Operation Zinduka: Kielelezo cha ujinga wetu?


Nostradamus

Nostradamus

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2009
Messages
393
Likes
0
Points
0
Nostradamus

Nostradamus

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2009
393 0 0
Naomba msinichukulie kama mkosoaji wa kila kitu,ila katika mambo ya msingi watanzania tumedhihirisha udhaifu uliokithiri.ajabu!! hata afya zetu na wanetu tunaleta siasa na ufisadi!!??
Nilikuwa nafuatila kwa ukaribu uzinduzi wa mkakati mpya wa kitaifa wa kupambana na maleria,nilitarajia mkakati huu utakuja na suluhisho juu ya jinsi ya kupambana na hili janga linalotishia uhai wa kizazi hiki.lakini kwa mshangao mkubwa nilishuhudia yaleyale ya siku zote.(usanii,unafiki,na siasa.)
Ukitaka kujua hata wahusika hawakuwa makini na tukio zima hebu ona moja kati ya kauli mbiu zao....'' sisi ndio tuwe kizazi cha mwisho kufa kwa maleria''
Hata bila utaalamu wa lugha,hiyo kauli haiendani na mkakati wao kwa maana kauli mbiu yenyewe inatutaka hata sisi wenyewe tufe kwa maleria japo tutakuwa ni kizazi cha mwisho kufa kwa maleria.
Nadhani kauli sahihi ingekuwa''sisi ndio tuwe kizazi cha kwanza kutokufa kwa maleria.
Haya mambo tuwaachie wataalamu wa lugha na turejee kwenye mada ya msingi.Wakati nakua(bahati nzuri nimekulia katika miji yote ya pwani,mtwara,lindi,mafya,dar,tanga na zanzibar),palikuwa na operation maalum ya kupambana na maleria kwa kuangamiza vyanzo na mazalia ya mbu.nilishuhudia kwa macho yangu watu wakipita na mitungi iliyo na dawa mgongoni na kupuliza maeneo yote kama kwenye chambers za maji,madimbwi,mifereji n.k.
Hii ilisaidia sana kuangamiza mazalia na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya mbu na hivyo kupunguza kiwango cha wagonjwa na hata vifo vinavyosababaishwa na maleria.
Kinachodhihirisha ujinga wetu ni namna ambavyo tunapambana na maleria katika zama hizi.
Hatumuongelei mbu na jinsi ya kumuangamiza bali tunaongele jinsi ya kumzuia asituume.Damn,,,, how can we do that?????kwa ujumla huu ndio mtazamo wangu katika swala zima la maleria.
1.Kiasi alichotoa rais mstaafu wa america Georg W Bush kufadhili mapambano dhidi ya maleria,kingetosha kabisa kuangamiza mbu na vizazi vyao katika maeneo yote ya nchi hii kuanzi vijijini ndani kabisa mpaka mijini.Lakini kwa sababu ya ufisadi wa kitanzania,fedha zote zimepelekwa katika utengenezaji wa vyandarua na uingizaji wa madawa ya kutibu maleria.amini nakwambia,hii miradi miwili ya vyandarua na uingizaji wa madawa ya kutibu maleria ina husisha vingozi wakubwa kabisa serikalini kama miradi yao binafsi.
2.Hakuna ukweli(nina uthibitisho na anayebisha niko tayari kumthibitishia) kuwa vyandarua wanavyovitangaza kuwa vina dawa inayodumu miaka mitano.Vyandarua hivi si lolote si chochote kwani usipokuwa makini ya jinsi ya kuweka chandarua chako, asubuhi utakuta mbu wamejaa ndani ya neti wakiwa wameshiba na hakuna hata mmoja aliyekufa.
3.Kampeni imelenga kushawishi watu wanunue vyandarua(marketing) kuliko kushawishi watu wajilinde dhidi ya mbu.

Labda nihitimishe kwa kusema,Rais mstaafu wa marekani Bill Clinton alikuwa ni swahiba mkubwa wa Ben Mkapa kupitia AIDS foundation,na mpaka sasa Ben Mkapa ni tajiri wa kutupa kupitia hiyo foundation(kumbuka foundation yake ndio wakala wa ARV na akiwa rais alihakikishaserikali zote za kiafrica zinanunua ARV na kuzigawa bure kwa wananchi wake).Bill Clinton ana kiwanda cha kutengeneza ARV. hebu ona jinsi viongozi wetu wanavyotajirika kupitia vifo vyetu.
Nachelea kusema kuwa Rais Kikwete anapitia njia ileile ya Mkapa kwa kupitia mlango wa maleria.Kwani uswahiba wake na Bush ni replica ya uswahiba wa Mkapa na Clinton.
simple mathematics
CLINTON+MKAPA= AIDS
BUSH+KIKWETE= MALERIA

Ukijaribu ku intergrate from the first principle jibu utakalopata linatisha haswa ukizingatia wanaofanya hivyo ni viongozi wetu walioingia madarakani kupitia sanduku la kura na wala sio mapinduzi ya kijeshi.
labda nikudokeze tu kuhusu jibu nililopata(vifo vyetu=neema kwao)

Nawasilisha,,,
 

Forum statistics

Threads 1,250,964
Members 481,523
Posts 29,752,625