Operation Cointelpro

Operation Cointelpro

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
362
Reaction score
906
"OPERATION COINTELPRO" OPERESHINI MAALUM ILIO SUKWA NA FBI, ILIINJINIA VIFO VYA MALCOM X NA MARTIN LUTHER KING Jr, WANAHARAKATI WEUSI WASIO SAULIKA.

Na.Comred Mbwana Allyamtu
Friday -28/6/2019.
Dakawa, Mvomero, Morogoro -Tanzania

Siku chache zilizopita rafiki yangu Bahati Samwel aliweka makala humu iliyo mzungumzia Malcolm X, ambayo ilikwenda kwa jina la "Malcolm X Mmarekani mweusi aliyeishi bila uhuru na akafa bila uhuru" kufatia makala hiyo nimeona ni vyema tukafahamu sababu iliyopelekea kifo chake, nje ya Malcolm X pia tutatazama kifo cha Martin Luther King Jr na namna operation hii Cointelpro ilivyo husika.

Vifo vya watu hawa avikuwa vya bahati mbaya bali vilisababishwa na sababu za kitaifa (national security Interest) vifo hivyo kwa sehemu kubwa vilipangwa na aliyewahi kuwa mkurugenzi wa FBI bwana John Anthony Hoover, huyu bwana ndie aliyetoa mchango mkubwa katika kuijenga taasisi hiyo ambayo ilishiriki pakubwa katika kufanikisha mipango kadhaa kufatia kuwadhibiti wanaharakati kadhaa nje na ndani ya Marekani, huyu bwana anatajwa kama mtu aliyeogopwa sana akifanya kazi kinyume cha sheria hadi kufikia hatua ya kuogopwa hadi na Marais wa Nchi yake!

Kifo cha Malcolm X na Martin Luther King Jr ni mkakati maalumu uliopangwa kupitia opareshen maalumu iliyofanyika katika utawala wa bwana Hoover, jasusi na mkurugenzi wa FBI, ambae ndie aliye panga mipango yote ya utekelezaji wa Operation ya kuuwawa kwa wanaharakati hao, Hoover alilatibu mkakati maalumu uliopewa jina ''Operation Cointelpro" operation hii iliwalenga wanaharakati wote maarufu wa haki za watu weusi katika taifa hilo ambao walitazamwa kama watu hatari kimkakati katika usalama wa taifa hilo hivyo walitakiwa kupoteza maisha kwa kupigwa risasi.

Oparesheni COINTELPRO ambayo iliratibiwa kuanzia mwaka 1957 hadi mwaka 1971. Operation hii ilipewa code ya Cointelpro lilitokana na jina "COUNTER INTELIGENCE PROGRAM" jina lilo manisha (BLACK NATIONALIST,-HATE GROUPS)

Operation Cointelpro yenyewe......

Operation hii ilikuwa ni moja ya mfululizo wa oparesheni za siri za shirika la upelelezi la Marekani (FBI) uliolenga katika kufuatilia, kujipenyeza, kuzuia na kuyashushia hadhi makundi au watu wote walioonekana kuwa kinyume na Sera za serikali ya Marekani ndani ya nchi hiyo! kama nilipo elewa hapo nyuma ni kwamba COINTELPRO yenyewe imefupishwa kutoka kwenye maneno Counter Intelligence Programme.

Oparesheni hii ilianza mwaka 1957 ikiwa chini ya mkurugenzi John Anthony Hoover, ikisimamiwa kwa karibu na bwana William C.Sullivan akisaidiana na Bwana Robert F. Kennedy ndugu yake Rais Jonny F. Kennedy ambaye yeye alikuwa mwanasheria mkuu wa Marekani kipindi hicho Operation hii ilijikita katika kuwafichua, kuzuia, kupotosha, kushusha hadhi, kudhoofisha na ikiwezezekana kuyafuta makundi yote na watu wote walioonekana kuwa na misimamo kinzani na serikali ya Marekani kwa kutumia njia za kiharamia kama kutengeneza nyaraka za uongo, habari za uongo na kupotosha kuhusu watu au makundi hayo, watu kupigiwa simu zisizojulikana, kutegewa vifaa vya kurekodia, kupandikiza chuki baina ya makundi hayo, kijipenyeza ndani ya makundi hayo na kutengeneza woga baina ya wafuasi, kukamata watu ovyo, kupika ushahidi na wakati mwingine hata kuwaua wahusika wa makundi husika.

Makundi yaliyolengwa zaidi yalikuwa kama vile the Black Power movements( The Southern Christian Leadership Conference ya Martin Rurther King Jr.), the Black Panthor Party( kundi lilikuwa likitumia nguvu dhidi ya vyombo vya usalama!) na kundi la Ku Klux Klan, makundi yote haya kwa nyakati tofauti yalionekana kama tishio katika usalama wa taifa la Marekani hivyo kupelekea.

Operation hii "COINTELPRO" haikuishia wa watu weusi na wale wenye misimamamo mikali tu peke yao bali ilianza kutumika pia kama silaha ya kisiasa na ilipata baraka za uongozi wa juu wa serikali ya Marekani kipindi hicho na ndio inayoweza kuwa sababu iliyowafanya karibia marais wote waliofanya kazi na Hoover kumuogopa mno na hata kushindwa kumfuta kazi pale walipoona hafanyi vile ambavyo wangependa kuona anafanya hali iliyomfanya Hoover aiongoze idara hii kwa mda mrefu hadi alipofariki dunia mwaka 1972

Kwa mfano kipindi cha utawala wa Rais Jonson aliwahi kuwataka FBI kufanya utambuzi wa majina wa watu wote waliokuwa wakikosoa utawala wake wakiwemo maseneta, hasa hasa Seneta Barry Goldwater na wasaidizi wake wote hii ilikuwa ni kosa katika sheria za ndani za Marekani hasa sheria ile ya Congress privacy and special security Act ambayo inazuia rais kudukua taarifa za wabunge (wawakilishi) na maseneta wa taifa, kufatia hatua hiyo ilipelekea raisi Lyndon Johnson kushindwa kumshugurikia Hoover hata pale walipo pishana kutokana na Hoover kushika mpini ambao ungeweza kumuweka pabaya Rais Johnson.

Pia Raisi Flanklin Roosevert yeye aliwahi kuwataka FBI kuweka kwenye faili majina ya raia wote waliokuwa wakimtumia telegramu kupinga Sera zake za ulinzi, ili aweze kuwashughrikia jambo ambalo ni marufuku katika sheria za Marekani pia. Hii pia ilikuwa ni mpini kwa Hoover dhidi ya Rais Roosevelt. Hali hii pia ilijitokeza katika utawala wa Kennedy watu mbali mbali waliwekewa vifaa vya kurekodiwa wakiwemo viongozi ndani ya baraza la Congress jambo ambalo linakioluka sheria za haki kwa usalama wa viongozi wa Marekani.

Kifo cha "Malcolm X" chini ya Operation Cointelpro......

Malcom Little maarufu kama Malcom X alifariki February 21 mwaka 1965 baada ya kupigwa risasi na mtu anayesemekana kuwa mfuasi wa kundi la "The Nation Of Muslims" ambalo kabla ya kifo chake yeye mwenyewe alikuwa mwanachama na kiongozi kabla ya kutofautiana! Aliingia kwenye harakati baada ya kutoka jela mwaka 1952, alifungwa baada ya kushitakiwa kwa kosa la wizi na akiwa jela ndipo alipopata mafunzo ya dini ya kiislam na baadae akawa ni mmoja wahamasishaji na viongozi wakuu wa kundi la Nation Of Muslims ambalo wakati anafariki alikuwa ametofautiana nalo sana na kukawa na mgogoro mkubwa kati yao. Kabla ya kifo alikuwa amepokea vitisho vingi sana na wakati fulani nyumba yake ilichomwa moto.

Huyu Malcolm X alizaliwa kama Malcolm Little Mei 19, 1925 huko katika mji wa Omaha, Nebraska. Baba yake, Earl Little alikuwa mchungaji asiyeogopa kusema ukweli, na pia alikuwa msaada mkubwa sana wa kiongozi wa Harakati za Weusi (Black Nationalist) wakati huo, Marcus Garvey. Malcolm X alilelewa katika imani ya kisabato na mama yake katika makuzi yake.

Maisha ya Malcolm mwanzoni yalikumbwa na masaibu mengi. Kwa mfano, mwaka 1929 nyumba yao iliyopo Lansing, Michigan ilichomwa moto na kundi la wazungu lenye chuki alikuwa na umri wa miaka sita tu wakati baba yake alipokufa katika kifo kibaya sana, mama yake akawekwa katika hospitali ya watu wenye matatizo ya akili (mtindio wa ubongo), kisha Malcon X akachukuliwa kwenda kulelewa katika vituo vya kulelea watoto wasio na uwezo.

Mwalimu wake alivunja ndoto zake za kuwa mwanasheria, alimwambia kazi hiyo haiendani na maniga (weusi), akamuusia awe fundi seremala akimsisitiza hata Yesu alikuwa seremala. Akaacha shule japokuwa alionesha ana uwezo mkubwa wa akili, akatumia sasa muda wake mwingi Boston, katika jimbo la Massachusetts kufanya kazi za ajabu ajabu, japokuwa kazi yake ya mwanzo ilikuwa kung’arisha viatu, akasafiri kuhamia Harlem, New York ambapo huko akafanya uhalifu sana, kabla ya mwaka 1942, alikuwa mwongozaji vikundi vya madawa ya kulevya, umalaya, ukahaba, na kamari, na ilipofika mwaka 1946, alihukumiwa kwenda jela kwa miaka 10 kutokana na kukutwa na kosa la ujambazi (wizi wa kuvunja nyumba).

Malcolm X alijiongezea elimu yake wakati yuko jela. Ilikuwa humo humo gerezani ndio ambapo aliimeza Dictionary (aliihifadhi kichwani kamusi ya kiengereza yote), alisoma Biblia na kila kitu kuanzia somo linalohusu mabaki ya kale (Archeology) mpaka Somo la Uzazi na Kurithiana (Genetics). Wakati yupo humo gerezani, Malcolm akafata imani ya muislam mweusi na baada ya kuachiwa kutoka gerezani, akawa mjumbe katika Chama cha Waislamu Weusi (Nation of Islam) na kuchaguliwa kuwa msemaji wao. Nation of Islam ni kundi lilopotoka linalojinasibisha na Uislamu wa mtu mweusi.

Lakini baadae Malcolm X alijitoa toka katika kundi la Nation of Islam mwaka 1964 na kuanzisha kundi lingine liitwalo Muslim Mosque, Inc na pia akaunda Chama cha Umoja wa Wamerika Weusi (Organization of Afro-American Unity), kundi ambalo linatetea uzalendo wa watu weusi.

Baadhi ya Waislamu wa Kisunni walimuusia sana Malcolm kuusoma Uislam wa kweli. Malcolm X alikubali ushauri ule ambao ukamfanya ajiungue kutoka katika Nation of Islam na baadae kukiri kwa maneno yake kwamba “Katika chuo kimoja na kengine ambapo nilipita kuongea katika mikutano isiyo rasmi, wengi kati ya watu weupe wamekuwa wakinifata wakijitambulisha kama waarabu, wa Mashariki ya Kati, au wanatoka kaskazini mwa Afrika na wapo hapa kimasomo, kikazi au wengine wana makazi ya kudumu. Wakawa wananiambia pamoja na maneno yangu ya kuwachukia wazungu, ni kweli sikosei ninavyojichukulia kuwa ni Muislamu lakini walihisi niusome vizuri Uislamu, nitauelewa na kuukubali. Kama mfuasi wa Elijah (kiongozi wa Nation of Islam), nilikasirishwa na walichokuwa wakinisema.

Lakini baada ya hali hii kujirudia kwa muda, nikajiuliza mwenyewe, kama kweli mtu yuko kidhati katika kuitangaza na kuifata dini hii, iweje mtu arudi nyuma katika kujiongezea maarifa ya kuijua dini hiyo zaidi na zaidi?!…”

Mmoja wa hao Waislamu waliojitolea alikuwa Dkt. Mahmoud Youssef Shawarbi ambae nae aliongozwa na kauli ya Mtume “Mmoja wenu hawezi kuamini mpaka ampendelee mwenzake kile akipendacho nafsini mwake.”alimshauri Malcolm X kuukubali uislam wa kweli.

Baadae Malcolm alifunga safari kwenda kuhiji Makkah ambapo aliugundua uislam wa ukweli na akawa muislam wa Kisunni akatoa shahada upya (mwenyewe) na kubadili jina lake kuwa Al-Hajji Malik Al-Shabbazz. Malcolm alikuwa na furaha baada ya kukamilisha Hijja yake akisema amefurahi kuwa mweusi wa kwanza kwa wazaliwa wa Marekani kuhijji.

Siku zake za kuhiji zilileta mabadiliko kuhusu msimamo wake wa kuchukia weupe. Akasema “Kulikuwa na makumi elfu mengi ya mahujaji kutoka sehemu mbalimbali duniani, walikuwa watu wa rangi zote, kuanzia wale wazungu wenye macho ya rangi ya samawi mpaka Waafrika Weusi.

Lakini wote tulikuwa tukishiriki katika ibada kuonesha imani ya mshikamano na umoja ambayo katika maisha yangu ya Marekani sikuwahi kuota kuwa itawezekana…Amerika inapasa kuufahamu uislam, kwa sababu hii ndio dini iliyoondoa tatizo la ubaguzi wa rangi katika jamii wakati dini hii iliposhushwa. Katika kuzunguuka kwangu katika mataifa ya Waislamu nimekutana, nimeongea na hata kula pamoja na watu ambao Marekani walikuwa wakichukuliwa ni weupe (wazungu). lakini kwa hawa ile tabia chafu ya kibaguzi ya uweupe imeondoshwa katika fikra zao kwa Uislamu wao. Sijawahi kuona kabla, upendo huu wa dhati ambao hawa wanautekeleza bila kuzingatia tofauti zao za rangi.”

Wakati akiwa Hijja, aliandika barua kwa wasaidizi wake wa chama chake kipya (Muslim Mosque) kule Harlem na kuwaomba wazisambaze kwenye vyombo vya habari. Aliandika, “Sijawahi kushuhudia ukarimu mkubwa na roho ya udugu wa kweli kama niliouona ule wa rangi zote kule ardhi takatifu, nyumba ya Ibrahim, Muhammad na mitume wote waliopita. Kwa wiki nzima sikuwa mzungumzaji ila ni kushangazwa tu kwa yale mapenzi yalioneshwa kwangu na wale watu wenye rangi tofauti….najua mnaweza kushangazwa na maneno haya yanayotoka kinywani mwangu.

Ukweli hijja hii, imenilazimisha kubadili fikra zangu ambazo zilikuwa zimejaa mwanzoni na sasa nimeamua kutumia upande mwengine wa shilingi kwa baadhi ya mambo niliyokuwa nayaamini. Hili halijakuwa gumu kwangu. Japokuwa nimekuwa nikiiamini imani yangu kidhati, siku zote nimekuwa mtu mwenye kujaribu kukumbana na ukweli, na kuukubali uhalisia wa maisha.

Siku zote nimekuwa ni mwenye kukiwacha kichwa changu wazi ili kiweze kwenda mkono kwa mkono na utafutaji mzuri wa ukweli. Katika kipindi cha siku hizi kumi na moja zilizopita, nimekula chakula kutoka katika sinia moja, nimekunywa kwa kutumia bilauri moja, na nimelala katika sehemu moja huku tukiabudu kuelekea kwa Mungu mmoja- pamoja na Waislamu wenzangu, ambao macho yao ni ya rangi ya kisamawati kuliko! Wenye nywele zenye umanjano kuliko! Na wenye ngozi yenye weupe pe! Ila kwa maneno na matendo ya Waislamu hawa weupe, nimejihisi kama niko pamoja na wenzangu (Waislamu weusi) kutoka Nigeria, Sudan na Ghana.

Kwa kweli kila mtu alikuwa kaka wa kweli kwa mwenzake, kwani ile imani ya kuabudia Mungu mmoja imeondoa kule kujiona kutoka vichwani mwao, kutoka tabia zao na hata kutoka katika hulka zao. Nimeona kweli kama wazungu wa Marekani wangekubali kuabudia Mungu mmoja basi bila shaka wangekubali umoja wa binadamu pia kuepuka kuwadhuru wenzao kwa sababu ya tofauti rangi tu. Kwa ubaguzi huu unaoenea Marekani kama saratani isiyo na tiba, tulitegemea wale wazungu wanaojiita wana mioyo ya kristo basi wangelivalia njuga tatizo hili kwa kufanya harakati za kulitokomeza.

Huu ndio ulitakiwa uwe muda mahsusi wa kuiokoa Marekani kutokana na janga hili kubwa janga lililoimaliza Ujerumani baada ya kuwamaliza Wajerumani wenyewe. Waliponiuliza kuhusu lipi lililokuvutia katika Hijja nikajibu ni huu udugu wa kweli, watu aina tofauti, wenye rangi tafauti, tokea maeneo tofuati duniani wanakuja kukaa pamoja na kuwa kitu kimoja! Kwa kweli jambo hili limenionesha nguvu za Upekee (U-moja) wa Mungu. Wote tumekuwa tukila kimoja, tukilala sehemu moja, kila kitu tulikifanya kwa pamoja katika kumuelekea Mungu mmoja.”

Malcolm X akarudi kutoka Hijja akiwa mtu tofauti, akiwa yuko katika silika yake ya asili kama alivyo mtoto asiye na dhambi hata kidogo, kabla ya kubadilishwa na mazingira. Mtume wa uislam, Muhammad alisema, “Yule anayekuja kwenye nyumba ya Mungu (Kaa’ba) akiwa na niya ya kuhiji na asiwe mwenye kusema au kutenda ovu, basi atarudi akiwa kama mtoto aliyetoka kwa mama yake punde.”[2]. Kutokana na hivyo, kule kuchukia weupe kwa Malcolm-X kulisafishwa baada ya kujifunza Uislamu huu wa kweli. Na tarehe 27 Disemba 1964, Malcolm alisema, “Nadhani hii ndiyo sababu kwanini Uislamu unaenea siku hadi siku. Uislamu hauna ubaguzi wa rangi hata kidogo katika mafundisho yake. Hakuna mafundisho yanayokutaka umhukumu mtu kwa rangi yake. Hata uwe na rangi gani katika Uislamu, utabaki kuwa Muislamu na utabaki kuwa ndugu yetu.”

Malcolm alibahatika kutembelea maeneo tofauti tofauti ulimwenguni na kukutana na watu mbali mbali wenye haiba kubwa. Miongoni mwa nchi alizotembelea ilikuwa ni Saudia Arabia ambapo alikutana na Muhammad Faisal, mjukuu wa mfalme, pia alifika Ghana ambapo alikutana na Kwame Nkurumah, Misri ambapo alikutana na Gamal Abdel Nasser, Algeria na kukutana na Ahmed Ben Bella, kiongozi mkuu wa mapambano ya Algeria dhidi ya wakoloni wa Wafaransa, na alikuwa waziri mkuu wa mwanzo wa Algeria (1962-63) na akawa rais wa kwanza (1963-65).

Pia, Malcolm X alitembelea Nigeria ambapo akafanya muhadhara mkubwa chuo kikuu cha Ibadan. Nchi nyengine ni Ethiopia, Tanzania, Guinea, Sudan, Senegal, Ufaransa, Liberia na Morocco. 21 Sept 1960, Malcolm alikutana na Fidel Castro katika hoteli ya Theresa, Harlem. Tarehe 3 Disemba mwaka wa 1964, Malcolm alikuwa Uingereza akishiriki mdahalo katika chuo kikuu cha Oxford. Yeye akawa upande wa kutetea kichwa cha mdahalo kilichobeba ujumbe “Siasa Kali (isiyo na kadiri) Katika Kuutafuta Uhuru Sio Kosa, na Siasa Poa (mwendo wa kiasi) Katika Kutafuta Haki Siyo nzuri.” Kwa Kiengereza kichwa cha mdahalo ni “Extremism in the Defense of Liberty is No Vice; Moderation in the Pursuit of Justice is No Virtue” Na mdahalo huo ulirushwa na televisheni ya BBC. Katika mdahalo, Malcolm X alijitamba kwa fakhari kabisa, “Uislamu ni dini yangu, namuamini Allah, na namuamini Muhammad.”

Akiwa anafanya muhadhara katika ukumbi wa Manhattan 21 Februari 1965, washika mitutu watatu walimsogelea Malcolm X karibu na jukwaa na kummiminia risasi 15. Malcolm akiwa na miaka 39, baada kupigwa risasi hizo baadae ilitangazwa kuwa ameshaaga dunia mara tu mwili wake ulipowasili katika hospitali ya kidini ya Columbia, New York. Akazikwa katika makaburi ya Ferncliff huko Hartsdale, New York. Katika msiba wake Ossie Davis (1917-2005), mwigizaji na mwongozaji filamu wa kimarekani, mshairi, mwandishi na mpiganaji wa haki za binaadam, alitoa hotuba katika msiba huo wa Malcolm X, aliyeipa kichwa “Mwanamfalme Mweusi Aliyeng’aa”:

Malcolm X nchini ni mtu aliyeacha alama katika harakati za mtu mweusi
ndani na nje ya Marekani, picha ya Malcolm imekuwa ikitumika katika stempu za posta. Na shule nyingi, mitaa, na barabara zimekuwa zikipewa jina lake kwa ajili ya kumkumbuka. Baadhi ya vyuo na shule hizo ni Malcolm X Community College huko Chicago, Malcolm X Liberation University pia Durham, N.C, The Malcolm X Society, Malcom X Shabazz High School iliyopo Newark, New Jersey, Malcolm Shabazz City High School nayo iliyopo Madison, Wisconsin, mtaa wa Reid uliopo Brooklyn, New York ulibadilishwa na kuwa Malcolm X Boulevard; mwaka 2005 chuo kikuu Columbia kilitangaza ufunguzi wa kituo cha elimu walichokiita Malcolm X and Dr. Betty Shabazz Memorial and Educational Center. Afrika ndio kawaida kabisa kuona mabasi yameandikwa Malcolm X au watu wamevaa fulana zenye picha yake.

Hayo yote tisa, kumi; Malcolm X alijitolea kusambaza uilslamu sio tu Marekani bali kwa wote dunia nzima. Kutoka kwake katika kundi lililopotoka la Nation of Islam na kuingia katika Uislamu sahihi kuliacha athari hadi kwa mtoto wa Elijah Muhammad, Wallace Muhammad ambae baada ya kifo cha baba yake alikiongoza chama cha Nation of Islam kufata yale aliyofanya Malcom kwa kufata Uislamu sahihi. Na kwa kweli, kitabu cha historia yake “The Autobiography of Malcolm X”kimewafanya wengi waingie katika Uislamu.

Malcolm X alioana na Betty X (aliyezaliwa kama Betty Sanders) maeneo ya Lansing, Michigan mwaka 1958. Walikuwa na watoto wa kike sita, Atallah Shabazz aliyezaliwa Novemba 1958, Qubilah Shabazz (Disemba 1960), Ilyasah Shabazz (Julai 1962); Gamillah Shabazz (Julai 1964) na mapacha Malaak na Malikah Shabazz waliozaliwa baada ya kifo chake Septemba 1965.

Mwanahistoria Robin D.G Kelley aliandika “Malcolm X kashaitwa majina mengi, mwanaharakati wa weusi, baba wa taifa la weusi, mdini, msiri, mjamaa, na kitisho kwa jamii. Maisha yake siasa na itikadi zake – yanakubaliwa kwa sehemu ndogo…Malcolm amekuwa mfano wa mtihani wenye machaguo huru ambapo kila mtu anaweza kuandika alivyoelewa yeye kuhusu siasa na itikadi zake. Chuck D kutoka kundi la Rap liitwalo Public Enemy na Jaji wa mahakama Clarence Thomas wote wanamwita Malcolm X kama shujaa wao.”

Kifo cha "Martin Luther King Jr" chini ya operation Cointelpro..........

Huyu Martin Luther King Jr alikuwa ni Mchungaji wa Kanisa na mtetezi wa haki za watu weusi kama ilivyokuwa kwa MalcomX ambae na yeye alikuwa mchungaji kwa upande wa uislam. Huyu Martin Luther King Jr alikuwa kiongozi wa "The Southern Christian Churches Leadership", likifanya kazi kubwa ya kuratibu makanisa ya watu weusi na kuandaa harakati za kupinga ubaguzi bila kutumia nguvu au vurugu. Mwaka 1964 alishinda tuzo ya Nobel kutokana na harakati zake za kutetea usawa kwa weusi bila matumizi ya vurumai, lakini pia alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakipinga sana vita ya Vietnam!

Martin Luther King Jr ni mmojawapo wa watu ambao simu zao zilikuwa zimewekewa vifaa vya kurekodi na FBI na ni kati ya watu ambao walikutana na vitisho mbalimbali kutoka kwa FBI, kwa mfano mwaka 1963 aliyekuwa mkurugenzi wa FBI Hoover alinukuliwa akisema kuwa "kutokana na nguvu ya hotuba za King, lazima tumuuangalie kwa ukaribu mno sasa kama hatukuweza kufanya hivo kabla kama mtu mweusi hatari zaidi siku zijazo katika taifa hili, hasa katika muktadha wa ujamaa, watu weusi na usalama wa taifa hili"

Lakini pia Martin Luther King Jr aliwahi kuandikiwa barua ikimtaka ajinyonge, kutokana na kile kilichosemwa kuwa ni ouvu uliokuwa umefichukiwa dhidi yake, hii ni sehemu ya barua hiyo: "Kutokana na maisha yako kugubikwa na uchafu mwingi, sitaweza kukuita Mr, Mchungaji au Dr bali nitakuita King. King, angalia moyo wako, unajua wewe ni muongo na mzigo mkubwa sana kwetu sisi watu weusi, wewe ni muongo na shetani, wewe si mtu wa wa Mungu na unalijua hilo. King kama walivo waongo wengine mwisho wako umekaribia, shahada zako za heshima, tuzo yako ya Nobel na heshima zote ulizotunukiwa hazitakusaidia, king, narudia umekwisha.

Hakuna mtu anayeweza kushindana na ukweli, uchafu wako wote yakiwemo matendo ya ngono na kurekodiwa na utayakuta ndani ya tape. Narudia tena hakuna mtu anaweza kushindana na ukweli, umekwisha King, kwenye tape utakuta uchafu wako ukiofanya na wenza wako wa kike na wa kiume, King, una jambo moja tu ulilobaki nalo! Unajua ni lipi! Una masaa 34 kulitekeleza jambo hilo.Kuna njia moja tu ya kukutoa katika haya, ni afadhali ukaichukua sasa kabla uchafu wako haujaeekwa hadharani"

Martin Luther King Jr alifariki April 4, 1968 akiwa na miaka 39 kwa kupigwa risasi akiwa hotelini mjini Memphis Tennessee alipokuwa amekwenda kushiriki kuhamasisha harakati za kudai mazingira bora ya kikazi kwa watu weusi, aliyemuua alifahamika kama James Earl Ray na alikamatwa nchini Uingereza na kurejeshwa Marekani, baada ya kifo cha King iliundwa kamati kuchunguza kifo hicho lakini taarifa zake hadi sasa ni siri na zinatarajiwa kuwekwa wazi mwaka 2027 kufatia sheria za usalama za Marekani zinazoongoza taratibu za taarifa za siri.

Wataalamu walioufanyia uchunguzi mwili wa King wanasema moyo wake ulikuwa kama wa mtu wa miaka 60 japo alikuwa na miaka 39 na kwamba hii ilitokana na msongo wa mawazo uliotokana na harakati zake za kudai usawa kwa watu weusi.

Huyu Martin Luther King Jr ni moja ya wanaharakati wakubwa sana nchini Marekani hasa katika kupigania haki za waamerika weusi katia karne ya 20, mwanaharakati huyu alizaliwa Januari 15,1929 huko Atlanta ,Georgia nchini Marekani .Wazazi wake walimlea katika maadili ya dini ya kikristo na inasemekana walikuwa viongozi wa Dhehebu la Baptist. Nje ya kuwa mwanaharakati wa masuala ya Haki na Usawa kwa wamarekani weusi Luther alikuwa ni Mhubiri wa Dhehebu la Baptist.

Martin Luther King Jr alijibebea umaarufu mkubwa sana kwenye Hotuba nzito sana inayojulikana kama "I HAVE A DREAM" aliyoitoa Agosti 28,1963 mjini New york katika mnara wa Kumbukumbu wa Rais Abraham Lincoln. Katika hotuba hiyo alielezea matumaini Makubwa kwa watu weusi akisema ipo siku wamarekani weusi wataupata Uhuru na Usawa katika Ardhi ya Amerika. Katika hotuba hiyo watu takribani 200000 walihudhuria kumsikiliza mwanaharakati huyu wa kupinga ubaguzi katika Amerika na Duniani kote. Aliuchukia ubaguzi wa rangi,Kidini,Kipato n.k .

Wakati wa karne ya 20 huko Marekani kuliibuka ubaguzi mkubwa wa Kirangi kwenye Taasisi za Kielimu ,kiafya na kidini ,vyombo vya usafiri ,Kwenye kumbi za Starehe ,Kwenye Ofisi za Umma ,Kwenye mashamba,Kwenye Viwanda ,Kwenye maduka,Kwenye masoko,n.k waamerika weusi walinyanyapaliwa sana. Ilikuwa ukimuona mzungu na umekaa kwenye seat unampisha ikiwa gari limejaa, ukigoma unaadhibiwa vibaya sana,mwaafrika ulikuwa huruhusiwi kula hoteli moja na mzungu, Mwafrika hakuruhusiwa kusoma Shule na Mzungu au mtoto wa kizungu ,Ilikuwa hairuhusiwi mzungu na mwafrika kuoana na lilikuwa ni kosa kubwa sana kufanya hivyo n.k. Hivyo kulikuwa na hotel,hospitali ,maeneo ya burudani ,makanisa n.k ya wazungu na waafrika .

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya akina Marcus Garvey ,William Dubois ,Malcolm X walisimama kidete kutoa hotuba za kulaani vikali vitendo vibaya vya kibaguzi vilivyokuwa vinafanywa na wazungu kwa kutumia majarida,vitabu ,kuandika mapendekezo ya sheria zinazolinda watu weusi dhidi ya wazungu ktk Bunge la Marekani ,walitumia Redio na Televisheni kupinga ubaguzi wa Rangi,walitumia mbinu ya maandamano kuamusha hisia za Tabaka baguliwa (Waamerika weusi) n.k .Watu hawa walifanya kazi kubwa sana ya kupinga ubaguzi uliofanywa na wazungu.

William Dubous na wanaharakati wengine walianzisha mpango uliojulikana kama "BACK MOVEMENT " Ukimaanisha kuwa sasa waafrika warudi kwao wakaijenge Afrika yao ,wengi walirudi na wengine wengi pia walibaki wakiamini kuwa ipo siku wangepata Uhuru na Usawa ktk Ardhi ya Amerika.William Dubous alionyesha mfano kwa kuhama Marekani na kuja kuishi Afrika ktk nchi ya Ghana mjini Accra. Martin Luther King Jr ni moja ya watu walioamini kuwa ukombozi utapatikana huko huko Marekani na hakuamini katika kuikimbia Marekani .Funzo tunalopata haki haipiganiwi ukiwa ng'ambo bali ukiwa katika nchi yako.

Martin Luther King Jr aliendelea kuwapigania waafrika huko huko Marekani na kujitwalia Tuzo kadhaa za Amani (Nobel Prizes) baada ya kuutambua mchango wake katika kuwapigania waamerika weusi huko Marekani, harakati za kupigania Uhuru na Usawa kwa wamarekani weusi zilikuwa ngumu sana kwani kulikuwa na kikundi cha Siri kilichojulikana kama Ku Klux Klan au Kuklux Clan kilichoundwa na wazungu ili kufifisha harakati za wamarekani weusi kudai Uhuru na usawa huko Marekani. Kikundi hiki kilikuwa hatari sana kwani kilikuwa kinawalenga viongozi wa harakati ili kiwaue.

Martin Luther king Jr aliuwa kwa kupigwa risasi mwezi wa Aprili 3,1968 kijana aliyetekeleza unyama huu alikuwa ni wa kizungu alijulikana kwa jina la James Earl Ray huko mjini Memphis, jimbo la Tennessee. Martin Luther king Jr atakumbukwa kwa mbinu zake za kudai haki ,Uhuru na Usawa miongoni mwa wazungu na watu wa jamii ya kiafrika, alidai haki ,Uhuru na usawa bila kuofia kulipa damu yake katika harakati za ukombozi. Martin Luther king Jr alituma ujumbe mzito Barani Afrika, Amerika ya kusini na Asia kuwa Uhuru, Haki na Usawa unapaswa kuheshimiwa kwa Binadamu wote bila kujali wewe ni wa Rangi gani ,kipato gani,Dini gani ,n.k

Martin Luther king Jr atakumbukwa sana hasa ktk hotuba yake maarufu ya "I HAVE A DREAM" Akimaanisha "Nina ndoto" ambayo ilitoa unabii mkubwa sana wa Uhuru, haki na Usawa na hatimaye Dunia ilishuhudia Marekani ikiongozwa na mwamerika mweusi mh.Barack Obama wakati miaka ya nyuma ilikuwa ni marufuku kwa wamarekani weusi kushiriki katika medani za kisiasa na hata kupiga kura hawakuruhusiwa Harakati za Martine Luther King Jr umeleta mafanikio makubwa ndani ya Marekani ya Leo. Kuna tofauti sana na Marekani ya Jana hasa katika kuutazama usawa kati ya Marekani mweusi na mmarekani mweupe.

Operation hii inabaki kuwa moja ya OPERATATION muhimu katika shirika la upelelezi la FBI nchini Marekani, kufatia kutamatisha viongozi ambao kipindi hicho serikali ya Marekani iliwaona hatari kwa masrahi yake, lakini Operation hii ni moja ya OPERATATION iliyo acha maumivu makubwa kwa wapenda haki, uhuru na ukombozi wa mtu mweusi.

Katika moja ya Operation ambazo zilifanikiwa kwa kiwango kikubwa ndani ya Marekani ni hii ya Operation Cointelpro ambayo ilifanya kazi kwa mafanikio makubwa katika historia ya nchi hiyo, toka operation hiyo kumalizika nchini humo aijawahi kuinjiniwa operasheni nyingine iliyohusisha kudhibiti watu hatari kimkakati katika nchi ya Marekani.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu

Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2019, All Rights Reserved.
FB_IMG_1561745988484.jpeg
FB_IMG_1561753490751.jpeg
FB_IMG_1561745801045.jpeg
 
Copyright 2019, All Rights Reserved.View attachment 1141674View attachment 1141675View attachment 1141676
Hivi huyo Mkurugenzi wa FBI alikuwa John Edgar au John Antony?
 
Mada nzuri ila kuna lengo la Udini uliopindukia humu, Mchungaji Lutheran hujamuelezea kuhusu kazi zake za kidini kama Malcom, Waislamu mna kazi sana
There is beauty beyond religions tuache kufuatilia viashiria vya dini kuonyesha usawa maisha yatakua ni mazur sana
 
Sijaielewa vizuri hii mada. Hivi ilitakiwa iwaelezee Malcolm X na Martin Luther King Jr au ielezee Operation Cointelpro ilivyoendeshwa hadi kuwaua akina Malcolm X na Martin Luther King Jr?
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Mada nzuri ila kuna lengo la Udini uliopindukia humu, Mchungaji Lutheran hujamuelezea kuhusu kazi zake za kidini kama Malcom, Waislamu mna kazi sana
Nilijua mimi pekee nimeliona hili, Shaabaz kasimuliwa, kapambwa mpaka na nukuu za Qur'an kapewa.
Lakini mtu ambaye hata jela hakuwahi kukanyaga kasimuliwa kihuni huni tu..
Tuna safari ndefu.
 
There is beauty beyond religions tuache kufuatilia viashiria vya dini kuonyesha usawa maisha yatakua ni mazur sana
Nadhani pia tuache kuweka viashiria vya dini tunaposimulia simulizi kama hizi.
 
Back
Top Bottom