OPERESHENI Okoa Kusini ya CHADEMA yashika kasi

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Baada ya jana kufanya mikutano ya hadhara, kufungua matawi na kuweka uongozi wa muda kata zote 15 za Wilaya ya Mtwara Mjini, leo Operesheni Okoa Kusini imeingia vijijini.

Ratiba ya leo Wilaya ya Mtwara Vijijini ni ifuatavyo: Timu ya Mwenyekiti Freeman Mbowe itakuwa Kata za Madimba na Tangazo, Timu ya Makamu Mwenyekiti Said Mohamed Issa itakuwa Kata za Msanga Mkuu na Ziwani, Timu ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa itakuwa Mtimbilimbwi na Nanyamba, Timu ya John Mnyika itakuwa Nanguruwe na Mayanga, Timu ya Tundu Lissu itakuwa Nitekela na Milangominne, Timu ya John Heche itakuwa Bilimba na Mnima, Timu ya Godbless Lema itakuwa Mtinjiko na Mbembaleo, Timu ya Ezekia Wenje itakuwa Kata za Kitere na Libobe.

Kazi ni ile ile mikutano ya hadhara, mikutano ya ndani, kufungua matawi, kusimika uongozi wa muda kuelekea uchaguzi wa ndani kuanzia Juni 1 mwaka huu!

Kujenga oganaizesheni ya chama kuanzia vijijini mpaka mjini, kueneza elimu ya uraia, hasa suala la katiba mpya, kuendelea kudai uwajibikaji wa serikali kwa wananchi katika ngazi zote hasa ktk kushughulikia vyanzo vya matatizo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, yanayoikabili nchi kwa sasa, badala ya kushughulikia matokeo ya matatizo hayo kama inavyofanywa na serikali ya CCM hivi sasa.
 
hii ni kama operation sangara, hongereni.....yuel M/Mweti wa bavicha yeye anaenda wapi?
 
Huu ndio wakati muafaka wa kuwaandaa watanzania kwa ajili ya katiba mpya na uchaguzi wa 2015.
CCM walikuwa wanajidai kujulikana sana vijijini lakini sasa mtaji huo umekwisha na Chadema wameweza kufika mpaka vijijini na kuwaonesha wananchi kuwa si chama cha mjini pekee kama baadhi ya watu wanavyozusha.
Hongera makamanda wote na hakula kuchoka mpaka kieleweke.
 
NA UWEZEKANO MKUBWA CCM IKAWA CHANZO CHA KUCHOMWA MAKANISA ILI KUWAGAWA WATANZANIA,WALIANZA KWA KUWAPAKA MATOPE CUF BAADA YA KUUNGANA NAO WAKAHAMIA CHADEMA ETI UDINI WAKASHINDWA SASA UKASKAZINI NINA WASIWASI KUNA MKONO WA CCM:israel:
 
Mungu awape nguvu na afya njema Makamanda, kazi mnayoifanya si bure,
Mmejitolea kwa ajili ya watanzania wote,
Mbarikiwe!!
 
Timu ya Nape itakuwa Nungwi na timu ya lukuvi itakuwa mwnakwerekwe! Pia timu ya Wasira itakuwa arumeru, bila ya kusahau timu ya lusinde itakuwa Uamshoni!

Operation vaa Uzalendo choma makanisa!
 
Ukaskazini hawataintetain tena,nape amenambia leo kuwa hawajui watoke vp baada ya makamanda kutinga kusini
 
Baada ya jana kufanya mikutano ya hadhara, kufungua matawi na kuweka uongozi wa muda kata zote 15 za Wilaya ya Mtwara Mjini, leo Operesheni Okoa Kusini imeingia vijijini.

Ratiba ya leo Wilaya ya Mtwara Vijijini ni ifuatavyo: Timu ya Mwenyekiti Freeman Mbowe itakuwa Kata za Madimba na Tangazo, Timu ya Makamu Mwenyekiti Said Mohamed Issa itakuwa Kata za Msanga Mkuu na Ziwani, Timu ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa itakuwa Mtimbilimbwi na Nanyamba, Timu ya John Mnyika itakuwa Nanguruwe na Mayanga, Timu ya Tundu Lissu itakuwa Nitekela na Milangominne, Timu ya John Heche itakuwa Bilimba na Mnima, Timu ya Godbless Lema itakuwa Mtinjiko na Mbembaleo, Timu ya Ezekia Wenje itakuwa Kata za Kitere na Libobe.

Kazi ni ile ile mikutano ya hadhara, mikutano ya ndani, kufungua matawi, kusimika uongozi wa muda kuelekea uchaguzi wa ndani kuanzia Juni 1 mwaka huu!

Kujenga oganaizesheni ya chama kuanzia vijijini mpaka mjini, kueneza elimu ya uraia, hasa suala la katiba mpya, kuendelea kudai uwajibikaji wa serikali kwa wananchi katika ngazi zote hasa ktk kushughulikia vyanzo vya matatizo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, yanayoikabili nchi kwa sasa, badala ya kushughulikia matokeo ya matatizo hayo kama inavyofanywa na serikali ya CCM hivi sasa.

Ni mara chache utakuta post NZURI kama hii! What a consoling message! Kweli makamanda wamejipanga. It really warms my heart! Thanx n00b for such a wanderful post!
 
Back
Top Bottom