On Tarnishing Tanzania;- A US student Sexual harassment | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

On Tarnishing Tanzania;- A US student Sexual harassment

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Choveki, Dec 9, 2007.

 1. C

  Choveki JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2007
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Baada ya kusoma ile ishu ya mmarekani chuo cha sanaa nimeona nipost hii inayohusu University of Dar es Salaam na sexual harassment ati wazipatazo wanadada:

  Sijui kama kuna ukweli au vipi, ila huyu mwanadada mmarekani anasema kweli yamemtokea.

  Kwa kifupi tu soma hapa;

  "....When Rachel Jamison received a full scholarship to study in Tanzania for a year, she said University officials told her to expect intense sexual harassment.
  An experienced world traveler, Jamison said she thought she knew what to expect. .....But repeated rape attempts, catcalls and assaults were more than she could have anticipated......."


  Link kamili:
  http://www.mndaily.com/articles/2007/02/27/70948
   
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mimi nimefanya kazi kwenye kampuni ya Wamarekani hapa Europe kwa miaka saba, wanavyoelewa sexual harassment ni tofauti sana na tunavyoelewa hapa Europe.

  Hata kumfungulia mlango mwanamke, wao walikuwa wanaona shida, mkiwa kwenye mkutano, ukimwachia kiti na wewe kwenda kutafuta kingine ilikuwa ni sexual harassment.

  Wakati kuna nchi za Europe, mkifika mlangoni, wanawake wanasimama wakisubiri wanaume wafungue mlango, au hata darasani kama kuna viti vichache wanaume inabidi wasimame ili dada zao wake.

  Bahati wengine tulikuwa tunasoma culture za Marekani ili kuondoa matatizo. Inatakiwa hawa wanaoenda TZ wasome japo kidogo culture zetu kabla ya kwenda ili wasipate culture shock.

  Kuna mambo kweli hata kwa dada zetu waliokulia katika hayo mazingira hayafai, lakini mengine naweza kusema ni kutokuelewa culture ya sehemu husika.
   
 3. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2007
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii nayo si ingeunganishwa na ile nyingine?

  Tusisahau, pamoja na matatizo ya mazingira, hawa wenzetu pia wapo kutafuta ulaji kama nafasi inajitokeza. Kwa mfano huyu, inaelekea analenga kujipatia chochote kutokana na kutopewa taarifa zote na chuo chake kabla ya kuja Dar. Anatafuta 'loophole' ya kuwanasa.
   
 4. P

  Pedro Senior Member

  #4
  Dec 9, 2007
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 114
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika kuzijua culture zetu kabla hawajaja ni muhimu, lakini mtu anakuja ku-register katika darasa halafu huyo clerk anamwambia niachie tako ndo niku-register hizo jamani sio culture zetu Tanzania hata kidogo, huo ni uhalifu wa kupigwa vita kabisa.
   
 5. C

  Choveki JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2007
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hata mimi mwanzoni nilitaka kuziunganisha, nikadhania inaweza haribu ule mjadala mwingine, ndiyo baadaye nikaamua niipe kichwa cha habari kinachoshabihana na ile nyingine kutilia mkazo zinzvyofanana, na pia unyanyasaji wa kijinsia ili inavyotofautiana. Pi hii ilijadiliwa kwenye gazeti la huko USA, MINNESOTA DAILY, wakati ile nyingine imetoka magazeti ya tanzania, ila kwa kiasi kikubwa zinafanana.
   
 6. t

  tz_devil JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2007
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 272
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Siyo kweli, wanawake wanafunguliwa milango hapa Marekani na wanapenda kweli. Kumuachia kiti mwanamke does not constitute to sexual harassment in the US. Tafadhali angalia hii link:

  http://en.wikipedia.org/wiki/Sexual_harassment
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  It has been suggested that the term "sexual harassment" was coined in 1974 at Cornell University

  Naona ni cultural perceptions tofauti. Haya maneno yametoka huko2- gender empowerment, feminisim, racial profiling etc. Hao kabla ya kuja Tz yabidi waelimishwe kwanza- hayo mambo yao ya vitabuni ni tofauti na hali halisi ya mila na tamaduni zetu. Nimesoma Tz sikuwahi kusikia dada zetu wakisema wamekuwa harassed eti kwa kuwa vijana wanawataka kimapenzi!
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tz_devil,

  Unatumia wikipendia kupata maana ya sexual harassment?

  Nina uhakika na nilichosema, nilikuwa nafanya kampuni kubwa, yenye wafanyakazi zaidi ya 150,000 kwenye telecom, na hivyo vitu tulikuwa tunafundishwa hapa Europe. Hata Wamarekani wenyewe walikuwa wanasema wazi kwanini umfungulie mlango?

  Sexual harassment kwa Wamarekani ni kubwa mno kuliko wikipendia wanavyosema, of course hutakuwa accussed kwasababu umemfungulia mwanamke mlango mara moja. Lakini hiyo inaweza kutumika kama sababu ya kuwa accussed au kampuni kushitakiwa.
   
 9. t

  tz_devil JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2007
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 272
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kuna tatizo gani kutumia wikipedia wakati inatoa mwanga wa kutosha kuhusu sexual harassment? Huwezi kumfungulia mtu mlango ikawa sexual harasment. Mimi ninaishi nao hapa na wanafunguliwa milango kila siku na wanapenda kweli kweli. Labda hatuelewani maana ya kufunguliwa milango. Sijui majimbo mengine, lakini jimbo ninaloishi mimi sexual harasment poster zipo kila kona. Mtu akiajiriwa anapewa ki-poster cha sexual harassment na kufunguliwa mlango siyo moja wapo.

