On a serious note: kutetea umachinga ni ushujaa?

On a serious note: kutetea umachinga ni ushujaa?

iringa is very fertile, Msigwa could use this advantage to motivate these strong and energetic young men to untite and make something out of farming or agricultural activties.

kuwafanya wana Iringa sawa na wamachinga wa dsm ambako hakuna space for kilimo ni failure kubwa sana kwa mbunge

yet shujaa??
Naafiki na mantiki ya wazo hili.
Hivi ni lini ndugu zetu wa Iringa walitoka kwenye kundi la The Big Four ya wazalishaji wakuu wa chakula nchini?

Cheap thinking and an equally cheap solution makes Mch Msigwa a novice katika Tanzania politics.
Vijana Iringa watakufa njaa kwa sababu hakuna political initiative ya kuwa galvanise into a production force.

Umachinga is basically a begging initiative.
Ni aibu.
 
Nimesoma thread nyingi sana za wadau, mengi yamesemwa na ni reflection halisi ya dhana ya umachinga na uchumi wetu. Bila shaka mnamkumbuka comrade mwananzuoni prof. Chachage. S. Chachage (late) aliwahi andika kitabu chake ''makuwadi wa soko huria'' hebu jaribuni kukitafuta na mkisome kwa umakini wana jamvi mtajua nini maana ya umachinga na hatma ya uchumi wa mlala hoi. To remove ignorance we start with conscious habit of learning. Ahsanten.
 
Naafiki na mantiki ya wazo hili.
Hivi ni lini ndugu zetu wa Iringa walitoka kwenye kundi la The Big Four ya wazalishaji wakuu wa chakula nchini?

Cheap thinking and an equally cheap solution makes Mch Msigwa a novice katika Tanzania politics.
Vijana Iringa watakufa njaa kwa sababu hakuna political initiative ya kuwa galvanise into a production force.

Umachinga is basically a begging initiative.
Ni aibu.

Hivi tukiwaondoa hao vijana mtaani, wataenda kulimaee. Au unadhani hawafanyi kilimo ksbu ya kufanya umachinga?
 
Erosion ya thinking katika safu ya wawakilishi wa wananchi sasa inaelekea kubaya-kwa maoni yangu!

Kwa mtu anayeelewa jinsi dhana nzima ya umachinga ilivyo asingeitetea kama mkombozi wa wananchi wasio na uwezo.
Thinking ni kwamba kwa vile barabara zipo, kwa hiyo kuna wateja barabarani, mtu hakodi cha kuweka tumboni.
Cheap thinking just as it is cheap attempt at appeasing political supporters.

Hebu tuichunguze dhana nzima ya umachinga.
Hii ni outlet of goods bila ya record za aina yoyote, kwa wasomi wa siasa ni kama kutetea anarchy, a political status quo ambayo hakuna control ya aina yoyote.

Kuna ukiukwaaji mkubwa wa kodi katika dhana hii ya umachinga, kwa vile records za bidhaa zilizoingizwa nchini, na ufuatiliaji wake wa kodi huwa hakuna.

Sasa kutetea hali hii inaleta wasiwasi kwa jamii yoyote ile.
Ni vema ikajulikana kuwa kama kuna kulipa kodi basi kila mtu asilipe ili iwe survival for the fittest.
Ni wazi kwa mtindo huu taifa linajinyonga lenyewe.

Tutofautishe kati ya wamachinga na dhana ya umachinga.

Wamachinga , originally kutoka Lindi ni kundi la vijana waliokosa kazi ya kuwapa ajira ya maana.

Hivyo basi ni vema wanasiasa wetu wakajikita katika kutatua tatizo la kuwapa vijana wetu matumainio ya maendeleo kwa kukuanzisha miradi yenye tija na manufaa kwa jamii.

Kutetea vijana kukaa vibarazani mwa wahindi au barabarani kuuza njugu na viatu hadi mitumba ni kujipatia umaarufu usio na tija. Ni kama kuvuta bangi ya kisiasana kutegemea matatizo yatapotea yenyewe.
pHakuna shortcut ya kutatua matatizo ya vijan wa nchi hii, na umachinga siyo solution.


UNAWEZA KUWA UNAJARIBU KUWAZA VEMA; LAKINI TULIFIKA VIPI HAPO? NA TUNAONDOKA VIPI HAPO BILA KUIUMIZA JAMII YA WATZ WANAOISHI KWA MTINDO HUO? JE KUNA MKAKATI WA KIELIMU, KISIASA NA KIJAMII KUTUTOA HAPO? JE NINI FOCUS YA KITAIFA KUKABILI HALII HII? AU NDO MAWAZO MEPESI KWA MAMBO MAZITO KIASI HIKI? JE JAMBO HILI HALIBEBI MUSTAKABALI WA AMANI YA NCHI HII? N.K. ANGALIZO KABLA HAUJAMPONDA MTU TAFAKARI KWANZA!!
 
Wawakilishi wetu wanawakilisha mawazo mbadala ambayo una choice ya kuyaafiki au kutokubaliana nayo lakini yakiwa yamewakilishwa. Mawazo unayoyataka wewe haimkini yamewakilishwa na umeridhika yalivyowakilishwa. "Erosion ya thinking" ina maana mmomonyoko wa fikira nikitafsiri neno kwa neno. Fikra hazimomonyoki ila zinadumaa (conservative), au zinabadilika kuwa bora au kuwa dhaifu ndiyo maana ya fikra mbadala.



Umejikita kwenye event ya barabara na tukio la Iringa ambalo hutaki kulitaja. Dhana kiswahili sahihi inanyumbulika kudhania, n.k "Tumekuwa tunadhania kwamba tuna fikra sahihi ya kuendesha nchi yetu kwa fikra za chama cha mapinduzi; sasa tunadhania vyama vya upinzani vinatoa mwelekeo mpya kuhusu maendeleo yetu" Dhana kimsingi ni mawazo tu ambayo yanaweza kuwa sahihi au vinginevyo. Kwa maelezo hayo hakuna dhana ya "umachinga" kwa sababu umachinga ni reality ni ukweli dhahiri. Hapo ndipo pa kuanzia. Unaweza kujitambulisha na kujianisha na wanaoonewa kwa kunyimwa fursa za uchumi au kinyume chake hayo ndiyo matokeo ya fikra na mwelekeo wa kiitikadi na HAIZUILIKI. Kujitambua au kujianisha kutakuweka moja kwa moja na kundi husika. Kwa mfano wamachinga wana wafuasi wengi lakini wapinga wamachinga nao wana wafuasi labda kwa sababu ni waathirika na umachinga. Hizo ndizo zinazo"align political support".



Narudia hakuna dhana ya umachinga, kuna umachinga ambao ni product ya watu kujitafutia fursa za kipato kwa kiwango cha uwezo wao wa mtaji. Pia ni product ya serikali iliyoko madarakani kushindwa (fail) kujipanga kutumia rasilimali watu katika uzalishaji, usamabazaji na utumiaji wa bidhaa zinazohitajika kila siku na malaji.

Si suala la wasomi, watawala tayari wametengeneza mfumo usio na utaratibu "arnachy", udumavu wa mfumo wa siasa zisizo na tija. Hapa umenikuna maana hapo ndicho chanzo cha matatizo yote. Nasikia siku hizo umepewa jina la MFUMO DHAIFU.

Mtazamo wako huo ukiupanua, huna sababu ya kuwalalamikia wamachinga walipe kodi kwa bidhaa ambazo zimeingia nchini bila kodi kutokana na mfumo dhaifu wa utawala. Kodi ya uhakika inayokusanya na serikali yetu ni kutokana na wafanyakazi wake. Mimi nafanya kazi kwenye Kampuni binafsi, mishaharaa mizuri sana, lakini inayolipiwa kodi ni chini ya nusu anacholipwa mfanyakazi. Labda nje ya mada kodi haina maelezo au ushahidi ya jinsi inavyotumika; inasababisha fikra kuwa kodi si wajibu bali ni ulazima unaoweza kuukwepa unapopata nafasi ya kwanza.

Lakini pia tujiulize pamoja na usimamizi mbaya wa ukusanyaji kodi, hawa machinga wanaweza wakachangia kodi kiasi gani ambayo ingeleta tofauti katika makusanyo ya kodi. Hii nalinganisha na ukwepaji wa ulipa kodi wa biashara rasmi.

Habari za uhakika ni kuwa halmashauri zinawatoza kodi machinga lakini hizo kodi hazielekezwi kuwasadia hao machinga walipa kodi.



Nashukuru kuwatambua wamachinga tofauti na umacxhinga. Kwa umri wangu na hata baada ya uhuru kulikuwa na watu wakiitwa Guo Guo wahindi fulani weusi waliokuwa wanatembea kwa miguu kuuza(kusambaza) bidhaa zao hadi vijijini. Hii inaipa fursa kuwaita WASAMABAZAJI wa bidhaa sehemu ambazo hazina mfumo rasmi wa maduka ya bidhaa. Wazungu wanaita "distribution chain". Kwetu upareni tulikuwa (sasa imefifia) na masoko (kiete)ambayo ni pamoja na njia wanazopita watu ambazo mtu aliweza kujipatia bidhaa.

