Ona Mchezo wa Kibati ulivyo Madeni pasua kichwa kwa taswira nyingine.

Fya-fyafya

Member
May 2, 2019
43
125
Mchezo wa Kibati ni mchezo wa waminifu ambao watu wawili au zaidi hucheza kwa kupeana hela/ fedha kwa zamu.

Zamu hizo hufanyika kwa mzunguko wa siku fulani kutokana na makubariano ya wachezaji wenyewe.

Hapa nchini, katika makundi tofauti ya jamii, nchezo huu umekuwa maarufu sana kwa kuchezwa na watu hasa wenye nia na lengo moja la kujikwamua kimaidha.

Aidha, mpaka Sasa kuna kundi kubwa la watu tena wengi tu ambao hawauelewi kabisa huu mchezo. Yaaani hawaelewi moja kwa moja faida zake na hudhani kuwa kuvheza kibati ni pengine kujipotezea muda, hivo Basi hawachezi. kuna na wengine nao wengi tu wanauelewa huu mchezo na wanaucheza na hawaoni Sababu za kuacha na hawaji kuachakucheza.

Baada ya utangulizi huo, Sasa twende Kwenye maada husika isemayo :" Ona Mchezo wa kibati ulivyo Madeni pasua kichwa kwa twaswira nyingine."

Deni ni mali, kitu, fedha au kitu chochote cha mtu mwingine kwa njia ya makubariano au vinginevyo unachomiliki au ulichotumia nk kwa maana ya kukirudisha tena kwa mtu huyo aliekupa. Au kwa maana nyepesi, Deni ni kitu au pesa unayodaiwa.

Mchezo wa kibati unakuweje tena Deni na tena deninpasua kichwa? Hii ni kutokana na hali ya Mchezo wenyewe: yaani watu wawili, wa tatu, wa nne au zaidi (vibati vingine huwa na members Hadi 50! ) Kuchanhishana pesa walizokubaliana na kumtoa (kumpa) mmoja wao au wawili kadri wali yokubaliana.

Hii inakuwa Deni kwa maana kwamba ; mtu akipokea pesa leo maana yake hii pesa aliyopata ni ya wenzake. Kwa hiyo zamu inayofuata na kwendelea atazidi kuzurudisha kwa awamu kwa wale walompa.

Kwa mfano kibati kina watu wa tano (05) na aamekubaliana kucheza kibati sh. 50. 000 kila mwezi. Maana yake kila mwenye zamu ya kupewa hela atakuwa anakabidhiwa sh 200.000 maa yake elfu hamsini hamsini za wenzie wanne.

Hicho kibati alichopewa cha sh. 200000 ni Kama Deni au mkopo usio na Riba ambao ataurudisha ndani ya miezi minne (04) mfururizo.

Hii na maana kwamba: kwa mfano mwezi huu ndo amepokea Basi mwezi ujao ataanza na kwendelea atakuwa anatoa laki moja moja kwa miezi hiyo minne mfururizo kwani itakuwa ni miezi ya vibati vya wenzie. Kwa maa niyo Basi hela ya kibati haikai mfukoni! Inaingia na kutoka!

Kwa maana hiyo Basi, Mchezo wa kibati unakuwa na sura mbili ambazo ni kutunziana au kushikiana pesa kwa muda au kukopesha pesa bila Riba.

Changamoto za Mchezo wenyewe.

1. Ukosefu wa waminifu.

Hii hujitokeza sana pele wacheza kibati wenyewe wanaposhindwa kupeana pesa kwa muda . Kwa uchunguzi kidogo ulofanywa ni kwamba kwenye kibati, kiwe cha watu wawili , wa tatu ama zaidi; kunatokea baadhi ya washiriki ambao huwasilisha pesa zao too late.

Kwa mfano Memba X anapewa pesa leo lakini hapewi mpaka pengine juma mosi kwa sababu tu wote hawajamalizia kutoa hela. Kwa ujumla kunakuwa na hali ya baadhi ya members kujivuta kuchanga hasa wale ambao zamu zao zilishapita! Hivo hukwamisha wenzao.

2. Kugombania kuwa wa kwanza kupokea kibati.

Katika vibati vingi, kuna hali ya marumbano ya kila memba kutaka kuwa wa kwanza kupokea kibati. Yaaani kila mtu anataka ile day one kibati kimeundwa Basi yeye awe wa kwanza kukusanyiwa mupunga😀.

Hivo inasemekana huchukuwa muda kido wote kuafikiana nani awe wa kwanza maana kila mmoja hutoa shida zake za maana akikomvisi wengine ili hatimae apewe wa kwanza au awe wa pili Kama ni wengi.

Pia, inaelezwa kuwa kuna hali ambayo inajitokeza ndani ya Safari ambapo mtu zamu yake ni ya nne (04) au ya mwisho na halafu ndo kibati kipo zamu ya pili Sasa mtu huyo anaomba kubadilishiwa zamu ili yeye achukue zamu hiyo ya pili huku akisema amebanwa hana kitu na hana yakutoa.

Hii humwathiri yule mwenye zamu yake maana nae pia alikiwa amevumilia kwa kuto pesa Kwenye zamu za watu wengine bila kuchoka na alikuwa akisubiri zamu yake.

3. Zamu kuishia njiani

Kibati chenye watu wengi kuanzia wa tatu na kuendelea huwa kinakuwa na changamoto Nyingi ikiwemo ya zamu kukwama na kuishia njiani hivo kuleta tafrani na marumbano.

Hii hujitokeza pale ambapo wale members ambao walishachukua mpunga Kwenye zamu zao wanapoishiwa pesa pindi wanapotoa au kurejesha kwa zamu za watu wengine.

Watu wengi wakipokea kibati hutumia hiyo hela kujikwamua kiaisha Kama vile: kununua dhamani na vyombo vya ndani, kulipa Ada, kulipa Kodi ya nyumba, kufanyia starehe n.k .

Watu hao wanasahau kuwa hiyo hela ni ya watu na wao watawajibika kurejesha au kuchangia wengine Kwenye zamu zao!

Watu Sasa wanajikuta hawana hela ya kuchangia wenzao wa zamu inayofuata. Kwa hali hiyo Basi humcheleweshea mwenzao wakisahau kuwa huyo wanaemcheleweshea alikushawachangia pesa Kwenye zamu zao.

Wengine hufika mbali mpaka kibati kinasimama na kuanza kipelekana kwa Balozi, kwa mwenyekiti wa mtaa au kwa mtendaji kata.

My takes:

Hela ya kibati si ya kuchezea. Hello ya kibati ni mkopo usionariba, unaorudisha haraka kwa wenzako tena kwa mfururizo.

Ni hela ya kutumia kwa making tena kwa wangalifu kutokana na kipato chako ili kuepusha aibu na misuguano na wato mloaminiana pale mwanzo mlipokuaa mnaanza hicho kibati.

Cheza kibati ambacho hakitoathiri maisha yako baada ya kurejesha au kuwachangia wenzako. Usije ukacheza kibati ambacho kiko juu ya kipato chako ili kuepuka kukopa kopa pesa huku na kule ili tu upate ya kibati. Ukikosea tu utahatarisha familia yako na Ndoa kwa ujumla.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom