Opinion: The State of Software Development in Tanzania

Am Kenyan to begin with, huu uzi muhimu sana ila naona ulikosa wachangiaji, ni uzi ambao ulifaa kujadiliwa kwa kina na wadau wote kuchangia maana kuna mengi ya kujifunza.
Mimi binafsi nimewahi kuhusika kwenye miradi ya huko kwenu Tanzania, ila kuna kitu kimoja nilishuhudia, samahani kama kuna mtanielewa vibaya, Watanzania hamdhamini developers wenu kabisa, (sio kwamba Kenya tuko 100% perfect, lakini huwa tunajaribu sana kuinuana).

Nilikua naona developers wa Tanzania wenye maujuzi tu, lakini hawachukuliwi serious na wateja, kwamba mteja Mtanzania akisikia developer ni mzungu, Mhindi au Mkenya, hapo anakua makini hata kwenye kulipa, lakini ikitokea developer ni Mtanzania, atazungushwa kwenye masuala ya malipo na kutokuchukuliwa serious kabisa, au mteja anaanza kubadilisha badilisha scope ya project kisa ameona mradi unafanywa na Mtanzania, lakini ukifanywa na mgeni, anakua makini na hazingui.

Haya nayazungumza out of experience, kitu ambacho nilikua nakiona kabisa, kwa mfano kuna mradi mmoja nilihusika hapo Tanzania ambapo tulikua na developers kutokea Marekani, jamaa wakaboronga na kufanya very shoddy job ila wateja ambao ni Watanzania hawakua wanaona issue, wanakubali yote tu, tukiingia kwenye vikao hawaulizi maswali wala kuhoji, yaani hadi kero, mimi nilikua nalazimika kufunga goli upande wetu, yaani inanibidi niwe na vikao vya siri na hao wateja ili kuwaelekeza waone mapungufu ya system na wahoji kwenye vikao, imagine mimi nipo kwenye timu na hawa Wamarekani lakini nakua na vikao vya siri na Watanzania ili kuwachochea wahoji mapungufu maana mimi nikihoji Wamarekani walikua wananijia juu.

Sasa mambo yaliendelea hivi hadi mradi ukaisha, wazungu wakapokeza documentations nyingi zenye misamiati ya kubabaisha, Watanzania wakatia saini kwamba mradi umeisha bila matatizo ilhali binafsi nilikua naona issues kibao lakini hakuna wa kuniskliza.
Waliporudi kwao, mradi ukapokezwa developers Watanzania wafanye maintenance, hapo sasa ndio shughuli ikaanza kuwa noma, maana wateja walizingua balaa, vikao baada ya vikao wanataja issues na kubadilisha badilisha scope, mambo ambayo waligoma kufanya wakati wazungu walikuwepo.
Kuna wafanyakazi mabogus wengi sana upande wa serikali linapokuja swala la IT - wanaweza kukubali au kuthamini kitu chochote bila kuquestion kwa sababu tu kimetengenezwa na mzungu! Kuna taasisi moja humu nchini ilitengenezwa mfumo na wazungu, mtanzania mmoja alipoifanyia auditing kwa kujitolea alikuta kuna security vulnerabilities na matatizo mengine mengi ya kimfumo, zaidi ya 100. Cha ajabu bosi aliyewakodi hao wazungu ili apige dili badala ya kuchukua ushauri akamchukia na kumletea visa.
 
Uzi mzuri sana na kwa kuongezea kuna vijana wa chache ambao wanafanya real programming wana design vitu matata , tatizo ni kqamba hata serikali yenyewe haiwapi support.
 
Back
Top Bottom