Ongezeko la riba kwenye mfuko wa hifadhi NSSF

Godi haule

Member
Joined
Nov 15, 2022
Posts
6
Reaction score
11
Kwanini NSSF Wasiweke Mfumo wa Riba Kwenye Michango ya Wanachama Wao?

NSSF chini ya sheria yake inamuagiza mwajiri kuwasilisha 20% ya ujira wa kila mfanyakazi wake kila mwezi, ambapo sheria inaeleza mfanyakazi hatakiwi kuchangia zaidi ya 50% ya kiwango hicho.

Fedha hizi huwekezwa kwenye miradi mbalimbali ambayo lengo ni kutengeneza faida.

Kama lengo la uwekezaji ni kutengeneza faida, kwanini mchangiaji hapati chochote kama gawio/riba kwenye michango yake kutoka kwenye hiyo faida?

Nchini India kuna India’s Employees’ Provident Fund (EPF), EPF ni sawa na NSSF kwa hapa Tanzania.

EPF huwekeza fedha za michango ya wanachama wake katika sehemu mbalimbali kama vile hati fungani za serikali & hisa.EPF haiishii hapo; wao hutoa riba kwa wachangiaji wake kwa kiwango cha 8% hadi 9% kwa mwaka, lengo ni kumuandalia mazingira mazuri mchangiaji anapostaafu/kuchukua mafao yake kwani atakua na pesa ndefu itayompa nafuu ya maisha baada ya utumishi.

Swali la kujiuliza; Kama NSSF inatengeneza faida kutokana na uwekezaji wa michango ya wanachama wake kwenye miradi mbaliambali, kwanini mchangiaji asifaidike na hilo hata kupitia riba kwenye michango yake?

Hii haitakuza mfuko wa mwanachama pekee, bali itahamasisha hata wale ambao sio waajiriwa wataona umuhimu wa kujiwekea akiba kwa kupeleka michango yao NSSF.
 
Daah,umeongea Mambo ya msingi sana ila ndo bahati mbaya uzi umekosa wachangiaji....ila wabongo!
 
Huu uzi ni dhahabu kwa watanzania kama utafanyiwa kazi ...........

Kwa Tanzania kuna uwekezaji wa pamoja kama UTT AMIS , FAIDA FUND, INUKA FUND , M-WEKEZA etc ambayo riba yake kwa mwaka ni walau asilimia 12 ba kuendelea sasa kwanini mifuko ya jamii kama NSSF na PSSF wasiwekeze pesa za wachangiaji huku ili walau wafanyakazi wawekewe walau 8% kwa mwaka, kumbuka mifuko hii ya uwekezaji wa pamoja ina risk ndogo sana hivyo hakuna uwoga kwamba kutakuwa na hasara LENGO NI KUONGEZA RIBA ILI MCHANGIAJI APATE PESA YA KUTOSHA ANAPOSTAAFU...... NSSF@PSSF
 
Ingekuwa mada khs ushoga wachangiaji wangekuwa ukurasa wa 5 au 6
Vitu muhimu wachangiaji wachache
 
Back
Top Bottom