Opinion: Uteuzi wa James Mbatia ni "Political Tactics, Strategies na Manouvering to Tame M4C?!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Opinion: Uteuzi wa James Mbatia ni "Political Tactics, Strategies na Manouvering to Tame M4C?!.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, May 4, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,320
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Uteuzi wa James Mbatia kuwa mbunge wa kuteuliwa ni kitendo tuu, wengi wanajadili matokeo ya uteuzi huo wakidhani Mbatia nae atapewa uwaziri wowote au unaibu, kiukweli, Mbatia hatapewa uwaziri wowote wala unaibu!.

  Watakaukwaa uwaziri ni Prof na Mama Mbene, Mbatia atabaki hivyo hivyo alivyo kwa kazi maalum!.

  Linapofanyika jambo, wengi hutazama matokeo ila wachache hujiuliza the motive behind uteuzi huo!. Kwa maoni yangu, Uteuzi wa Mbatia ni maandalizi ya replacement ya Mrema 2015 ili kuwazuia Chadema wasichukue jimbo!. Mrema is a spent force, by 2015 he will be too exorsted and worn out. Bunge la 1995, James Mbatia ndiye mbunge aliyeingia bungeni kwa kura nyingi sana, alishinda kwa kura 69,000 plus!. Kwa vile Moshi wanachagua mtu na sio chama, na CCM inajua wazi, haiwezi kiushinda Moshi mjini wala Vunjo, CCM wameamua kumset Mbatia kwa kumjengea momemtum ili Mrema asigroom successor na kwa vile ivumayo ni CDM, then kuuzuia sunami ya M4C ya CDM isiikumbe Vunjo!.

  Hizi zinaitwa long time political tactics, strategies na manouvering. Chadema kama wanaangalia mbali, wanatakiewa kiuanza kujipanga mapema kutengeneza possible line-up ya wagombea wao kwa 2015 ili wajioteshe mizizi kabla. Wakiambiwa hawajajipanga, wanakasirika!, CCM imechokwa ila inaanza kujipanga!. Sometimes simba aliyejeruhiwa ni hatari zaidi kuliko simba aliye fit!. CCM wamejeruhiwa vibaya Arumeru, wanasubiri kipigo Arusha!, hivyo wameanza kujipanga kujiweka vizuri kukomboa baadhi ya majimbo!. Mfano wameshajua jimbo la Moshi mjini, Ndesamburo hatagombea tena kwa sababu zile zile za Mrema kutogombea 2015. CCM inajua haiwezi kuchaguliwa hata kwa dawa, hivyo ili kulipoka jimbo la Moshi mjini toka Chadema, lazima li groom mtu kutoka NCCR ili kumzuia Ndesapesa kuweka Successor!.

  Haya ni maoni tuu!.

  Pasco
   
 2. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  sasa profesa atapewa vp wakati hatoapishwa mbaka bunge lijalo au unataka kusema JK ataitisha bunge maalum?? inamaana wizara itakaa kipindi chote bila waziri ili kumsubiri profesa aapishwe tu???? na Janet Mbene alikua mbunge wa viti maalum (Kinondoni) na namjua personally sasa huo uwaziri kwanini asimpe kipindi chote hicho?? ni mchumi mzuri tu!! acheni blah blah bwana! hatoki waziri kati ya hao!!
   
 3. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ni kama kuna ukweli vile! tusubiri tuone baraza kwanza.
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  This is a fantastic analysis. Keep it up! M4C iko imara sana.
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ni kweli.Siku za karibuni Pasco umepunguza unazi wako kwa CCM
   
 6. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu umenena, swala la kuwa na wagombea ambao wanaweka mizizi mapema jimboni ni muhimu sana. kitendo cha kupata mgombea vodafasta wakati wa uteuzi huwa si rahisi kupata mtu aliye makini na mwenye kukubalika na sehemu kubwa ya jamii ile. Ni lazima wagombea wakajenge chama majimboni kwao ili watu wawajue, siyo kukimbilia tu wakati wa uteuzi.
   
