Opera Software ASA wamefanyia upgrade Opera Mini 7.0 na kuitoa upya ikiwa 7.1.
Kikubwa walichoboresha ni download manager. Wamefanya yafuatayo:
Speed ya kudownload imeongezwa kwa kufanya marekebisho katika servers zao, hasa kwa mafaili yasiyozidi Mb 15
Download dialogue sasa inakuruhusu kusimamisha download process(pause downloads) na unaweza kufunga opera mini(exit) kisha ukarudi baadaye ukaendelea na kudownload hilo faili!
Wakati wa ku download file unaweza kulipa jina jipya kabla hujali save!
Pia download manager inakumbuka kila aina ya fail umeli save katika folder gani! Kwa mfano ukidownload mp3 file ukasave katika "my music" hutaulizwa tena utakapokuwa unadownload mp3 wakati mwingine kuwa unasave wapi litaelekezwa moja kwa moja katika my music! n.k.
Huenda usione ufanisi mkubwa katika matumizi ya opera mini 7.1 download manager ama kutokana na simu yako au sababu myingiezo wanakaribisha maoni ili wayafanyie kazi.
Kwa maeleza zaidi, maoni ya wale ambao tayari wameonja na download link tembelea hapa.
(ANGALIZO: Mimi nimekuwa na tatizo la kudownload opera mini kwa wiki za karibuni. Hata hii 7.1 nimeshindwa kuidownload. Huenda na wewe ukakumbana na tatizo hilo itabidi kuwa na subira. Wale wasio na tatizo hilo nawatakia mafanikio. Nyama ikikushinda kwa kutokuwa na meno unawaachia wenye meno watafune hadi ya kwako yatakapoota!)
na kama unapata shida ya kudownload ina maana simu yako inaprefer jar over jad na always kawaida opera kuna jad files kwa file la jar lisilosumbua kudownload utalipata hapa