Ngalikivembu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,959
- 876
HIVI karibuni vyombo vya habari nchini, vilipambwa na taarifa ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Haule, maarufu kama Profesa Jay kujiunga na siasa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Taarifa hiyo iliambatana na picha ya msanii huyo akiwa na msanii mwenzake anayefanya muziki wa hip hop, wakiwa pamoja na mweyeji wao Joseph Mbilinyi Sugu ambaye pia ni mbunge wa Mbeya Mjini kupitia CHADEMA.
Nimemwita Sugu kuwa mwenyeji wao, kutokana na ukweli kuwa ni mkongwe wa muziki huo aliyetangulia kutua CHADEMA na kisha hiyo juzi kuwakabidhi kadi ya chama Proffesa Jay pamoja na msanii mwingine Levison Kuselwa K wa Mapacha.
Pia wasanii wote hao kwa pamoja walionekana wakiwa na mbunge wa jimbo la Ubungo, John Mnyika, ambaye alishirikiana nao katika hafla hiyo ya kukabidhi kadi hizo kwa wanachama hao wapya.
Kutokana na hatua hiyo mimi kwa mtazamo wangu naona kuwa wasanii hao wamefungua njia kwa wasanii wengine kuiga mfano huo ili kupata fursa ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama na serikali.
Kwa mtazamo wangu, wasanii nchini ni kama waliofungiwa sehemu ambayo haiwawezeshi kushiriki masuala yoyote katika jamii tofauti na maonesho au matamasha yao, hali ambayo inadhihirishwa na kutojiamini kwao na kufanya mambo yasiyotarajiwa kwenye jamii.
Kwani licha ya kukubalika kwa wasanii mbalimbali kutokana na muziki wao, mchango wao katika jamii umekuwa ukithaminiwa kwa muda tu na kupotea.
Ikumbukwe kwamba mara kwa mara wasanii wamekuwa wakitumika katika kampeni za kisiasa kwa kusherehesha watu wengine katika mikutano ambayo wanasiasa huwania nafasi mbalimbali za uongozi ambao hata hivyo wakishachaguliwa hawana wanalowasaidia katika kutetea maslahi yao.
Miongoni mwa kilio kikubwa ambacho hutolewa na wasanii wengi nchini ni hali ya kutothaminiwa kwa kazi zao kwa kutumiwa hovyo pasipo faida yoyote hali inayochangia umaskini mkubwa miongoni mwao, licha ya kazi kubwa wanayofanya ya kuelimisha jamii.
Hii inadhihirisha wazi kuwa wawakilishi wao ambao wanawachagua hawaaminiki kwa kuwa hawawezi kufanya kama wanavyotaka kwa maombi yao kutotekelezwa na viongozi waliowachagua kwa wakati.
Kutokana na hali hiyo, naamini kuwa yapo mambo mengi ambayo ni kero kwa maendeleo ya wasanii nchini ambayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi zaidi ikiwa wasanii wenyewe wataungana na kutengeneza mpango wenye tija katika maisha yao kwa kuwa na wawakilishi wao serikalini wanaotokana na wao.
Mimi naamini kuwa kila msanii anapaswa kushiriki fursa zote kama raia wengine bila kumhofia mtu yeyote kwa kuwa kazi yake ya muziki hudhihirisha kuwa anahitaji mabadiliko ambayo naamini yanaweza kutekelezwa na yeye akiwa kiongozi.
Hii isiwe tu kwa wasanii wa bongo fleva tu, bali hata kwa wasanii wa tasnia nyingine, kwani jamii inapaswa kuamka na kutambua wajibu wake kwa kutekeleza majukumu ili kufanya mambo ambayo yamesahaulika katika kujiletea maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.
Kama vile haitoshi wasanii mbio zao zisiishie kujiunga na vyama vya siasa pekee, bali wanapaswa kushiriki katika michakato mbalimbali ya uchaguzi ili kuongeza chachu ya mabadiliko nchini kwa kuwa kila mmoja anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
Source:Tanzania Daima