 7. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ok! ni maoni tu.
   
 8. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mie nashangaa kwani najiuliza kama unazi kwa lowassa umeisha kwa Pasco
  OTIS
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. g

  geophysics JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Usemayo yana ukweli ndani yake
   
 10. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na maoni yako Pasco na saa ingine ccm wanataka kihamishia watu kujadili inshu ya Mbatia wao wakapiga deal hapa kati, so far so good na doubt ikiwa mbatia pamoja na kushikwa mkono/jengewa momentum mapema hivi atalikomboa jimbo la Vunjo ama lolote
   
 11. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Labda kwa asiyejuwa lakini mbatia sio mpinzani siku nyingi watu wanajuwa hilo kama jk kafikiri hivyo kakosea
   
 12. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM hofu yao iko katika nafasi ya urais na sio ubunge, tena wa jimbo moja tu. JK hawezi kutimia nafasi yake ya kuteua mbunge kwa ajili ya jimbo ambalo hata hawajui mgombea wa CDM atakuwa nani. Nafasi hizi zinatumiwa kwa uangalifu sana ndio maana mpaka sasa bado ziko wazi. Mbatia ni mwenyekiti wa chama na bado ni kijana. Kwa kawaida wenyeviti wa vyama ndio wanakuwa wagombea. Mbatia amepoteza mvuto kwa wananchi lakini ameonyesha anaweza kuyamudu mapigo ndani ya chama chake. Ni dhahiri akiwa mbunge ataendelea kushika nafasi ya uenyekiti na hatimaye atagombania uraisi. Wanachofanya ni kujenga potential presidential candidates wengi kwenye kambi ya upinzani ili kugawa kura za upinzani na hatimaye mgombea urais wa ccm apate ahueni aweze kupita. Wanajua CCM haiwezi kuongeza kura hivyo ni bora kupunguza kura za CDM.
   
 13. B

  Bubona JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sina uhakika kama momentum hii 'anayojengewa' Mbatia itamsidia!! Mimi naona anamalizwa kisiasa! No one will trust him from now on!!
  Nakubaliana na hoja ya wagombea kujijenga mapema majimboni!!
   
 14. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Well said ningependa hii ndiyo iwe thread kuliko aliyoanzisha Pasco.
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,320
  Trophy Points: 280
  Mshauri aanzishe au muanzishie kwa sababu hakuna limits za kuanzisha thread!.
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,320
  Trophy Points: 280
  Jembe Ulaya, asante kunifungua macho kwa mtazamo huu nadhani hii sasa ndio inaweza kuwa the motive behind!.
   
 17. Petiro

  Petiro JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu jamaa alisema uchaguzi uliopita alitaka kugombea Vunjo ila akamheshimu babu Mrema maana alikua mgombea ila bila shaka huu ni mkakati wa kumweka tena kwny ramani ya siasa kwa manufaa ya magamba na maslahi yao binafsi. M4C kwa vunjo yapaswa ianze mapema na mtu mwenye kubaliwa maana lile jimbo linasifa kuu ya kuangalia mgombea zaidi ya chama
   
 18. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  John Mrema naamini ataipeperusha vyema bendera ya Chadema Vunjo. Ngoja tutapambana kumpa madiwani wakutosha. Kwa upandewa Moshi Mjini Mstahiki Meya Jaffari Michael inshallah yakiwa mapenzi yake Mola atatutetea wanyonge Mjengoni baada ya Ndesa-pesa.
   
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  NCCR wamepigwa magoti na rungu la polisi, kunyanyuka mara moja sijui, itawachukua muda.
   
 20. Vijijini Lawama

  Vijijini Lawama JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mi navyoamini mbatia hana lake tena kwenye siasa za Tanzania ngoja apewe ili naye apozee hapo uchungu wa kukosa jimbo la kawe
   
Loading...