Ona haya ya elimu

Securelens

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
316
541
Kila kona ya nchi yetu, watanzania wanafurahia kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Mheshimiwa Rais Magufuli katika sekta ya elimu ikiwemo kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari Mpaka mwezi Februari 2020, serikali iligharamia malipo hayo kwa shilingi trilioni 1.01 ikiwa inatoa wastanin wa bilioni 23 kila mwezi kulipia elimu hiyo kwa watoto maskini wa wakitanzania.

Mbali na kutoa elimu bure, serikali ya Mhe Rais Magufuli imeongeza idadi ya shule za msingi kutoka 16,899 mwaka 2015 hadi 17,804 mwaka huu; na shule za sekondari kutoka 4,708 mwaka 2015 hadi shule 5,330 mwaka 2020. Vilevile, serikali mekarabati shule kongwe za sekondari 73 kati ya 89. Shule hzo sasa ni nzuri san ana ukarabati kwa shule zilizosalia unaendelea.

Katika kuboresha mazingira mazuri ya masomo kwa Watoto wetu, serikali imejenga mabweni 253 na vyumba vya maabara ya 227. Aidha, serikali ya JPM metoa vifaa kwenye maabara zipatazo 2,956 na imepunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa madawati, ambapo idadi yake imeongezeka kutoka madawati 3,024,311 mwaka 2015 hadi kufikia 8,095,207; sawa na ongezeko la zaidi ya asilimia 200.

Utawala wa Mheshimiwa Rais Magufuli pia umeongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu kutoka shilingi bilioni 348.7 mwaka 2014/2015 hadi shilingi bilioni 450 mwaka wa Fedha 2019/2020

Kutokana na hatua hizo, uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza umeongozeka maradufu kutoka wastani wa wanafunzi milioni 1 mwaka 2015 26 hadi kufikia milioni 1.6 hivi sasa. Aidha, idadi ya wanafunzi wa kidato cha I – IV imeongezeka kutoka 1,648,359 mwaka 2015 hadi 2,185,037. Idadi ya wanafunzi wa VETA imeongezeka kutoka 117,067 mwaka 2015 hadi 226,767 mwaka 2020; na idadi ya wanafunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) imeongezeka kutoka 6,693 mwaka 2016/17 hadi 9,736 mwaka 2018/19.

Kwa upande wa vyuo vikuu, idadi ya wanafunzi wanaojiunga mwaka wa kwanza imeongezeka kutoka 65,064 mwaka 2015 hadi 87,813 mwaka 2020; na wenye kupata mikopo wameongezeka kutoka 98,300 mwaka 2014/2015 hadi 130,883 mwaka 2019/2020. (Takwimu zote ni kwa mujibu wa hotuba ya Mhe Rais Magufuli wakati wa kufunga Bunge tarehe 16 Juni 2020)

Ubora wa elimu pia umeongezeka sana kutoka na uwekezaji wa elimu uliofanywa na Serikali ya JPM. Mwezi Agosti mwaka huu tulishuhudia katika matokeo ya mtihani wa kidato cha Sita, katika shule 10 bora kitaifa, shule za Serikali zilikuwa 8 na shule mbili tu za watu binafsi. Na katika shule hizo 8 za serikali shule 3 ni za kata ambazo ni Kasimiri, Mwandeti na Dareda . Shule kongwe za serikali katika orodha hiyo ya kumi bora zilikuwa ni Mzumbe, Shule ya wasichana Tabora, shule ya wavulana Tabora, Iiliboru na Kibaha.

Viva Mhe Rais Magufuli. Watanzania tunakwenda kukuchagua kwa kura nyingi Oktoba 28 ili tuendelee kupata elimu bila malipo na mikopo ya masomo vyuo vikuu tena inayotolewa kwa wakati bila kusubiri kwanza migomo. Tunakwenda kukuchagua ili shule za serikali ziendelee kung’aa katika ubora. Tukikupa miaka mitano mingine tutashuhudia watanzania wakipendelea zaidi watoto wao wasome shule za serikali kuliko shule binafsi kama ilivyokuwa zamani. Tutakuchagua wewe mwana maendeleo. Watanzania wapenda maendeleo tumchague Rais Magufuli.
 
Hongera kwa kuandika makala ndefu. Lkn pole Sana. Maana watanzania tumeamua tunataka mabadiliko.
 
Back
Top Bottom