Option ya Mifuko ya jamii kulipa madeni ya HESLB

jannelle

JF-Expert Member
Feb 8, 2020
536
1,003
Hi champions..
Currently Wengi wameongelea juu ya kuiomba serikali kuondoa riba ya 6%, Ile inayotozwa na bodi ya mikopo
ya elimu ya juu HESLB kwa kila mnufaika(per year),ikihusisha maumivu kwa kukua kila mwaka(ikizingatiwa ajira Ni ngumu kwa wapendwa wetu).

Bt nimewaza guys
Hatuwezi anzisha option ya kutumia akiba ya NSSF/PSSSF etc, katika kulipa madeni ya bodi ya mikopo hata kabla ya muda wa kustaafu?
God willing
 
Ni mpaka itokee marekebisho ya sheria iliyoanzisha mifuko hiyo. Inawezekana ikafanyika.
 
Hii naona ni nzuri hasa kwa waliochelewa kuanza kukatwa.

Sasa nani wa kutusemea haya kama wawakilishi wetu ndio hao wanateuliwa na serikali (dola) hiyo hiyo?
 
tatizo la wabunge wetu ni kupitisha sheria ambazo ni kandamizi bila kuangalia athari kwa wafanyakazi. Wanakuwa wakali tu pale ambapo wao wanaguswa maslahi yao tu.
 
Hiyo loan board haifai hata kuwepo, uroho wao wa pesa unawaletea mateso makubwa hawa vijana wa kitanzania wanaotafuta kesho yao kwenye elimu.
 
jamani kulipa hii hela ni pasua nkichwa..kila mwezi kukatawa 15% ya mshahara inaumiza mno...acha hiyo ya ongezeko la 6% kila mwaka....

hii 15% ya makato yanatupunguzia uwezo wetu wa kukopesheka...na maisha ya mwajiri bila mikopo hauwezi kusogea kabisa..
 
jamani kulipa hii hela ni pasua nkichwa..kila mwezi kukatawa 15% ya mshahara inaumiza mno...acha hiyo ya ongezeko la 6% kila mwaka....

hii 15% ya makato yanatupunguzia uwezo wetu wa kukopesheka...na maisha ya mwajiri bila mikopo hauwezi kusogea kabisa..
Kweli Kaka..changamoto sana
 
Kweli Kaka..changamoto sana
huwaga nikiwaza namna makato yalivyo mengi kwenye mshahara wangu huwa nanyongea kabisa...yani mwishow wa siku tunagawana gross salary sasa (50%)..na mishahara yenyewe ilivyo midogo basi
 
Je hiyo mifuko ina 'ubavu' wa kiuchumi na kisheria?
Tatizo ni HESLB!!!! Badru, hivi vilio ni juu yako.
Au ulitunga kwa hiari au kwa lazima.
 
Back
Top Bottom