Ontario ameshindwa Twitter, kuna wajanja wengi sana kule

Status
Not open for further replies.
Huwa napata ukakasi sana mbongo anapokazana kulazimisha kutaka wengine wapihe pesa.kwani ukipiga pesa zako kimya kimya tatizo liko wapi.
Ni mfatliaji wa story zake nyingi zina mikanganyiko. Anahangaika sana na watu wa mtandaoni. Kwanini asijipigie hela zake kimya kimya?

Ila hata kama anawaibia wengine bado kwangu jamaa ni kichwa.
 
Watu wamepost mpaka matokeo yake ya Chuoo Jamaa ni mjingaa tuu
Ni lini matokeo ya chuo yakawa siri? Hata wewe mtu akijua jina lako na umesoma wapi dakika sifuri anaweka matokeo yako hadharani. Kufaulu darasani haijawahi kuwa kigezo cha kupata maendeleo.
Jamaa ana akili..kama kweli anawatapeli watu hadi sasa hivi basi ni genius wa ukweli kwenye sekta hiyo.
Na bado watu watatapeliwa siku zote
 
Huwa napata ukakasi sana mbongo anapokazana kulazimisha kutaka wengine wapihe pesa.kwani ukipiga pesa zako kimya kimya tatizo liko wapi.
Ni mfatliaji wa story zake nyingi zina mikanganyiko. Anahangaika sana na watu wa mtandaoni. Kwanini asijipigie hela zake kimya kimya?

Ila hata kama anawaibia wengine bado kwangu jamaa ni kichwa.
Biashara matangazo ndugu
 
Hizi IB links, commission, training fees, na spread pips charge ndizo anazitafuta kwa Sasa sababu ndio ziliwafanya wapate faida ya nusu billion pale TMT kutoka kwa watu walio watrain kupitia hizo components nilizotaja hapo juu.

Nimefanya Forex muda mrefu nazijua tricks almost zote za hii biashara.

Na Kama angekuwa anapiga hela kweli angeendelea kutrade mwenyewe kimyakimya ili apate faida mwenyewe. Kwanini anawatafuta zaidi watu kwa nguvu zote kwenye social networks zote?

Hujiulizi kwanini hawafundishi watu kumix na kutengeneza chakula Cha kuku? Wakati yeye ni mtaalamu wa ishu hizo? Anachokitafuta kwenye Forex Ni watu hili awakamue kwenye hayo madude hapo juu!

Imagine second batch gharama ya training kila kichwa ilikuwa 120,000/= na kwenye trainings kwa zile sessions alipata watu 1000 Sasa zidisha kwa 120,000×1000= 120,000,000= hii Ni net profit bila Kodi Wala VAT. Achana na IB links, spread charges, e.t.c

Unfortunately hela zote alizopata alikutana na wasauzi(wazulu) alokuwa anafanya nao kazi... nao wakapita na mkwanja wote akabaki na mavi tu tumboni. Nikamkuta KB Bar ya Tegeta anakula mishkaki ya jero jero.

Ana haki ya kurudi tena kwa nguvu atafute makoro yake buku atangeneze milion 300,000,000= kwa mwezi mmoja. Just that! Na ingewezekana kwa nguvu ya kipawa cha ushawishi wa kitapeli aliyonayo tatizo hajui kuishi na watu vizuri ana kiburi, dharau, jeuri na maringo ambayo yatamchelewesha Sana kumfikisha kwenye climax Yake ya mafanikio maana Sasa Yuko busy kuharibu reputation yake badala ya kuijenga.
 
Kwa wote mnaosema Forex ni scam

Msichanganye forex na Jeff,,
Forex is real ila jeff anaweza asiwe real (forex sio wizi ila forex traders ndio wanaweza kua wezi)

Mimi nimejifunza na nili focus nayo kipindi kile cha templer na mpesa, na nina idea nayo na ninajua jinsi inavyofanya kazi. Sikuipa kipao mbele kama hao kina Magnetico au 255Millionairs kwa sababu sina uwezo wa kufundisha na kukuza mitaji kupitia ada za wanaojifunza.

Napiga mbanga zangu zikisimama nitarudi kwenye trading. Ni sawa Jeff anaweza kua mwizi au tapeli ila nyie mnaosema forex ni utapeli hapana na wakatalia, angalieni isije kua kushindwa kwenu kuielewa ndo mkaitumia kuisema vibaya.

Sio forex tu, ujuzi wowote asilimia kubwa huwezi kupewa bure ndio maana mashuleni watu wanalipa ada "If you are good in something don't do it for free" hii ni moja ya mbinu itumikayo na watu wengi tu kujipatia kipato cha ziada the same thing kwa hao wanaofundisha forex.

MANENO YA BIBLIA HAYA

Ecclesiastes 11:1

Invest your money in foreign trade, and one of these days you will make a profit.
 
Ni lini matokeo ya chuo yakawa siri? Hata wewe mtu akijua jina lako na umesoma wapi dakika sifuri anaweka matokeo yako hadharani. Kufaulu darasani haijawahi kuwa kigezo cha kupata maendeleo.
Jamaa ana akili..kama kweli anawatapeli watu hadi sasa hivi basi ni genius wa ukweli kwenye sekta hiyo.
Na bado watu watatapeliwa siku zote
Atakuwaje Genius wakati anao watapeli ni WAJINGA wenzake ?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom