Oscar Pistorius Ni umaarufu, pesa, huruma au sheria?

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
10,344
14,117
“Sikudhamiria kumuua Reeva Steenkamp ila nilidhamiria kumuua yeyote aliyekuwa chooni. Nampenda Reeva, sikudhamiria kumuu. Hakuna hukumu katika mahakama hii ambayo unaweza ukalinganisha na kilichotokea(kifo cha Reeva). Nimeshajijutia mimi mwenyewe”. Ni maneno machache ambayo yalifanikiwa kutoka katika kinywa cha mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius wakati akijitetea mbele ya jaji Thokozile Masipa.
Oscar-Pistorius-and-Reeva-Steenkamp.jpg

Mnamo julai 6 mwaka huu nikiwa mbele ya televisheni yangu nilikuwa na huzuni iliyoje mara baada ya kumshuhudia mwanariadha mlemavu ninayempenda katika maisha yangu akiwa mahakama kuu jijini Pretoria nchini Afrika Kusini mbele ya jaji Thokozile Masipa akisikiliza hukumu ya mashtaka ya mauaji ya mchumba wake, Reeva Steenkamp yaliyotokea Februari 14, 2013. Pistorius alikuwa amepanda kizimbani huku akikabiliwa na kundi kubwa la watu nyuma yake ambao mara zote wamekuwa wakipingana katika mlolongo mzima wa usikilizwaji wa kesi hiyo.
south-africa-pistorius-18-752x501.jpg

Pistorius akiwa amevalia suti ya rangi ya kijivu muda wote alionekana akiwa ameinamisha kichwa chini kuzuia machozi ambayo mara zote alipokuwa akifikishwa mahakamani amejikuta akishindwa kujizuia na kuangua kilio kwa kile kinachoelezwa ni kujutia kitendo alichokifanya. Upande wa pili wa mahakama wazazi wa marehemu Reeva Steenkamp, Barry na June walikuwa kimya muda wote wakifatilia mwenendo mzima wa kesi hiyo ambayo imekuwa ikigusa macho na masikio ya watu wengi ulimwenguni kote.

Pistorius ambaye ni mshindi mara sita wa medali ya dhahabu katika mashindano ya Paralympics ikiwemo yale yaliofanyika jijini London nchini Uingereza Septemba 9, 2012 alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka sita jela huku mahakama ikitoa siku 14 kwa upande( mshtakiwa au serikali) ambao utakuwa haujaridhishwa na hukumu hiyo kukata rufaa. Hapo ndipo unapotimia msemo wa wahenga usemao; ‘Jela haina mwenyewe’.
Oscar-Pistorius-im_3549927b.jpg

Mara baada ya hukumu hiyo Pistorius alionekana akimkumbatia dada yake Aimee Pistorius nje ya mahakama kitendo kinachotafsiriwa kama kulidhishwa na hukumu aliyopewa. Hata hivyo hukumu hiyo imelalamikiwa na wakosoaji wengi huku wakidai umaarufu pamoja na uwezo wa kifedha wa Pistorius umechangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza ukubwa wa hukumu yake. Hapo ndipo linapokuja swali; ni umaarufu, pesa, huruma au sheria kilichoamua mustakabali wa kesi ya Pistorius?

Hata hivyo shutuma hizo zinapingwa vikali na jaji Masipa ambaye anasema kifungo cha muda mrefu kwa Pistorius si kigezo cha kuonesha haki imetenda huku akiwataka wakosoaji wa hukumu yake kutoa maoni lakini hayawezi kuchangia chochote katika mlolongo mzima wa usikilizaji kesi katika mahakama. Baadhi ya magwiji katika sheria wamelalamikia kifungo cha Pistorius huku wakimshutumu jaji Masipa kuwa hukumu yake ililenga kwa kiasi kikubwa katika kumhurumia Pistorius kutokana na ulemavu alionao badala ya kufuata sheria inayotoa kifungo cha chini cha miaka 15 kwa mtu anayepatikana na hatia ya kuteda kosa la mauaji.
5c4fae94dbadadc7c17a4be897a5ba2e

Jaji Masipa anasema hukumu yake imezingatia ushahidi wa tukio zima la kifo cha Reeva hivyo hukumu imekuwa ya haki kwa pande zote mbili yaani Pistorius na familia ya marehemu Reeva hususani wazazi wake. Hukumu hiyo ya Pistorius inakuja katika kipindi hiki ambacho nchi ya Afrika Kusini imekuwa ikikabiliwa na idadi kubwa ya matukio ya mauaji hivyo hukumu hii ya Pistorius imechukuliwa kama ni kiashiria cha kutokuzingatiwa kwa haki ya wale wanaokumbwa na matukio ya kuuawa.

Siku chache kabla ya hukumu, Pistorius alipokuwa amefikishwa mahakamani kwa ajili ya kutoa utetezi wake, alishauriwa na mawakili wake wanaomtetea kuvua miguu yake ya bandia ili kupata huruma ya jaji hasa ikizingatiwa ni mlemavu ambaye licha ya ulemavu wake amekuwa akishindana na kuiletea medali mbalimbali nchi yake. Je jaji Masipa alitumia utetezi huu wa Pistorius katika kutoa hukumu yake? Ukweli unabaki moyoni mwa jaji Masipa.
pistorius-e1466003445400.jpg

Pistorius ambaye February 14, 2013(siku ya wapendanao duniani) alimpiga risasi mara nne mchumba ake, Reeva Steenkamp mpaka kusababisha kifo chake mara zote amekuwa akijitetea hakudhamiria kumuua Reeva bali alifyatua risasi mara baada ya kudhani ni majambazi waliokuwa wamemuingilia kupitia upande wa chooni kumbe alikuwa ni mchumba wake Reeva aliyekuwa amekuja bila taarifa nyumbani kwake na kujificha chooni akilenga kumfanyia ‘surprise’ Pistorius.

Hukumu hii kwa Pistorius inachukuliwa kama ni ushindi kwake pamoja na jopo zima la mawakili waliokuwa wakimtetea na ndugu zake ambao kupitia kwa dada yake Aimee Pistorius wamemshukuru jaji Thokozile Masipa kwa hukumu dhidi ya ndugu yao. Upande wa pili wa wazazi wa Reeva Steenkamp, baba yake Barry Steenkamp ameonekana kutoridhishwa na hukumu hiyo huku akisema inaashiria mambo yamefika mwisho hivyo maisha hayana budi kuendelea japo maisha hayawezi kuwa sawa kama hapo mwanzo walipokuwa na mtoto wao( Reeva).
_74223668_ba046bfc-fc30-4325-8856-beff192fe939.jpg

Watetezi wa haki za wanawake nchini Afrika Kusini wamekuwa wakielezea mauaji haya ya Reeva Steenkamp kama kisa cha unyanyasi wa kijinsia dhidi ya wanawake kauli ambayo inakosa mashiko kutokana na kutokuwepo kwa ushahidi wa waziwazi unaoelezea kuwepo kwa ugomvi baina ya Pistorius na Reeva kabla ya kutokea kwa mauaji hayo. Mmoja wa mchangiaji katika kituo cha Radio 720 kilichopo ndani ya Afrika Kusini alikaliliwa akisema “ Afrika Kusini ni shamba la wanyama, baadhi ya wanyama wana haki kuliko wengine”.

Katika gazeti la kila siku la Maverick kulichapishwa makala ambayo ilikuwa na maneno yasemayo “ huu ni ushahidi wa muendelezo wa upendeleo kwa watu weupe. Nilishasema na sasa imethibitika Afrika Kusini ni nchi ambayo huwezi kupata unachotaka labda rangi ya ngozi yako iwe nyeupe na uwe na uwezo wa kulipa Rand 17.5million kwa mawakili”. Maneno haya yanaonekana kama ni mwiba mwingine katika nchi hiyo ambayo bado inapigana katika kutoka katika ubaguzi wa rangi kati ya waafrika kusini wenye rangi nyeupe wanaoonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha dhidi ya wale weusi ambao ni watu wenye uchumi wa kati.
2016-06-15t152402z_1_lynxnpec5e0yv_rtroptp_3_safrica-pistorius-800.jpg

Mjadala wa mwenendo mzimo wa kesi hadi kuhukumiwa kwa Oscar Pistorius utaendelea kusimama katika mkinzano wa kambi nne ambazo kila moja inaamini kesi hiyo ilizingatia upande wake katika kutolewa hukumu. Kambi ya kwanza inaamini kwa kiasi kikubwa umaarufu wa Pistorius ndio umechangia kupungua kwa ukubwa wa kifungo, huku kambi ya pili ikiamini katika uwezo wake wa kifedha. Kambi ya tatu inaamini huruma ya jaji Masipo pamoja na upendeleo kwa watu weupe ndivyo vilivyomsaidia Pistorius. Kambi ya nne inaamini ni sheria imefata mkondo wake. Je wewe unakubaliana na mawazo ya kambi ipi?:):):):):):)


C:\Users\user\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.jpg
C:\Users\user\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image004.jpg
 
Back
Top Bottom