PreGE2025 Othman Masoud Othman: Inakuwaje Polisi waongozwe na Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya ambaye ameelezwa wajibu wake ni kuhakikisha CCM inashinda?

PreGE2025 Othman Masoud Othman: Inakuwaje Polisi waongozwe na Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya ambaye ameelezwa wajibu wake ni kuhakikisha CCM inashinda?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo na Makamu wa kwanza wa Rais Zazibar Othman Masoud Othman anaeleza kuwa

"Kwenye Tume ya Haki Jinai nilipendekeza Polisi wasiongozwe na wanasiasa. Inakuwaje Polisi waongozwe na Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya ambaye ameelezwa wajibu wake ni kuhakikisha CCM inashinda? Mimi ninajua hata Polisi wenyewe hawapendi kuongozwa na wanasiasa. Jeshi la Polisi liwe chombo huru kinachofanya kazi kwa weledi."
View attachment 3348661
 
Attachments

  • 20250528_191328.jpg
    20250528_191328.jpg
    232.9 KB · Views: 6
Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo na Makamu wa kwanza wa Rais Zazibar Othman Masoud Othman anaeleza kuwa

"Kwenye Tume ya Haki Jinai nilipendekeza Polisi wasiongozwe na wanasiasa. Inakuwaje Polisi waongozwe na Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya ambaye ameelezwa wajibu wake ni kuhakikisha CCM inashinda? Mimi ninajua hata Polisi wenyewe hawapendi kuongozwa na wanasiasa. Jeshi la Polisi liwe chombo huru kinachofanya kazi kwa weledi."
View attachment 3348661
CCM ni serikali na Serikali ni CCM.
 
Inakuwaje Polisi waongozwe na Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya ambaye ameelezwa wajibu wake ni kuhakikisha CCM inashinda?
Hilo suala la DC na RC kuwa kada/chawa wa ccm ni makosa makubwa sana.
Ingefaa hao wasiwe na upande (neutral), maana ni watumishi wa Watanzania wote.

Ndiyo sababu Katiba mpya ni muhimu sana kwa sasa ili kufanya marekebisho na kuondoa ujinga kama huo
 
KILIO MAKATIBU WA CCM WILAYA YA MKURANGA.

Chama Makao Makuu, mtusaidie SISI makatibu wa CHAMA na Jumuiya zake wilaya ya Mkuranga. Tumechoka kutumika.

Mbunge wetu anatulazimisha kufanya mambo kinyume na utaratibu wa Chama Chetu ili kumtafutia kura.

Mara kadhaa amekua anatulazimisha Kuwaita wajumbe kutumia kivuli cha semina elekezi, kumfanyia kampeni (yeye au mkewe) na kuwatisha kua atawashughulikia wanaompinga kutumia mamlaka yake.

Sasa TAR_*EHE 03.06.2025, Ametulazimisha, kuwaita wajumbe wote wa kamati za Utekelezaji kaka zote 25 na matawi yote 247 ya wilaya ya Mkuranga, watakua wajumbe zaidi ya 5000*_, kwa ajili ya semina elekezi, zote zifanyike siku moja na kila jumuiya ktk ukumbi wao. Lengo Kuu ni kuwapa maelekezo wamchague yeye uchaguzi ujao wa 2025, na apate fursa ya kuongea nao na kuwapa pesa ili awashawishi wamchague tena.

Mafunzo gani ya watu zaidi ya 5000?

*Kama hiyo haitoshi amekua anatulazimisha kupeleka viongozi na wanachama wale anoahisi hawamuungi mkono takukuru*_. Hadi sasa tushapeleka zaidi na wanachama/viongozi wa Chama Chetu zaidi 50 takukuru, kinachofanyika huko ni kutishwa na kutakiwa wamuunge mkono mbunge uchaguzi ujao, kwani yeye kiongozi Mkubwa na atawashughulikia wale wote wasiomuunga mkono.

Hali hii inaleta MPASUKO NA CHUKI KWA CHAMA CHETU WILAYA MKURANGA.

Mtusaidie.
 
Attachments

  • IMG-20250529-WA0002.jpg
    IMG-20250529-WA0002.jpg
    33.4 KB · Views: 8
Back
Top Bottom