Kuna tatizo gani kutumia wikipedia wakati inatoa mwanga wa kutosha kuhusu sexual harassment? Huwezi kumfungulia mtu mlango ikawa sexual harasment. Mimi ninaishi nao hapa na wanafunguliwa milango kila siku na wanapenda kweli kweli. Labda hatuelewani maana ya kufunguliwa milango. Sijui majimbo mengine, lakini jimbo ninaloishi mimi sexual harasment poster zipo kila kona. Mtu akiajiriwa anapewa ki-poster cha sexual harassment na kufunguliwa mlango siyo moja wapo.
Ukitoka na demu kwa mara ya kwanza, ukimfungulia mlango wa gari itakuwa sexual harassment?
Suala la huyu mmarekani litaangaliwa kutokana na sheria zetu kama lina fit definition yetu ya sexual harassment au hapana.
Tz_devil,
Nafikiri ungesoma nilichoandika, mimi nimesema kazini. Sijasema girfriend au ndugu. Lakini hata huko kazini haina maana ukimfungulia mlango msichana basi atasema umemfanyia sexual harassment.
Inatagemea na wakati gani na kwasababu zipi. Kwa mfano ukitangulia mbele utamfungulia, na yeye siku zingine akitangulia anaweza kufungulia mlango wanaume.
Lakini hapa Europe kuna nchi ambako kumfungulia msichana mlango ni sehemu ya culture zao, wasichana kama wameongozana na wavulana, wakifika mlangoni unaona wanasimama, wanategemea hata kama ulikuwa nyuma basi unaenda mbele na kufungua mlango. Hata kama hamfahamiani ila mumeongozana tu wakati wa kufika mlangoni. Usipofanya hivyo watakushangaa, unaonekana hujastaarabika. Waingereza kwasasa wako neutral juu ya hilo.
Hicho ndicho ambacho makampuni ya Marekani, na hasa kwa Europe wanakifundisha kama njia ya kujihami na cases za sexual harassment. Hata Wamarekeni wenyewe wasichana wasingelitaka hilo.
Nina uhakika wasingepoteza mapesa kufundisha kitu ambacho hakina madhara, kwa vyovyote kuna cases kama hizo zimetokea sehemu na ili kuondoa risk ya liabilities kwa kampuni wanatoa training ili
hata ukipatikana na hatia basi uwe wewe as an individual na wala sio kampuni.
Kuhusu wikipendia, ni kwamba kwenye professional documents wanaona wikependia sio reliable kwahiyo mara nyingi huwezi kutumia kama reference.
Sasa ulitaka suala la kufungua mlango lifundishwe USA? Kwa USA hilo sio tatizo kwani hiyo sio culture ya Wamarekani kwamba lazima umfungulia mwanamke mlango.