Ongezeko Posho Elimu ya Juu Changa La Macho, Haitoshi!

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Naipongeza serikali kwa kupandisha posho angalao kufikia 7,500. Lakini ukweli wakati walipoanza kulipa shs 5000 ilikuwa inatosha maana chakula, nauli, vyumba na gharama nyingine za maisha zilikuwa chini. Tujiulize, wakati wamepandisha hadi elfu 5, sahani ya chakula ilikuwa shs ngapi? leo shilingi ngapi? Kuna mabadiliko ya asilimia ngapi? Utakuta gharama zimepanda kwa zaidi ya 100% lakini utaikuta serikali inajivuna kuwa ni sikivu wakati hakuna kilichopanda in the real sense.

Kwa maoni yangu, Serikali ya Mkapa pamoja na kwamba ilikuwa haipandishi sana mishahara na posho za wanafunzi, ilikuwa nzuri maana mfumuko wa bei ulikuwa chini sana na thamani ya shs ilikuwa stable. JK anapandisha sana mishahara na posho ila inflation na depreciation of currence ipo juu hivyo wananchi wanaumia zaidi. Njia pekee ni serikali sasa kupunguza kukopa hasa ndani na kudhibiti thamani ya shilingi na mfumuko wa bei. Je, wana waziri wa fedha, gavana na watendaji wengine wenye uwezo?
 
Back
Top Bottom