PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Mgombea wa urais wa Zanzibar, kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman amewataka Wazanzibari kuwapima viongozi kwa vigezo mbalimbali ikiwemo kujali maslahi ya wananchi anaowaongoza.
“Mkitaka kupima kiongozi, mpime kwa kiasi hicho au kwa vigezo hivyo, maslahi makubwa ya wananchi ni haki katika nchi yao, ikifika mahali ukachukua haki ya mwananchi na kumpa mgeni unakiuka kiapo chako,” amesema Othman.
Othman amesema viongozi wakiingia katika ofisi za umma, wanakula kiapo kwa Mungu kwamba wanakwenda kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, bila uoga na kuweka mbele ya maslahi ya watu wanaokwenda kuwatumikia.
Othman maarufu ‘OMO’ ametoa ahadi hiyo Jumamosi Oktoba 11,2025 katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyikwa uwanja wa Kivumbi Jimbo la Amani, Mkoa wa Mjini Magharibi.
“Ukiwa kiongozi wa nchi, uwe Rais, mwakilishi au mbunge, kazi yako kubwa ni kulinda maslahi ya nchi na maslahi ya wananchi, sio maslahi yako binafsi au familia yako,” ameeleza mgombea huyo.
Amesisitiza kuwa wajibu wa kwanza wa kiongozi ni kutunza haki za mwananchi, lakini hali tofauti ilivyo Zanzibar ndio maana kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi wakidai kudhulumiwa haki zao ikiwemo ardhi.
Othman amewatoa hofu Wazanzibari, akiwataka kuwa amani kuelekea Oktoba 29, akidai ACT-Wazalendo kinaingia katika uchaguzi kikiwa na matumaini makubwa ya ushindi, kwa sababu waliomsimamisha ana sifa zote za kuongoza.