Othman Masoud Aahidi Utumishi Uliotukuka

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
608
1,540
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Ndugu Othman Masoud Othman, amewaahidi viongozi pamoja na wanachama wa chama kuwa ataendelea kuitumikia nchi pamoja na chama ili kuona dhamira ya chama inafikiwa.

Mheshimiwa Othman ameyasema hayo katika ufunguzi wa kikao cha Kamati Kuu Chama ilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada iliyopo Ilala Boma jijini Dar es Salaam. Mara baada ya kutambulishwa kwa wajumbe wa Kamati Kuu ambayo ni mara yake ya kwanza kuhudhuria vikao vyake tangu kuteuliwa kumrithi aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, aliyefariki dunia Februari mwaka huu.

Ndugu Othman amesema imani aliyoipata kwa viongozi pamoja na wanachama katika kusimamia dhamira ya chama ndio njia pekee itakayomsaidia katika utendaji imara

Amesisitiza kuwa bado kuna nafasi kubwa kwa viongozi wa chama kuendelea kumuongoza katika utendaji wa kazi za kukiendeleza chama ili kuona mabadiliko katika taifa yanapatikana.

Aidha amewakumbusha viongozi pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu kuendeleza umoja na mshikamano ikiwa ni ishara ya kuendeleza mema yaliyoachwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Marehemu Maalim Seif.

Kikao cha Kamati Kuu kinachokusanya wajumbe 51 ni cha kwanza kwa mwaka huu wa 2021 na kimeitishwa kujadili maendeleo ya chama.

IMG-20210619-WA0017.jpg
IMG-20210619-WA0021.jpg
 
Back
Top Bottom