hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,545
Tumechoshwa na vitendo vya kuzomewa kwa mgombea wetu. Kuanzia kule Mbeya na hata hapa Dar es Salaam,Dr. Magufuli amekuwa akizomewa na kuoneshwa wazi kuwa hatakiwi. Yeye hujikaza kisabuni tu. Hutetemeka lakini huimarika.
Amewakosea nini hadi mumzomee? Wana-Dar es Salaam hamna tabia hiyo. Mmekuwa watiifu kwa CCM kwa muda wote. Mmekuwa hata wavumilivu kuitwa wala-miguu ya kuku. Kiwewapata nini? Nani kawaondoa utii kwa CCM?
Mkimzomea tena Dr. Magufuli,nasi tutamzomea wenu hata kwa kuigiza kwenye giza. Mnapaswa kumshangilia Dr. Magufuli na kumpa kura zenu. Msimzomee na kumnyima kura tafadhari!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
CCM siasa zetu za kistaarabu. UKAWA wanaendeshwa kwa viroba! Katika hali kama hiyo ni lazima watafanya hizo tabia za kuzomea.
Aidha, UKAWA waelewe kuwa, CCM ina wanachama na wapenzi wengi pia, hivi na sisi tukiamua kuanza hiyo tabia ya zomea zomea, mgombea wao Lowassa atapona kweli?
Rai yangu ni kwamba vijana waache kukubali kutumiwa na wanasiasa kwa kupewa viroba ili kukidhi matakwa yao ya kudhalilisha wagombea. Hii tabia sio nzuri na haikubaliki.
napenda sana kuwashukuru wazazi wangu
kipindi kile wananikazania kuhusu elimu sikuwa ninaaelewa umuhimu wake
leo ndio ninaelewa kuwa shule ni kila kitu
wanaozomea ni mafala na malofa ... huwezi kuwa ukawa na akili nzuri na mwenye elimu yako ukakaa barabarani ukazomea unless hujaelimika ila tu umekaa tu muda mrefu darasani.....

HakikaNi bora kuzomewa kuliko matusi yanayotolewa huko majukwaani.