One step foward, two steps back | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

One step foward, two steps back

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MpiganajiNambaMoja, Oct 15, 2008.

 1. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #1
  Oct 15, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi jamani agenda zetu za kitaifa ni zipi? Naamaanisha sisi kama Taifa nini tunataka ku achieve in 2010, 2015, 2020 etc.

  Nauliza hivi kwa sababu hivi karibuni nilikuwa nafanya utafiti mdogo kuhusu mfumo wa serikali toka enzi ya ukoloni hadi leo hii.

  Kwa karibu kiasi kikubwa mfumo wa serikali yetu haujabadilika kwa kiasi kikubwa tangu enzi hizo hadi sasa, regardless ya mabadiliko mengi ya kiteknolojia, uchumi na ya kijamii ambayo yametokea katika karne hii ya 21.

  Ni dhahiri kuwa mfumo wa sasa haukidhi mahitaji na unahitaji mabadiliko makubwa. Matatizo yote yanayotokea hivi sasa ni kwa sababu ya mfumo duni wa serikali (public sector).

  Mfano wingi wa tume ni dalili moja ya kuonyesha kuwa mfumo wetu haukidhi mahitaji. Katika hali ya kawaida kila kitu kinatakiwa kifanyike ndani ya mfumo wa serikali na hakuna haja ya kuunda tume kila siku au kila jambo lina potokea. Hivi ni mara ngapi umesikia Rais wa Marekani ameunda tume kuchunguza au kufuatilia jambo flani?

  Public sector ndo injini ya serikali; kama public sector haijakaa vizuri hakuna maendeleo yatakayopatikana. Mara nyigi tumekuwa tukijadili watu badala ya mifumo na hivyo tumekuwa tnapoteza mwelekeo na muda mwingi kujadili watu bila kujali hawa watu wanafanya kazi katika mazingira gani na wanaongozwa na mfumo gani.

  Mfano mwaka jana watu walimshikia bango aliyekuwa Director wa wanyama pori ndugu Emmanuel Severe. Severe alishikiw bango hadi hatimaye akaondolewa. Lakini baada ya kuondolewa Severe je tumeshaangali au tumeendelea kufuatilia nini kinaendelea katika idara hiyo muhimu inayo simamia mali asili ya wanyapori wetu?

  Kama tukifuatilia kwa makini, tutagundua kuwa tatizo halikuwa Severe, bali ni mfumo, sheria na taratibu za serikali yetu.

  Waandishi wote waliokuwa wanamshikia bango Severe hadi akaondoka hawajarudi na kuwaeleza wananchi mwaka mmoja sasa tangu Severe aondoke nini kimekuwa tofauti. Wamekaa kimya.

  Ni ukweli kuwa mtu kama mtu anaweza kuwa na upungufu na matizo yake kama mtu, lakini kwa kiwango kikubwa matitizo mengi ya serikali hayatokani na watu bali mfumo. Mfumo ndo una waruhusu hawa watu kufanya wanayofanywa kwa sababu hawabanwi.

  Katika utafiti wangu pia nimeona kuwa siyo kwamba serikali haijui kuwa mfumo wa sasa una upungufu. La hasha wanalijua hilo. Je ni nani anatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kurekebisaha huu mfumo?

  Katika report moja ya serikali nilipata hii!
  "By the early 1990s a consensus emerged that the shift towards a free-market economy (where the private sector was to serve as the engine of growth) needed to be better reflected in the structure and size of the nation’s public service. This consensus was expressed through the Civil Service Reform Programme (CSRP), which was officially launched in July 1991. The Programme, which ran until 1999, focused on COST CONTAINMENT and the RESTRUCTURING of Government. During this period some of the main changes included:
  A redefinition of Government roles and functions. A Local Government
  decentralisation programme began, Executive Agencies were created and
  non-core services were contracted out to the private sector. The exercise
  reduced ministries by 25 percent".

  Toka mwaka 2000 serikali imekuwa iki implement programu ya maboresho ya utumishi wa umma iitwayo PSRP. Pesa za hii programu kwa kiasi kikubwa ni mkopo kutoka World Bank. Serikali wakati inajua kabisa haina nia ya dhati ya kufanya maboresho katika sector ya umma bado imekuwa ikiendelea kutumia pesa za mkopo kufanya mambo ambayo haina nia ya kuyaendeleza.

  Mfano, moja ya mikakati ya maboresho ilikuwa kupunguza idadi ya wizara na kuweka wakala (agencies) ili kazi zifanywe na wakala badala ya mawizara. Ndo maana unaona wakati wa Mkapa agency nyingi ziliundwa kama EWURA, SUMATRA, TFDA n.k. na kulikuwa kuna nyingine nyingi ambazo ilitakiwa ziundwe ikiwemo ya Misitu, wanyamapori etc. Lakini baada ya kuingia Muungwana hakuna kilicho endelea.

  Ni ukweli kuwa wizara zimekaa kisiasa zaidi kuliko ki taalam, na haziwezi kutekeleza majukumu yake kikamilifu kama zina pokuwa agency. Lengo la kuwa na wizara chache kwa ajili ya ku oversee policies at high level na kuachia agency kufanya kazi halipo tena. Tuna kwenda mbele hatua moja, tunarudi nyuma hatua mbili.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,536
  Trophy Points: 280
  Japo sio kweli mbele hatua moja nyuma hatua mbili tungeshafika kwenye ujima. Ni mbele hatua moja nyuma nusu hatua. Maana yangu tunakwenda ila kidogo kidogo mno lakini hatimaye tutafika.
  Mipango ipo. Ile mipango ya maendeleo ya miaka mitano mitano bado ipo. Tuna Millenium Developments Goals kufikia 2015, na tuna Vission 2025.
  Tatizo kubwa ni utekelezaji. Katika kutekeleza haya ndipo ikaja PSRP I imeisha sasa tuko PSRP II. Tumeweka na baadhi ya mikakati kama MKUKUTA, MKURABITA na MKUMBITA ambayo yote bado inaendelea kufanya kazi ila taratibu.
  Nakubaliana na wewe kiutendaji bado tuko nyumasana na hizi tume tume ni weaknesses na ulaji. Hebu fikiria li nchi kubwa kama LiMarekani lina wizara 6 tuu ka nchi kadogo kama Tanzania kana wizara 38 mawaziri na manaibu wao 60!
  Katiba ya Marekani ya Mwaka 1776-imefanyiwa marekebisho mara 6 tuu mpaka sasa. Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977 imeshafanyiwa marekebisho mara 17!. Na Muafaka ukikubaliwa marekebisho ya 18 yanakuja kabla ya 2010.
  Hayo yote ni uthibitisho bado tunacheza makida makidamakida ila tutafika tuu. god knws when.
   
Loading...