Oya shika mchuma!

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
*Kondakta *: Kaa mkao wa pesa.
*Abiria *: Si tumetosha? Twende basi!
*Kondakta*: Tunafanya kazi kwa hesabu mama mdogo.
*Abiria*: Hebu twendeni. Kuna watu huko mbele.
*Kondakta*: Kama una haraka ungeenda toka juzi. Tuko kazini hapa.
*Mpiga debe*: Wenye haraka wanaonyesha. Wenye haraka huchukua teksi.
*Abiria*: Tukichukua teksi mtakula wapi. Hebu acheni dharau. Twendeni, gari
si imejaa?
*Mpiga debe*: Jamani, mchuma haujai. Inayojaa ni ndoo ya maji. Haya,
Kariakoo, Kariakoo... gari nyeupe hii.
 
Ni saa tano usiku. Siku ya jumamosi. Kituo cha mabasi Mwenge. Tunaelekea
Mbezi Beach.
*Abiria*: Dereva twende bwana...saa za majeruhi hizi.
*Kondakta*: Bado vichwa babu. Gari haiendi mswaki hii hata siku moja.
*Abiria* (amelewa chakari): Nina haraka ya kufumania. Nimeambiwa saa tano na
nusu ndio saa ya kumfumania mbaya wangu.
Mara abiria huyu aliyelewa anaanza kutapika.
*Abiria 1*: Jamani watu wameanza kutapika humu ndani.
*Abiria 2*: Nipisheni nitoke miye...
*Abiria 3*: Afadhali niende kwa miguu.
*Kondakta*: Kuna wagonjwa huku?
*Abiria 4:* Twendeni. Hamjui ni mambo ya wikiendi haya?
*Abiria 5*: Pombe za bure hizo.
*Kondakta*: Kama sio pombe za bure basi ni za mkopo. Shuka bwana mzee.
Walevi hawa kwanza huwa hawataki kulipa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom