Over speed kwa private car sio kosa!!

Hao jamaa walinidaka Jumapili iliyopita tunavoenda Arusha, kiukweli nilikwazika ila wako sahihi ukiwa ndani ya 50kph mark ni lazima uende speed hiyo mpaka uimalize ila nje ya hapo ukiwa na private waeza gonga hadi 260kph kama gari yako inaruhusu hawatakuuliza. Ingawa kwa mabasi wana limit ya 80kph na wanapigwa tochi maporini hasa njia ya arusha na kwenda kushikwa mbele ya safari.
 
Hahaaa kuna jamaa unapomaliza tu mlima kitonga huwa anajificha kwenye karavati basi nshamsomea na mwingine hapa Karibu na melela kwa wamasai wachoma nyama anajificha kwenye mbuyu imekula kwake hawa jamaa ukiwa mzoefu na njia hawakusumbui,ila ukipinduka urudi kuandika sledi....
 
Ningekushauri ufanye IQ test kwanza kabla ya kuongeza muda leseni yako!
 
Sheria za barabarani ni kwa ajili ya wote sio vyombo vya umma tu, kumbuka kwamba mwendo kasi mkubwa kupita kiasi unaweza kusababisha madhara kwa watumiaji wengine wa barabara pia.
 
Aseeee kumbe washawahi kula 30 zangu za overspeeding
 
Kwa wenye Smartphone hao Traffic Officers wenye Tourch utawaona hata wajifiche kwenye Handaki kama unataka kuwaepuka na unataka ku-over-speed ila ukipinduka na ki-Starlet chako utalipa faini Mbinguni
 
Mleta mada*
umeanza kuendesha gari mwaka gani?
Ulijifundishia wapi?
Unayo valid driving license?
Walikufundisha sheria za Barabarani huko ulikojifundishia gari?
 
Mleta mada*
umeanza kuendesha gari mwaka gani?
Ulijifundishia wapi?
Unayo valid driving license?
Walikufundisha sheria za Barabarani huko ulikojifundishia gari?
Nazijua sana tu...issue iliyopo ni moja tu...kwenye ike notification hakuna kosa tajwa la overspeed kwa private car!
 
Kwa wenye Smartphone hao Traffic Officers wenye Tourch utawaona hata wajifiche kwenye Handaki kama unataka kuwaepuka na unataka ku-over-speed ila ukipinduka na ki-Starlet chako utalipa faini Mbinguni
hebu share hizo techniques
 
Hata mimi kaka juzi wamenifanya vibaya kule Mara wameweka vibao vya 50kp/h kwenye miteremko karibu yote na hasa Trm wapiga kamera wanajificha kwny madaraja.
No kama Kuna kibao cha alama ukavunja basi unakosa, kama sio makazi na wewe ukaoverspeed I mean over 80km/hr. Hapo ni utashi wako Lakini kukiwa na kibao cha amri huna ujanja, kile cha kukushauri unaweka ukavunja Lakini ukikosea imekula kwako
 
Mimi nadhani check points zingewekwa kwenye entry na exits za mikoa kufanya mahesabu umetoka mkoa A saa ngapi na kuingia saa ngapi halafu wacalculate speed uliyotumiah
 
No kama Kuna kibao cha alama ukavunja basi unakosa, kama sio makazi na wewe ukaoverspeed I mean over 80km/hr. Hapo ni utashi wako Lakini kukiwa na kibao cha amri huna ujanja, kile cha kukushauri unaweka ukavunja Lakini ukikosea imekula kwako

Kwa ukweli ni makosa yayotafutwa kwa hila. Si haki vibao vimewekwa kwenye madaraja na ukiwa mgeni ni lazima tu utanasa mtego wao haramu kwa kweli jambo hili sasa ni kero .
Bora maeneo ya watu wengi (centre ) vibao vifanye kazi lakini si nje ya miji na hasa kwenye miteremko ni uonevu kwa madereva
 
Anayejua kutumia smartphone kuona speed camera zilipo atuelekeze.. Naskia hii kitu inawezekana
 
Taratibu zote zinawekwa kwa manufaa ya dereva abiria na watu wengine na pia vyombo vingine vya usafiri barabarani
 
Mjomba utakuwa traffic officer bila shaka unataka kuongeza mtaji sasa.
 
Kwa wenye Smartphone hao Traffic Officers wenye Tourch utawaona hata wajifiche kwenye Handaki kama unataka kuwaepuka na unataka ku-over-speed ila ukipinduka na ki-Starlet chako utalipa faini Mbinguni
Umesema kweli. Mimi huwa natumia app ya Be On Road kufahamu waliko na tochi zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…