangu tupate uhuru na tutatoa fundisho kwa mamlaka nyingine Afrika

Haki za kiraia na Demokrasia haziwezi kuhujumiwa kisha wahusika wakapona hivihivi
 
Last edited by a moderator:
Huyu Padre sasa anaenda too far,angepaswa awe tu mpigania haki na usawa katika jamii ila kuingia kabisa hivi anakosea maana Wakatoliki anawasalisha jambo wote wanapaswa wawe na matendo mema na wapiganie usawa na haki lakin wana maono tofauti juu ya viongozi wa siasa.

Hakupaswa kwenda this far

ILA KUMBUKA KAMA KWELI UNA MCHA MUNGU HUWEZI KUWA au KUIPENDA CCM, INAENDA KINYUME NA MAAMRISHO MENGI YA MWENYEZI MUNGU
 
Kwa hiyo kama Slaa ana matendo kama ya Yesu basi panapo mfaa ni kanisani zaidi kuliko Ikulu!

Lakini si shangai Mapadri kupigiana chapuo...nasubiri mpambano kati ya CUF na Chadema!

Nchi hii haito ongozwa na kiongozi wa dini!
 
Huyu Padri ataleta ugomvi kati ya CUF na Chadema.
 
Ni ngumu sana kutofautisha Kanisa na Chadema.

Huo udini utakufikisha wapi? Tuna waislam na hata wasiokua na Dini ndani ya Chadema

Mlisema Chadema ni cha wakristo kisha CUF ya Waislamu sasa CUF na CHADEMA vyama vya wakristu na Waislam wameungana ina maana CCM ni chama cha wapagani?

Achana na siasa hizi kaka.Nigeria hali tete kwa sababu ya ujinga huu
 
ritz,

usipende sana kujitoa ufahamu.katika miaka 15 aliyokua mbunge ameonyesha kuwa mbunge anapaswa kufanya nini

tatizo la nchi yetu ni mfumo mbovu wa ccm na tunahitaji overhaul na mtu wa kusimamia hili

kwa namna ambavyo dr.slaa amekua akisimamia maswala ya msingi na kuonyesha weledi wa kiwango cha juu na uzalendo ndiye anayeweza kusimamia haya

sisemi hivi kwa sababu ni kiongozi wangu kiutendaji isipokua wakati mwingine tuwe realistic

taifa hili limepoteza mwelekeo kisera na kiitikadi

yote yaliyosemwa na father mapunda ni ukweli mtupu

na mwaka huu tumejipanga kukabiliana na wale watawala wenye hila katika zoezi zima na kilichotokea kwa wale waliochakachua matokeo ya serikali za mtaa ni rasharasha tu.

Tutawakabili kwa nguvu na kila mbinu ambazo hamjawahi kushuhudia tangu tupate uhuru na tutatoa fundisho kwa mamlaka nyingine afrika

haki za kiraia na demokrasia haziwezi kuhujumiwa kisha wahusika wakapona hivihivi

tatizo ccm hawapendi ukweli, hongera father b mapunda
 
Kwa hiyo kama Slaa ana matendo kama ya Yesu basi panapo mfaa ni kanisani zaidi kuliko Ikulu!

Lakini si shangai Mapadri kupigiana chapuo...nasubiri mpambano kati ya CUF na Chadema!

Nchi hii haito ongozwa na kiongozi wa dini!

Badala ya kujenga hoja unaombea UKAWA mabaya
 
Ritz,

Usipende sana kujitoa ufahamu.Katika Miaka 15 aliyokua Mbunge ameonyesha kuwa mbunge anapaswa kufanya nini

Tatizo la nchi yetu ni mfumo mbovu wa CCM na tunahitaji overhaul na mtu wa kusimamia hili

Kwa namna ambavyo Dr.Slaa amekua akisimamia maswala ya msingi na kuonyesha weledi wa kiwango cha juu na uzalendo ndiye anayeweza kusimamia haya

Sisemi hivi kwa sababu ni kiongozi wangu kiutendaji isipokua wakati mwingine tuwe realistic

Taifa hili limepoteza mwelekeo kisera na kiitikadi

Yote yaliyosemwa na Father Mapunda ni ukweli mtupu

Na mwaka huu tumejipanga kukabiliana na wale watawala wenye hila katika zoezi zima na kilichotokea kwa wale waliochakachua matokeo ya serikali za mtaa ni rasharasha tu.

Tutawakabili kwa nguvu na kila mbinu ambazo hamjawahi kushuhudia tangu tupate uhuru na tutatoa fundisho kwa mamlaka nyingine Afrika

Haki za kiraia na Demokrasia haziwezi kuhujumiwa kisha wahusika wakapona hivihivi

Mngekuwa hamuendekezi njaa na kuhongwa kirahisi maneno yako ningeyaamini
 
Last edited by a moderator:
Siku hizi makanisa yamevamiwa mpaka wahuni wa vijiwenu wanajiita mapadri bure kabisa tutaanza kuwatia bakora wakileta mambo yao ya siasa kwenye nyumba za ibada.

Mbona nlishindwa kuchapa viboko wale wachungaji njaa waliokuwa kwenye binge maalum la katiba?Au ni kwa kuwa ni vibaraka wa ccm?
 
mkiona neno dr. Slaa makalio yanatikisika...

hauoni safu ya viongozi wa kanisa mkuu.

1) padre mapunda

2) padre slaa

3) mchungaji msigwa

4) mchungaji israel natse

na wengine wengi.

mungu yupi kamanda? Huyo mungu wa chadema amekubali kabisa chadema kiwe chama cha upinzani.

mkuu kumbe chadema hakuna masheikh.

huyu padri ataleta ugomvi kati ya cuf na chadema.

hivi ccm imewatuma kutetea dini gani? Ccm imewatuma kupinga dini gani? Hivi ccm inapigania dini gani? Mnataka kusema chochote kinachofanywa ndani ya ccm tukiangalie kwa jicho la kidini?
 
Back
Top Bottom