Padre, dogo na njia ya peponi

NewDawnTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
1,667
Reaction score
362
:cheer2:
Padre alipotea katikati ya mji akiwa anatafuta kwena mahali ofisi ya posta ya wilaya ilipo....

Kwa bahati nzuri Padre akamwona kijana mmoja mstaarabu akaamua kumuomba yule kijana maelekezo ya namna ya kufika posta

Kijana yule alimwelekeza mpaka padre akaelewa. Padre akamshukuru sana yule kijana. Kisha akamwambia kijana

Padre: Ahsante sana kijana wangu kwa kunionesha njia ya posta, na wewe karibu jumapili kanisani kwangu nikuoneshe njia ya peponi

Kijana akamwambia padre: "Njia ya posta yenyewe huijui, ya kwendea peponi utaijua
je?"
 


ahhahahaaaaaaa huyo mbaya
ehe padri alisemaje baada ya dogo kusema hvyo
 
Dogo hamkawizi mtu kampa sure hapohapo
 
Duh, Dogo Sijui Kama Atakuwa Na Imani Lol.
 
Duh!nahisi Padre aliondoka kimya kimya.Mhhhhhhhhhhhhhh hii kasheshe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…