Ondoa kumbukumbu ya vitu ulivyo tafuta mtandaoni

Ondoa kumbukumbu ya vitu ulivyo tafuta mtandaoni

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,347
Reaction score
2,754
Futa History ya Google search kwenye iphone na Android

Unahitaji kuondoa histori ya vitu ulivyovitafuta kwenye google search kupitia , chrome , Mozilla , Safari nk ili watu wasijue ulikua unatafuta Nini ?

Najua umeshawahi ku search kitu google sema shida unakuta historia yake bado ipo Yani ukitaka kutafuta kitu kipya basi vya zamani utaona vimetokea vingi chini.

Kuna baadhi ya taarifa ulizotafuta kupitia Google search utaki watu wajue [emoji2], unajua Kuna baadhi ya taarifa Huwa ni siri sio Kila Mtu ajue umetafuta Nini mtandaoni !!

Unajua google Wana hifadhi Kila kitu kwenye Seva Yako wakati unatafuta we ukiandika TU sijui jinsi ya kupata pesa , jinsi ya kutongoza nk basi google wana hifadhi hawaachi kitu.

[emoji820]Watumiaji wa Iphone
Ingia kwenye Google my activity >> utaona activity zote unazozifanya kupitia Google >> Gusa kwenye Delete Iko upande wa kulia juu ya activity.

• Gusa All time Kisha >> Next alafu >>delete. Hii itaondoa vitu vyote ulivyovitafuta mtandaoni kwa mara moja. Pia unaweza kuweka automatic delete ingia manage your account >> Data & privacy >>>history setting >>Gusa auto delete Kisha next alafu confirm.

[emoji820]Watumiaji wa Android
Fungua Google chrome >> Gusa vidoti vitatu Iko upande wa kulia juu Kisha>> chagua History >> clear Browser data Kisha utachagua All time >> clear data

[emoji820]Watumiaji wa kompyuta | laptop
Fungua browser Yako Kisha ingia kwenye manage your account from Gmail au Gusa Vidoti vitatu kwenye kivinjari Cha Chrome.

Gusa kwenye history >>utaona shughuli zote ulikua unazifanya kupitia Google utaweza kufuta Kila kitu kwa kubonyeza clear Browsing Data

Kuna wakati sio Kila unachokitafuta mtandaoni lazima ukiache unaweza kuzindoa TU baadhi ya taarifa !!

Teknolojia ni Yetu sote
 
IMG_20220515_200159_176.JPG
 
Back
Top Bottom