Mkuu hao wote wameshakuona we ndio fursa ya wao kuendelea kiuchumi.
Tajiri anaandika ili amuuzie maskini, maskini ananunua kwa kutoa hata kidogo alichonacho akidhani atapata mafanikio kama tajiri kwa kusoma mavitabu tu.
Sasa kwa vile Billgate mzungu anatoa orodha ya vitabu anavyosoma na wewe kalumanzira ndo unaiga kichwa kichwa bila kufahamu haswa siri iliyoko nyuma ya mafanikio yake.
Hao wazungu ni wajanja sana wanacheza na uvivu wenu wa kufanya kazi na kujituma.
Wanatengeneza fursa kupitia kwenu.
Nawewe anza kusoma vitabu alafu baada ya miaka kadhaa tupe mrejesho kama umefikia hata asilimia sifuri kama sio hasi ya ukwasi wa hao wanaokuandikia vitabu
Fahamu, hao ni wajasiliamali wanaandika vitabu na kukuuzia wewe masikini ili usifanye kazi uendelee kununua vitu vyao
Sent using
Jamii Forums mobile app