Ona maajabu ya siasa za tanzania

Mar 21, 2013
37
0
Kuna kitu kinashangaza sana kwenye siasa za Tanzania.Unakuta Mwanasiasa wa Tanzania ameharibu katika utendaji wake wa Kisiasa either Serikalini Mf Eddo alipojiuzuru Uwaziri Mkuu kutokana na Kashfa ya Richmond,Chenge Mzee wa Vijisenti na sasa ZZK aliyevuliwa nyadhifa zake zote za Uongozi ndani ya CHADEMA.

Mwisho wa Siku wariporejea Majimboni mwao wengine kwa kusapotiwa na Magamba katika Mapokezi yao yasiyo na bendera hata moja ya Chama chao.

Wananchi wa Majimboni mwao wamekuwa wakiwakumbatia kwa kigezo cha MWENZETU bila hata kuangalia na kuwahoji kwa Makosa waliyowafanyia Watanzania au vyama vyao.

Wengine wamechinjiwa hadi Ng'ombe na Sherehe kubwa kana kwamba walichowafanyia Watanzania ni sahihi.Rai yangu Watanzania tusiingie kwenye mtego wa Udini,Ukabila/Umwenzetu katika kutetea uozo bali tuangalie Hoja.

Nasema hivyo kwa sababu haiingii akilini mfano mimi kama Msukuma[japo sipendi kutumia kabila kujitambulisha] nimtetee bwana SHIBUDA akikutwa na hatia eti kwa Upuuzi wa Msukuma Mwenzangu bila kujikita kwenye Maadili na Utaratibu wa Chama.

Tusiwatetee watu kwa kigezo cha Makabila au dini zetu tujikite kwenye hoja ya Msingi kwa Masilahi mapana ya Taifa letu.Gutter politics [Siasa za Majitaka] zilizoasisiwa na Magamba ili watugawe na Watutawale tusiziruhusu kamwe.

Tusifiche Madhaifu ya Viongozi wetu kwa propaganda za Udini/Ukabila.Wananchi wa kawaida tusirubuniwe na Wanasiasa Uchwara/Matapeli wa Kisiasa kwa kutumia UNYUMBANI/UMWENZETU.
 

Sometimes

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
4,541
1,500
Mkuu tume elezwa kuwa ng'ombe akiumia machungani,hurudi zizini kwake kuhudumiwa. Itashangaza sana kama akirudi zizini apate mateso zaidi ya kutibiwa au kuliwazwa!
 

Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,992
2,000
Mkuu tume elezwa kuwa ng'ombe akiumia machungani,hurudi zizini kwake kuhudumiwa. Itashangaza sana kama akirudi zizini apate mateso zaidi ya kutibiwa au kuliwazwa!

Mkuu kwa hiyo unamaanisha ni faraja tu si ndivyo?
 

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,994
2,000
hata wanamkosoa Zitto wajikite kwenye "kweli" na "haki" lakini jambo la kushangaza wengi wao huongozwa na ushabiki ktk kumkosoa Zitto, ndio maana hawana hoja zaidi ya viroja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom