OPERESHENI Okoa Kusini ya CHADEMA yashika kasi

Pote CDM mnakopita nasikia mnapokea kadi za uanachama wa vyama vingine na kutoa kadi zenu; sijasikia mkitoa na katiba ya CDM kwa hao viongozi wanaochaguliwa? Hao wanaovunwa ukiacha msamiati wa UFISADI wanafahamu tofauti nyingine kati ya CDM na vyama vingine?
Rome was not built in a day!
 
MAFILILI ngoja nikusaidie kitu,kama ni kuijua mitaa ya Mtwara sawa unaijua baadhi.Jamani naomba mumsaidie huyu Mtu namna ya kufungua tawi,just imagin jana ndiyo wamefungua tawi leo wanaweza kupata Ofisi na kuanza kazi kweli?,alafu uliyotaja hiyo ni baadhi ya mitaa tu.Mie nakaa Railway ,amini nakuambia nafungua tawi na nagombea Udiwani na nachukua,Mpe salam hiz4 Mzee (Starehe) Omar
 
Usiwadanganye watu wa Mtwara hawataki kusikia CDM, jana wamejidanganya kufungua matawi, leo nimepita Ligula, Lilungu, Chikongora, Majengo, Vigaeni, Chuno, Magomeni, Rahaleo matawi yaliyofunguliwa jana, YAMEWEKWA BENDERA za CCM, Murji anatisha!
Kakojoe ulale!
 
Usiwadanganye watu wa Mtwara hawataki kusikia CDM, jana wamejidanganya kufungua matawi, leo nimepita Ligula, Lilungu, Chikongora, Majengo, Vigaeni, Chuno, Magomeni, Rahaleo matawi yaliyofunguliwa jana, YAMEWEKWA BENDERA za CCM, Murji anatisha!

Kama wewe unauhakika na ulichoandika hapa nijibu,Rahaleo mkutano walifanyia wapi ,waliongozwa na nani na hilo tawi walifungua wapi?,usichanganye watu tafadhari.
 
Mimi najiuliza, vyama vingine vyooooooote viko tuliiiii, CHADEMA ndio kila kukicha wanazunguka kufanya mikutano, hivi sheria ya vyama vya siasa inaruhusu haya mambo?
 
Rome was not built in a day!
Mlitika umeeleweka...USA Democratic wanajulikana wao wanatetea tabaka la chini Republican wao wanatetea uchumi mkubwa. CCM utambulisho wake ni wakulima na wafanyakazi; natamani nifahamu CDM utambulisho wenu ni nini?
 
Last edited by a moderator:
what a message,Mungu uliyeumba hii dunia na ukaaye mbinguni walinde hawa waja,na uwaepushe na hila zote mbaya za wale wanaowaangalia kwa jicho la husuda
 
Kama wewe unauhakika na ulichoandika hapa nijibu,Rahaleo mkutano walifanyia wapi ,waliongozwa na nani na hilo tawi walifungua wapi?,usichanganye watu tafadhari.

Nabwada siyo kufanya malumbano; Kesho asubuhi tuwe pamoja kwa Shilingi tupate supu. CCM Mtwara haina mpinzani zaidi ya CUF ambao kwa kiasi fulani wanajikongoja kwa kutumia misikiti.

Ukweli hapa Mtwara vyama vinashika nafasi kama ifuatavyo:-
1. CCM 80% wapiga kura
2. CUF 12% wapiga kura
3. NCCR Mageuzi 5%
4. CHADEMA, UDP, TLP, TADEA, NLD, UPDDP, Demokrasia Makini 3%
 
Baada ya jana kufanya mikutano ya hadhara, kufungua matawi na kuweka uongozi wa muda kata zote 15 za Wilaya ya Mtwara Mjini, leo Operesheni Okoa Kusini imeingia vijijini.

Ratiba ya leo Wilaya ya Mtwara Vijijini ni ifuatavyo: Timu ya Mwenyekiti Freeman Mbowe itakuwa Kata za Madimba na Tangazo, Timu ya Makamu Mwenyekiti Said Mohamed Issa itakuwa Kata za Msanga Mkuu na Ziwani, Timu ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa itakuwa Mtimbilimbwi na Nanyamba, Timu ya John Mnyika itakuwa Nanguruwe na Mayanga, Timu ya Tundu Lissu itakuwa Nitekela na Milangominne, Timu ya John Heche itakuwa Bilimba na Mnima, Timu ya Godbless Lema itakuwa Mtinjiko na Mbembaleo, Timu ya Ezekia Wenje itakuwa Kata za Kitere na Libobe.

Kazi ni ile ile mikutano ya hadhara, mikutano ya ndani, kufungua matawi, kusimika uongozi wa muda kuelekea uchaguzi wa ndani kuanzia Juni 1 mwaka huu!

Kujenga oganaizesheni ya chama kuanzia vijijini mpaka mjini, kueneza elimu ya uraia, hasa suala la katiba mpya, kuendelea kudai uwajibikaji wa serikali kwa wananchi katika ngazi zote hasa ktk kushughulikia vyanzo vya matatizo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, yanayoikabili nchi kwa sasa, badala ya kushughulikia matokeo ya matatizo hayo kama inavyofanywa na serikali ya CCM hivi sasa.

Mkuu n00b,

Tunashukuru kwa taarifa... Zaidi mtutumie Picha wana CCM waone jinsi harakati za kuikomboa Tanzania zinavyofika Mwisho...

Washauri Chadema waendelee na Mikutano hiyo ila Maoni ya watu wengi hapa Dar ni kuwa tar 27 kina Tundu lisu. Dr Slaa na Mbowe pamoja na makamanda wetu wengine hawakupata muda wa kutosha...
 
Mlitika umeeleweka...USA Democratic wanajulikana wao wanatetea tabaka la chini Republican wao wanatetea uchumi mkubwa. CCM utambulisho wake ni wakulima na wafanyakazi; natamani nifahamu CDM utambulisho wenu ni nini?
Ndachuwa; CHADEMA = Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Demokrasia = Utawala wa watu (Umma) na kwa ajili ya watu.
Maendeleo = Kujikwamua kutoka hali duni katika nyanja zote kimaisha kuelekea katika hali bora. Pakiwepo demokrasia ya kweli hakuna anayebaguliwa wala anayefaidi wengine waachwa.

Hii ndiyo tofauti ya CHADEMA na CCM. CCM haipiganii tena maendeleo ya hao wakulima na wafanyakazi Hiki ni chama cha kuwafaidisha na kuwalinda wachache (mafisadi) na adui wao mkubwa ni DEMOKRASIA (tuseme ukweli jamani). Hakuna demokrasia ndani ya CCM namna ya kugombea uongozi (hata wa ndani ya chama); hakuna demokrasia ndani ya CCM katika Tume ya Uchaguzi, jeshi la polisi na sasa hata mahakama.

CHADEMA ina dhamira ya dhati ya kuondoa uozo huu ndani ya nchi hii badala yake kujenga jamii ya kidemokrasia inayotafuta maendeleo ya kweli.
 
Back
Top Bottom