  Ukitoka na demu kwa mara ya kwanza, ukimfungulia mlango wa gari itakuwa sexual harassment?

  Suala la huyu mmarekani litaangaliwa kutokana na sheria zetu kama lina fit definition yetu ya sexual harassment au hapana.
   
 10. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tz_devil,
  Nafikiri ungesoma nilichoandika, mimi nimesema kazini. Sijasema girfriend au ndugu. Lakini hata huko kazini haina maana ukimfungulia mlango msichana basi atasema umemfanyia sexual harassment.

  Inatagemea na wakati gani na kwasababu zipi. Kwa mfano ukitangulia mbele utamfungulia, na yeye siku zingine akitangulia anaweza kufungulia mlango wanaume.

  Lakini hapa Europe kuna nchi ambako kumfungulia msichana mlango ni sehemu ya culture zao, wasichana kama wameongozana na wavulana, wakifika mlangoni unaona wanasimama, wanategemea hata kama ulikuwa nyuma basi unaenda mbele na kufungua mlango. Hata kama hamfahamiani ila mumeongozana tu wakati wa kufika mlangoni. Usipofanya hivyo watakushangaa, unaonekana hujastaarabika. Waingereza kwasasa wako neutral juu ya hilo.

  Hicho ndicho ambacho makampuni ya Marekani, na hasa kwa Europe wanakifundisha kama njia ya kujihami na cases za sexual harassment. Hata Wamarekeni wenyewe wasichana wasingelitaka hilo.

  Nina uhakika wasingepoteza mapesa kufundisha kitu ambacho hakina madhara, kwa vyovyote kuna cases kama hizo zimetokea sehemu na ili kuondoa risk ya liabilities kwa kampuni wanatoa training ili
  hata ukipatikana na hatia basi uwe wewe as an individual na wala sio kampuni.

  Kuhusu wikipendia, ni kwamba kwenye professional documents wanaona wikependia sio reliable kwahiyo mara nyingi huwezi kutumia kama reference.

  Sasa ulitaka suala la kufungua mlango lifundishwe USA? Kwa USA hilo sio tatizo kwani hiyo sio culture ya Wamarekani kwamba lazima umfungulia mwanamke mlango.
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2007
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Haya, ngoja nijiingize kichwa kwenye kitanzi!

  Hivi kweli wakina dada katika jamii yetu wanatendewa haki? Kwa bahati mbaya sehemu kubwa ya jamii yetu bado ina dhana kuwa mwanamke amewekwa ili awe asusa ya mwanaume! Wale tuliopitia JKT tutakumbuka jinsi mabinti walivyokuwa wakilazimishwa ( kwa kuadhibiwa kundi zima, kupewa upendeleo wa kijinga n.k) kutembea na maafande.

  Nakumbuka kuna watoto wadogo tuu walioingia kwa kuijtolea kutoka vijijini na suluba waliyokuwa wakiipata mpaka wamtimizie haja afande. Tunakumbuka jinsi mabinti walivyokuwa wakichaguliwa kuwahudumia wakubwa wakija kutoka makao makuu! Haya yote tuliyaona na kuyanyamazia kwa sababu tuliamini kuwa hawa wakina dada waliyataka. Wale waliopita mlimani watakumbuka vitendo alivyokuwa akivifanya Mr. Punch, kuwaanika wakina dada ati katika misingi ya kuwarekebisha tabia. Ukifika maofisini si jambo la kukataa kuwa kuna wengi tu ambao wanatumia nafasi zao kutembea na wale walio chini yao.

  Tunajua wote kuwa ni wengine wakisafiri shurti anakoenda atafutiwe blanketi na wenyeji wake. Wengi wetu ingawa tu wakali kuhusu binti zetu lakini hatuoni tatizo kuwafanyia vitendo vya aibu na kutumia maneno ya ajabu visichana vilivyo na umri mdogo kuliko hao binti zetu kwa sababu tu hawa wanafanya kazi katika kumbi za starehe.

  Mara ngapi tumesikia dada amevuliwa nguo akitembea mtaani ati kwa kile ambacho wahusika wameona amevaa nguo ambazo haziwapendezi? Mifano ni mingi tuu na wote tunaijua na kwa bahati mbaya tumeikubali (wake kwa waume)kuwa ndiyo hulka yetu. Wakija wenzetu wanaokataa kufanywa chachandu (?) kwa sababu tu amezaliwa mwanamke tunaona anatutukana! Tumezoea kujiona kuwa sisi ni God's own gift to humanity.

  Nadhani imefika wakati tujiangalie kwenye kioo kama jamii na tuanze kuwapa heshima wanayostahili na kuwaenzi dada na mama zetu.
   
 12. C

  Choveki JF-Expert Member

  #12
  Dec 10, 2007
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Pokea tano Mchundo!

  Hapo umenena, nadhani ndiyo tatizo ambalo linakabili jamii nyingi za kiafrika, umetumia neno "asusa ya mwanaume", na ndiyo maana kwa wale waliopo au waliopitia vyuoni kuna kitu kinaitwa maksi za chupi! Si hata baadhi ya viongozi wetu wa kike wamekuwa wanasemwa semwa kuwa wamepewa hivyo vyeo kwa sababu hizo hizo?
   
 13. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35


  ...ukware..........!!!!!!!!!!!!!!
   
 14. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  in short, most female students at UDSM who are victims of sexual harrassment are consenting to the act,whether you like or not....
   
 15. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  True True Mkuu.
   
 16. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  what a F.C.I.G political thread!
   
Loading...