Ongeza spidi kwa 20% | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ongeza spidi kwa 20%

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MziziMkavu, Jun 8, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Kuna wakati unaweza kufikiria unaibiwa na mtoa huduma ya internet kwakuwa spidi ya internet yako inakuwa taratibu mno,wengine wamediriki hata kwenda kwa mafundi na kulalamika kuwa kompyuta yangu ina matatizo,kwani internet ipo slo mno.

  Je ni kwa nini haswaa?

  Kiufupi ni kuwa,ufanyaji kazi wa internet ni kama wa barabara,barabara ni moja ila kuna magari mengiyanahitaji kupita juu yake,hapa utaona kuwa kila barabara ina uwezo wake wa kubeba magari husika,magari yakizidi basi kunatokea foleni,kwenye internet nako hivyohivyo,data zikizidi kunatokea foleni na ndio maana unaanza kulalamika internet yangu ipo taratibu mno.

  Sasa tukilinganisha barabara na internet ni kuwa magari ndio data ambazo wewe unahitaji kuzipata,iwe video,iwe miziki toka online na vinginevyo.Uwezo wa hizi barabara kubeba magari kwenye internet ndio kinaitwa bandwidth,yaani data kiasi ganicha data zinaweza kutumwa kwa sekunde moja.Hizi data zinapimwa kwa bit au byte(1byte=8bits).

  Hivyo basi ili kupima uwezo wa kusafirisha hizi data(packets kwa lugha ya kiufundi zaidi) tunatumia bits kwa sekunde,yaani bits ngapi zinaweza kupita kwa sekunde.Sasa kutokana na ukuaji wa internet siku hizi spidi zimeongezeka na tunauwezo wa kusafirisha data nyingi kwa pamoja hivo vipimo vikubwa vya hizi bits vinahitajika na hapo ndipo kukaja matumizi ya vipimo vingine zaidi ambavyo vina uiano na hizi bits, kama unavyoonekana hapo chini.

  1 byte = 8 bits
  1 kilobyte (K / Kb) = 2^10 bytes = 1,024 bytes
  1 megabyte (M / MB) = 2^20 bytes = 1,048,576 bytes
  1 gigabyte (G / GB) = 2^30 bytes = 1,073,741,824 bytes
  1 terabyte (T / TB) = 2^40 bytes = 1,099,511,627,776 bytes
  1 petabyte (P / PB) = 2^50 bytes = 1,125,899,906,842,624 bytes
  1 exabyte (E / EB) = 2^60 bytes = 1,152,921,504,606,846,976 bytes

  Vipimo hivi sio tu vinatumika kwenye ulimwengu wa internet,bali pia hata kwenye ulimwengu wa kompyuta ambapo utasikia mtu anasema nimenunua diski ngumu yenye uwezo wa Gigabyte mia tano.Kumbuka jinsi unavyotoka juu kwenda chini ndio ukubwa unavyoongezeka,na ukubwa unavyoongezeka ndio uwezo wa ufanisi unavyoongezeka.

  Tukirudi kwenye mfano wetu wa barabara,chukulia leo hii kiongozi fulani anapita barabara ya Mandela kuelekea Ubungo,ili kuhakikisha mheshimiwa anapita bila tabu kuna hatua kama tatu zinaweza kuchukuliwa.

  1.Kuzuia njia nzima kwa siku nzima[​IMG]
  2.Kuzuia njia nzima pindi tu kiongozi anapokaribia
  3.Kuzuia sehemu ya njia na sehemu iliyobaki kuruhusu magari yapite kimsuli.

  Hizo njia tatu zilizotumika hapo juu kwenye internet tunaziita Ubora wa huduma(Quality of Service-QoS),lengo lake ni kuzipa kipaombele zile data muhimu kupita kwanza,mfano wa hizi traffics ni kama sauti,video,simu za conference nk.Siku hizi tumeshuhudia matumizi ya simu za online ambapo hutumia huduma ya VoIP.Traffic hizi mara nyingi haziwezi kuvumilia foleni,ndio maana kuna wakati unapopiga simu za online halafu humsikii mtu,hapa inamaanisha mtaalamu wao hajafanya kazi vizuri kama inavyotakiwa.

  Ukiachia msafara wa kiongozi,chukulia gari la wagonjwa linampeleka mgonjwa Muhimbili,trafiki akisikia king'ora tu inabidi asimamamishe magari mengine kwani huyu mgonjwa akicheleweshwa tu hatunaye,ambapo kwenye internet ndio hizo zinazoitwa mission critical traffic(haziwezi kusubiri kitu).

  [​IMG]Ukiangalia hatua tatu za juu ambazo polisi wa usalama wa barabarani anaweza kutumia,mbili kidogo zina unafuu,ila ile ya kuzuia njia nzima inaboa.Hivyo kwenye uhalisia wa maisha hutumika mara chache,hata kwenye kopmyuta zetu vilevile huwa tunaikimbia njia hii.Kwenye kompyuta zetu nyingi tunatumia hii ya wa tatu inayofanana na ile ya kuzuia sehemu ya barabara na sehemu nyingine kuruhusu magari kupita.Hivyo basi wewe unaponunua internet yako hautumii yote,unatumia kiasi tu na kiasi kingine huwa inawekwa kusubiri hawa wazee kama simu za voip na nyinginezo ambazo haziwezi kusubiri foleni.Sasa ni wangapi tumekuwa tukitumia hizo huduma? Jibu hapana,Je nini kinahitajika? Wote tuunafahamu jibu lake,'Kuziondoa mara moja',hehe.

  Leo hii nitakuonesha jinsi ya kuondoa hiki kizuizi ili kukuwezesha kutumia kiasi chote cha bandwidth kama uluvyonunua,ila kwa kufanya hivi unaweza kusababisha baadhi ya mambo yasiende sawa.Hivyo kama wewe ni mtumiaji wa hizi huduma zisizoweka kusubiri,kaa mbali na hatua inayofuata.

  Kwa kufuatisha hatua chache utawezakuongeza spidi ya internet yako kwa asilimia 20% bureeee.
  Twende sasa...
  [​IMG]1. Nenda start-> Run-> andika gpedit.msc

  2. Tanua kijitawi kilichoandikwa Administrative Templates

  3. Tanua pia Network tab

  4. Ichague QoS Packet Scheduler

  5. Bonyeza Limit Reservable Bandwidth na uchague(check) enabled box

  6. Baada ya hapo,badilisha Bandwidth limit % na kuweka 0 %

  Baada ya kumaliza unatakiwa kurestart kompyuta yako, hadi hapo utaweza kufaidi ongezeko la spidi ya kompyuta kwa kasi zaidi ya 20% ya ilivyokuwa awali,duh!.

  [​IMG]Je una maswali ya ICT ambayo bado yana kutatiza? Tuma kwenye AfroIT forums au andika moja kwa moja kwenye fahamuict@afroit.com nasi tunaandaa makala itakayoelezea matatizo yako.Makala hii ni shukurani kwa bwana James Mutashobi ambaye alitaka kujua ni jinsi gani ataweza kuongeza spidi ya internet yake.


  source: Technology--Ongeza spidi kwa 20%
   
 2. SHAROBALO

  SHAROBALO JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Yeah thanks

  Pia u waweza ongeza speed ya computer na Internet kwa kufanya hivi

  -repair registry
  -delete cache
  -etc

  this program is free and it do The best!!! CCleaner - Download
   
Loading...