Padre aitaka CCM ijiandae KUONDOKA; Adai yuko tayari kupigwa risasi akisema ukweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Padre aitaka CCM ijiandae KUONDOKA; Adai yuko tayari kupigwa risasi akisema ukweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by R.B, Jun 25, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,168
  Likes Received: 1,103
  Trophy Points: 280
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeshauriwa kuanza kujiandaa kuondoka madarakani kutokana na kushindwa kuboresha maisha ya wananchi ambayo yanazidi kuwa magumu.

  Kauli hiyo ilitolewa na Padre wa Kanisa Katoliki, Baptiste Mapunda ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Faidika Afrika Mashariki, wakati akihubiri katika ibada ya misa ya Jumapili ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Yohana mtakatifu iliyofanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Karoli Lwanga, Yombo Dovya, Dar es Salaam jana.

  Padre Mapunda alisema kuwa yupo tayari kupigwa risasi, lakini hatamuogopa mtu katika kusema ukweli juu ya hali mbaya ya maisha inayowakabili wananchi kwa sasa.

  Alisema kuwa CCM haiwezi kukwepa lawama za maisha magumu kwa wananchi, na hivyo akawataka wajiandae kuondolewa madarakani kama ilivyotokea kwa vilivyokuwa vyama tawala katika nchi za Kenya, Zambia, Malawi, Ghana na kwingineko.

  "Hivi sasa nchi ipo katika hali mbaya, kila mtu anafanya lake, hakuna kiongozi wa kuwatetea wananchi, kila kiongozi anapigania masilahi binafsi jambo ambalo ni hatari," alisema Mapunda.

  Aliongeza kuwa, Tanzania inahitaji viongozi ambao watakuwa tayari kuitetea nchi hata kwa kukatwa kichwa, na hivyo kujigamba kuwa hata yeye yupo tayari kwa hilo.

  "Mimi sikuumbwa kumtumia diwani, mbunge wala kiongozi yeyote, bali nipo kwa ajili ya kuhubiri injili ambapo hadi sasa nina miaka 22 katika kazi hii," alisema padre huyo.

  Alisema nchi inaelekea kubaya,Watanzania wamebaki kutafakari na kuvitegemea vyombo vya usalama badala ya Mungu, na hiyo ni kutokana na hofu ya maisha waliyonayo.

  Padre Mapunda alibainisha kuwa, nchi haina amani kutokana na kufikia hatua ya kuchoma makanisa, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa huku chama tawala kikishuhudia.

  Alisema kutokana na viongozi wetu kutokuwa na hofu ya Mungu zaidi ya kujiangalia wao, imefikia hatua wabunge kuanza kutukana bungeni na kuacha kujadili masuala yenye masilahi kwa wananchi jambo ambalo ni hatari kwa taifa.

  "Matumizi ya dawa za kulevya, kupanda kwa mfumuko wa bei wa vitu, rushwa na maisha kwa ujumla ni moja ya dalili kuwa nchi imeshindwa kuongozwa, ni lazima wapatikane viongozi ambao watathubutu kuwatetea wananchi wake," alisema Mapunda.

  Alisema hivi sasa magonjwa ya saratani yameongezeka maradufu kutokana na kula vyakula vyenye sumu, ambavyo vinaruhusiwa na watendaji wasio waaminifu na Wizara ya Afya ikiacha jambo hilo liendelee.

  "Binafsi naunga mkono mgomo wa madaktari kwani wanadai haki, hata nje ya nchi migomo imekuwa ikifanyika na kulipwa stahiki zao, sasa kwanini hapa nyumbani wanashindwa kufanya hivyo?" alihoji Mapunda.

  Padre Mapunda aliirushia makombora Idara ya Usalama wa Taifa kuwa ndio inayomdanganya Rais Jakaya Kikwete kuwa hakuna matatizo wakati hali ni mbaya.

  Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kisesa, Luhanga Mpina (CCM), amejitokeza na kueleza msimamo wake wa kutopiga kura ya kupitisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

  Akizungumza na Tanzania Daima mjini Dodoma jana, Mpina alisema kuwa aliendelea kuwa na msimamo wake kutokana na serikali kushindwa kujibu hoja zake za kuongeza fedha katika mpango wa maendeleo ya taifa wa miaka mitano.

  "Kabla ya Waziri wa Fedha hajaanza kujibu hoja za wabunge, nilipata maelezo toka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wassira na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge), William Lukuvi kuwa hoja yangu imepokelewa na serikali na kwa kuwa muswada wa fedha haujapitishwa, hivyo bado ipo nafasi ya kutafuta fedha kugharamia mpango wa maendeleo," alieleza Mpina.

  Mbunge huyo alisema hoja yake kubwa ni kutaka fedha za maendeleo ziongezwe toka sh trilioni 2.2 kufikia trilioni 2.7 kwa fedha za ndani ili kukidhi mahitaji ya fedha zinazohitajika kutekeleza miradi mbalimbali iliyoainishwa katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

  Alisema kuwa, pamoja na kupata maelezo kutoka kwa mawaziri hao, bado hoja hiyo haijafungwa wala haijafika mwisho kwa kuwa mswada wa sheria ya fedha ya mwaka 2012 utawasilishwa na kuidhinishwa na Bunge mwishoni baada ya kupitia bajeti ya wizara zote.

  Mpina alisema sheria hiyo ndiyo inayoidhinisha mapato na matumizi ya vifungu vyote vya fedha, na kuongeza kuwa kutokana na hali hiyo, bado anatoa wito kwa wabunge wote bila kujali itikadi za vyama vyao, kuungana pamoja katika kupitia mafungu ili kupunguza na kufuta matumizi yasiyokuwa na tija na kuziokoa fedha hizo kwa kuzipeleka katika miradi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kutafuta vyanzo vipya vya mapato.