Hapa tulipo na umachinga na machinga ni kutokana na kushindwa kwa mfumo wetu rasmi wa kujiongoza kiuchumi kutikana na kushindwa kujipanga na shughuli zetu za uzalishaji na usambazji wa bidhaa. Sitaki kuwahukumu machinga wakati serikali nzima suala la biashara linaendeshwa kimachinga.

Kufupi machinga wapo na umachinga upo unahitaji kutetewa na kuhurumiwa na wenye huruma na wanasiasa shupavu dhidi ya udhaifu mkubwa wa uendeshaji wa utawala.


Vijana lazima watetewe kwa nguvu zote; Mungu kawajalia nguvu, akili na dhamira ya kujituma. Mfumo dhaifu umewazalisha bila nyenzo za kujikimu. Mfumo wetu umetengeneza matabaka ya kiuchumi vijana wakiwa waathirika wakubwa. Kibaya zaidi mfumo uliowatengeneza ndio unawakandamiza kwa nguvu za dola. Suluhu ya tatizo la ajira ipo. Kwanza unahitaji utetezi wa kulitambulisha, pili utetezi uwe shirikishi na mkakati wa muda mfupi wa kati na wa muda mrefu. Mkakati ambao utaingizwa kwenye mahitaji ya mtaji wa kiinchi. Kulianzishwa SIDO na VETA kukabili hili tatizo, sasa hivi hizo ni za wateule si walengwa. Kulikuwa na nyenzo na miundo mbinu ya kilimo vijijini baada ya uhuru, ikauwawa na vijiji vya ujamaa (naviita vijiji vya kukurupuka) maana viliua vijiji vya maendeleo. Hadithi au historia ni ndefu ni kuwa:-

1. Umachinga ni product ya kushindwa mfumo wa elimu katika kuzalisha rasilimali inayohitajika kwenye usambazaji wa bidhaa.

2. Umachinga ni prodcuct ya kutokuwepo mfumo wa uzalisha wa bidhaa ambao umeingiliwa na bidhaa mbadala na rahisi (hazilipiwi kodi) ambazo Wamachinga wana uwezo nazo.

3. Wamachinga wanahitaji moral, political, economic support kutoka kwa watu makini hasa wanasiasa makini wanoelewa uchungu wanaoupata katika dhamira ya kukabiliana na maisha(Kukomaa)

4. Serikali au watawala LAZIMA wabadili mtizamo wawaone machinga kama ni sehemu muhimu ya jamii ambayo inakera na inaiiabisha serikali, ambayo ni mtaji wa kisiasa ukitumiwa ipitasavyo.

On a serious note: kutetea umachinga ni ushujaa kwa sababu mwenye kulia nawe wakati wa dhiki si rafiki tu bali ni zaidi ya shujaa ni mkombozi
Mkuu umejitahidi kuwa na analysis nzuri ya matatizo yanayowakabili wananchi wetu hudusan vijana wetu.

Hatuwezi kutofautisha matatizo ya kiuchumi na kijamii na tatizo kubwa linanoibuka la umachinga.

Kama matatizo yetu ni ya kiuchumi usioendelevu na kukosekana uzalishaji mali napata kigugumizi kufikiria kuwa moja ya suluhisho la ajira kwa vijana wetu ni umachinga.
Umachinga halisi ni retail street business kwa bidhaa kutoka kwa mapapa wa kibiashara wasiolipa kodi nchini, hilo ni wazi.
Mapapa hawa wa kibiashara wanajua fika kuwa wanasiasa wanawategemea sana wamachinga kwa umaarufu wa kisiasa.

Sasa kwa mwanasiasa makini kutetea umachinga ni sawa kabisa na kuinua huo ukwepaji wa kodi ulio wazi.
Mbaya zaidi ni wanasiasa wetu(tena wa kambi zote) kutolipa kipumbele tatizo hili ili litatuliwe huko huko linakozalishwa.
Hivi ni kwa nini watu hatufikirii kilimo, viwanda vidogo na hata usindikaji wa vyakula huko huko vijijini ili mali hiyo iuzwe kwa ujumla nje na ndani ya nchi.

mkuu Mimibaba umetoa kwa kweli analysis nzuri lakini conclusion yako ni "quick fix solution" isiyo endelevu.
Kuukubali umachinga ni kukubali kushindwa kuwahudumia vijana wetu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom