zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 24,225
- 39,773
Kwa miaka mingi Marekani imewekeza trilioni za dola kwenye satelaiti, ndege za upelelezi, drones, rada na mashirika ya kijasusi ili kupata taarifa za adui. Lakini inaonekana Iran imegundua njia rahisi zaidi na ya gharama nafuu: bando la jero na kufungua tu TikTok, X, Instagram au Facebook.
Ripoti zinaonyesha kuwa CENTCOM imeanza kuwaonya wanajeshi wake kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii baada ya kubainika kuwa video na picha wanazopakia zinawasaidia wapinzani kuona kwa haraka makombora yamepiga wapi, yameleta uharibifu kiasi gani, na kama kuna haja ya kufanya secondary attack ili kuongeza madhara. Kwa kifupi, baadhi ya wanajeshi walikuwa wanatoa "battle damage assessment" bure kabisa bila kujua.
View: https://youtube.com/shorts/A_iCvFNeiLE?si=plvI0gqT6s5hdUtm
Ni jambo la kuchekesha ukilitazama kwa mbali. Marekani inatumia mabilioni kupeleka satelaiti angani, halafu mtu mmoja akiwa kambini anaamua kupost video ya "Bro, tulipigwa lakini niko salama," na ndani ya dakika chache adui anapata taarifa ambayo ingegharimu mamilioni kuikusanya kwa njia za kawaida.
Hii ndiyo nguvu ya open-source intelligence (OSINT) katika vita vya kisasa. Wakati mwingine taarifa muhimu hazitoki kwa jasusi aliyejificha gizani, bali zinatoka kwa mtu aliyeshika simu na kutafuta likes.
View: https://youtube.com/shorts/2DXnHa5c0mw?si=abXhBvsik4dwSPjJ
Vita vya leo havipiganwi kwa makombora pekee. Vinapiganwa pia kwenye screen za simu. Na wakati mwingine, adui hahitaji kuvunja mfumo wa siri; anasubiri tu mtu "ajimwambafy" maisha yake mtandaoni.
Inaonekana CENTCOM imeamua kwamba silaha rahisi ya kuizuia Iran kupata taarifa si kombora jipya, bali ni kuwaambia wanajeshi wake: "Wekeni simu chini kwanza."
Source: US commander warns troops their videos help Iran, sources say