Uko sawa kabisa kiongozi, ndiyo maana hapo juu nikasema wanaopata mimba sana ni watoto wa sekondari na wanandoa. Vitoto viko kwenye balehe na kuvunja ungo huko shule havujui kitu wala kufikiria madhara unategemea nini? Upande wa pili wanandoa inafika kipindi wanapitiwa hata njia za uzazi wa mpango zinakuwa ngumu, hasa ukifikiria kwamba idadi kubwa ya Watanzania wanatoka kijijini na elimu hawana. Kutoa watatoa sana mkuu mara nyingine bila hata waume zao kujua.