Natoa pole sana kwa watanzania wote kwa ajali ya meli.ila naomba sana tuache tabia ya kusubiri tatizo ndiyo tujitokeze kinafiki tukishangaa na kutoa pole,jambo lililotokea la kukiuka taratibu ni kawaida sana kwetu wananchi na viongozi pia.
Sisi wananchi hatuna utamaduni wa kuheshimu sheria,mtu anataka tu awahi hata kwa kuatarisha maisha yake,hapo ferry kigamboni watu wanakufa kila mara kwa kukimbilia kivuko baada ya pantoni kupiga honi ya kuondoka,ndugu zangu tubadilike tuheshimu taratibu kwa ajili ya maisha yetu na tuwe wakali pale tunapoona wanakikuka utaratibu,mfano hao abiria walitakiwa kutoa taarifa kuwa boti limejaza kupita maelezo.
Kwa viongozi
acheni ukatili mnacheza na roho za watu kwa dhamana waliowapa wenyewe,kwani hamsimamii sheria mpaka litokee tatizo ndiyo mnakuja na sura zenu zenye majonzi ya unafiki mkubwa,mfano kwenye kivuko kilichoko mjini kabisa hapo kigamboni kuna watu wameajiriwa kama waokozi lakini likitokea tatizo hawaonekani,kamanga,busisi, mwanza na morogoro hali ni ile ile.naomba mamlaka husika mtubandikia namba za simu za maichaji husika ua viongozi husika kwnye hizi huduma za jamii
poleni watanzania na mungu awape afya njema majerui wote na awaleze pema marehemu,amen