Oooooo baby nitakufa mikononi mwako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Oooooo baby nitakufa mikononi mwako

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jacaranda, Apr 10, 2012.

 1. J

  Jacaranda Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lilikuwa ni dirisha lililosukumwa na upepo na kujifunga huku likitoa sauti yenye mshindo mkubwa lililomuamsha toka usingizini.Baada ya kuamka macho yake yalikutana ana kwa ana na giza zito lililoutawala usiku huo ambao pia ulikuwa umeandamana na ukimya uliokuwa ukikatizwa na sauti ya upepo mara kwa mara na kuufanya usiku huo kuwa kama umetawaliwa na utawala wa shetani.

  paaaa sauti ya dirisha liliojifunga tena kwa mara ya pili ilimshtua tena na kumfanya anyanyuke kama mtu mwenyehasira ya kunyang'anywa mke kuelekea kwenye dirisha na kulifunga kwa nguvu.Macho yake kwa sasa yalikuwa yamelizoea giza na hivyo kumfanya aweze kuona baadhi ya vitu mle chumbani japo kwa shida.Akarudi kitandani na kukaa huku akimtazama mke wake aliyekuwa amelala fofo bila yya kushtushwa na kelele yoyote.Shuka alililokuwa amejifunika lilikuwa limeshuka mpaka juu kidogo ya kiuno na hivyo kuifanya night dress yake ya pinki kuonekana vizuri kwa upande wa juu. Pumzi aliyokuwa akiivuta na kuitoa ilienda sambamba na kunyanyuka na kushuka kwa kifua chake ambacho kilikuwa kimetunukiwa matiti yaliyojaa vizuri na kumfanya aonekane kama hajawi kunyonyesha.


  Alikuwa ni mwanamke mwenye umbo zuri na tabia nzuri,mwanamke ambaye mwanaume yoyote angejihisi mwenye bahati kubwa zaidi ya ile ya kuzaliwa kwenye ukoo wa kifalme kumumiliki na kumfanya kuwa mke wake.Lakini Jason hakujihisi kuwa mwenye bahati na kila mara alipokuwa akiambiwa na marafiki zake kuwa amebahatika kupata mwanamke mzuri alijibu asante huku akitabasamu,hakuna aliyejua kuwa ni midomo tu ndio ilikuwa ikitabasamu ila moyo wake ulikuwa umenuna na kukakamaa kila mara walipokuwa wakizungumza kuhusu yeye na mke wake Joan.

  Nywele za Joan usiku huo aliziacha bila kuzifunga na hivyo kuzifanya zianguke mpaka usoni na baadhi yake kufika mpaka katikati ya midomo yake. Jason akanyoosha mkono na kuziondoa toka usoni na kuzirudisha nyuma kichwani.Joan hakushtuka toka usingizini bali aliendelea kukoroma kwa sauti hafifu sana huku uso wake mzuri ukionekana kama wa malaika ambaye hajachafuliwa na uovu wowote wa dunia hii.Midomo yake kwa sasa ilionekana vizuri na kuifanya dhamira ya Jason ifunguke na kumsuta kama mwanamke aliyekamatwa kwa umbeya na shoga zake .
  Kwa miaka saba sasa amekuwa akiibusu midomo ya Joan wakati akili yake na moyo wake vyote viko kwa mwanamke mwingine.Hii ikamfanya azidi kujisikia aibu kwani kwa miaka saba midomo na ulimi wa Joan umetalii karibu kwenye kila kiungo cha mwili wake na mara nyingi kumfanya agumie kwa sauti zilizojaa raha. Jambo ambalo liko wazi nafsini mwake ni kuwa siku zote akili yake imekuwa ikifanya mapenzi na mtu mwingine.Jason akajihisi kuwa mtu mwenye hatia kubwa.Japokuwa katika maisha yake yote ya ndoa hajawahi kufanya mapenzi ya kimwili nje ya ndoa lakini nafsi yake ilimsuta wazi wazi na kumpigia kelele kuwa ni msaliti na ni kweli alikuwa ni msaliti.Ndani ya moyo wake na akilini mwake amefanya uzinzi zaidi ya mara moja ni zaidi ya mara elfu. Kila walichokuwa wakikifanya kitandani na Joan yeye akili yake ilikuwa mbali kwa mwanamke mwingine,mikono yake ilihisi inampapasa huyo mwanamke na hata vilio vya mahaba vya Joan alihisi ni vya mwanamke huyo.Jason alitambua ni bora mtu aziniye nje ya ndo huku akili yake na moyo wake vikifanya mapenzi na mke wake kuliko yeye ambaye akili na moyo viko kwa mwanamke mwingine na kilichobaki kwa mkewe ni mwili tu

  Jason akaiangalia midomo ya Joan ambayo ilikuwa imefunguka kidogo na kuifanya ionekane mizuri zaidi. Akatamani midomo ile isingefunguka siku ya harusi yao na kusema ‘mwenzangu poke pete hii iwe ishara ya upendo kwako" na kisha "ndiyo nakubali kuishi naye kwenye shida na raha".Shuka aliyokuwa amejifunika Joan kwa sasa ilikuwa imeshuka zaidi mpaka kwenye magoti na hivyo kuifanya nguo ya ndani ionekane kupitia kwenye nguo ya kulalia iliyokuwa imepanda juu kidogo na kuyaachia mapaja yake meupe na makubwa wastani kuonekana.Jason akaivuta shuka na kumfunika vizuri mpaka kwenye shingo na mara mvua kubwa ikaanza kunyesha.

  Jason akanyanyuka toka kitandani na kuelekea sebuleni akawasha taa kisha Akakaa kwenye kochi huku akisikiliza sauti ya mvua iliokuwa ikilipiga bati la nyumba yake na kulifanya litoe sauti ya maombolezo kama mwanamke aliyefiwa na watoto wake wote kwa wakati moja.Hakuna kitu duniani anachokichukia Jason zaidi ya mvua,kila mvua inyeshapo kumbukumbu za mpenzi wake wa kwanza uchimbuliwa toka kwenye ubongo na kurushwa kwenye fikra zake na kuonekana kama mkanda wa sinema na katika sinema ile yeye ndiye muhusika mkuu .Pale mvua inyeshapo mchana basi Jason usitisha kazi zake zote na kutokomea katika ulimwengu wa fikra,Ulimwengu ambao hakuna kiumbe chochote kinaweza kuufikia zaidi ya yeye mwenyewe.Katika ulimwengu huo umuona mpenzi wake wa zamani Alisy akimuita Jason mpenzi njoo njoo nilikuadi tutakufa pamoja nilikuwa sitani mpenzi njoo unikumbatie nilisikie joto lako na mara baada ya mvua kukatika Jason urudi tena kwenye dunia halisi ambayo yeye ni mume wa Joan na siyo Alisy hicho umfanya kuwa na uzuni kubwa moyoni na ndiyo sababu anaichukia mvua.

  Na kwa sasa fikra hizi zilikuwa tayari zimeanza kumuijia kwa kasi kama moto uliowashwa nyikani lakini kama mtu aliyedondoshiwa wazo kwenye ubongo wake akaisikia nafsi yake inamwambia "Jason kwa nini unaumia hivi,usiwe mjinga kiasi hicho,nyanyuka umuandikie barua Alisy, ni vizuri akajua unavyojisikia inaweza kukupunguzia machungu" Jason akapumua kwa nguvu huku fikra zake zikikubaliana na sauti ya nafsi yake akanyanyuka kuelekea kwenye shelfu la vitabu lakini kabla ajalifikia nafsi yake nyingine ikamwambia "Unakuwa mpumbavu, Alisy ni mwanamke katili hata ukimuandikia barua mia atajibu hata moja angalia toka mlipoachana hajawahi hata siku moja kukutafuta,unajidharirisha kumnyenyekea akipokea barua yake atacheka na baadae ataenda kuitawazia kamwe Jason usiandike chochote" hii ikamfanya Jason anyong'onye na kuanza kugeuka kurudi kwenye kochi lakini ghafla nafsi yake ikamwambia "ooo Jason utaendelea kuumia mpaka lini,usipoandika moyo wako utasononeka mpaka unapoingia kaburini" Akageuka na kulikimbilia shelf kama mtoto aliyeonyeshwa icecream, akanyofoa karatasi ambazo uzitumia kuandika barua akachukua kalamu kwa kasi ileile akaelekea kwenye meza Akakaa huku akitafakari nini cha kuandikia,akaisi kama ubongo wake umeporwa maneno na mikono yake imepooza akakaa kama hivyo kwa dakika ishirini na ghafla kama mtu aliyeshukiwa na roho mtakatifu akaanza kundika kwa kasi ya ajabu.Hakujua kama barua hiyo itabidirisha kabisa maisha yakeI yote na kuvivunja vyote alivyojenga maishani mwake.

  Dia Alicy

  Leo tena mvua imenyesha , siku ya kwanza nilipokutana na wewe nafikiri unakumbuka vizuri, siku hiyo mvua ilinyesha kubwa sana. Basi toka siku hiyo nimejifunza kuyasikiliza matone ya mvua yanapogonga kwenye bati huwa yanazungumza nini? Najua kuna ujumbe huwa umefichika ndani yake tunachoitaji ni kusikiliza kwa makini na tutagundua nini yanachozungumza. Leo nimesikiliza kwa makini tone moja baada ya jingine kila linapogonga kwenye bati la nyumba yangu huwezi kuamini nilichokisikia
  to be continued
   
 2. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka umetisha...very interesting story....Keep it up, I promise to read it to the end...
   
Loading...