  Alisema kutokana na upungufu wa sh bilioni 500 katika bajeti ya maendeleo, kumesababisha miradi mingi kupata fedha pungufu na mingine kukosa kabisa tofauti na ilivyoainishwa katika mpango huo.

  Aliitaja miradi ambayo ilipata fedha kidogo kuwa ni Tanzania Investment Bank (TIB) ambayo imetengewa sh bilioni 30 badala ya bilioni 125, Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) imetengewa sh bilioni 40 badala ya bilioni 100, kufanya upembuzi yakinifu na kujenga skimu za umwagiliaji zimetengwa sh bilioni 7.1 badala ya bilioni 242 na ujenzi na ukarabati wa reli ya kati zimetengwa sh bilioni 134 badala ya bilioni 198.

  "Kwa kuwa Waziri wa Fedha wakati akijibu hoja za wabunge licha ya kusisitiza kuwa ‘finance bill' haijapitishwa, lakini hakusema kama fedha za maendeleo zitaongezwa na kwa kuwa kanuni za kudumu za Bunge toleo la 2007 hazitoi mwanya kwa wabunge kuomba ufafanuzi wa ziada juu ya maelezo yaliyotolewa na waziri, hivyo niliamua kutopiga kura kwa sababu hoja yangu ilikuwa haijajibiwa licha ya kuwa nilipata maelezo ya awali ya mawaziri, ambayo yalikuwa nje ya kumbukumbu (hansard)," alisema.

  Alibainisha kuwa, msimamo wake unabaki palepale na atashuhudiwa siku ya kupitisha finance bill kama ataunga au hataunga mkono.
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Uamsho mwingine huo.
   
 3. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu padri mdini sana. Kwa kuwa mwenyekiti ni muislam ndio kaibuka. Alipokuwa mkapa alinyamaza kimya.
  2015 utasikia huyu ni mbunge wa chadema
   
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Hana tofauti na wale madevu wa Unguja.
  Akitaka kuingia siasa si anamwona Mchungaji Msigwa?
  Asitumie vibaya mimbari isiyo yake.
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Huyu Padre ni chama gani?
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Haya makanisa ndio yalianzisha chokochoko Rwanda watu wakauana kwa mamilioni.
   
 7. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tunasikia sana waislamu wananalalamika kwamba kuna Mfumo Kristo serikalini. Serikali hiyo imeundwa na CCM. Tunasikia sana viongozi wa dini ya Kikristo pamoja na wapenda maendeleo wengine wakipinga dhuluma wanazofanya viongozi wa serikali kwa wananchi. Cha kushangaza utasikia waislam wengi(hawahawa wenye kupinga mfumo kristo) wakiwabeza hawa viongozi wa dini za kikristo eti wanaikemea serikali kwa sababu rais au mwenyekiti wa CCM ni muislam. Hawajiulizi kwanini mkatoliki apinge serikali ileile inayoondeshwa na mfumo katoliki. Siku nyingine utawasikia eti nchi hii imepata umaskini kutokana na kuwa na viongozi wengi wa kikristo. Siku nyingine utawasikia ooh CCM itatawala milele CHADEMA mlie tu n.k n.k Mbona mimi siwaelewi hawa ndugu zangu akili zao zinavyofanza kazi? Wanataka nini hasa? Umaskini wa Tanzania uendelee? Mfumo kristo uendelee? Au ??
   
 8. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Tunaongelea mtu aitwaye Padre Mapunda na si Kanisa.
  Mbona husemi Uislamu ulivyoiangamiza Somalia.
  Watu wengine bwana kufikiri ni taabu tupu!!!
   
 9. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,755
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Nadhani Padre anayo haki ya kutoa maoni kama walivyo raia wengine.Hakuna ukweli zaidi ya huo,na waumini lazima waambiwe.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Na padre huwa anafanya kazi zake msikitini, au sio?
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  CCM ya Nyerere na Mkapa sio CCM ya leo.
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  chama cha uamsho
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  pia makanisa yalianzisha chochoko somalia, misri. algeria, Tunisia, Libya, syria, Iraq, Nigeria na Afraghastan......ambako wakristo ni wengi kuliko waislamu kama sensa ya haki itafanyika
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hawajiulizi kwanini mkatoliki apinge serikali ileile inayoondeshwa na mfumo katoliki

  wakristo wanapinga serikali inayoendeshwa na mfumo kristo????????????mmmmmh
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Katika maelezo yake padri hajatukana mtu wala uislamu amejenga hoja tutumie kujenga hoja kupinga alichosema
   
 16. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  padri huyu pengine kasomeshwa kwa pesa ZA MOU. kweli shukrani ya punda ni machuzi
   
 17. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe Ritz mbona umekimbia kujibu hoja kwa ndugu Nguruvi3 kule kwenye grtthinkers huyoooo jamaa anakusubiri..
   
 18. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hiyo dhana ya Mfumo Kristo ni ya waislam. Mimi nimewauliza kwanini hawajiulizi mkrito apinge mfumo kristo ambao wenyewe(waislam) wanasema unaendesha serikali?
   
 19. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona umemkimbia kule kwa Nguruvi3?
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Katika maelezo yake padri hajatukana mtu wala uislamu amejenga hoja tutumie kujenga hoja kupinga alichosema.

  Nilijua suala la kuchoma moto makanisa znz litaiweka CCM mbali na kanisa.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...