On a serious note: kutetea umachinga ni ushujaa?

On a serious note: kutetea umachinga ni ushujaa?

Suala la Machinga linabebwa na wanasiasa wengi wamaopenda kupata umaarufu wa reja reja.
Na umaarufu huo si kwa chama kimoja,bali wote CCM na hata CDM, Na huko nyuma NCCR.
Msomi na thinker lazima afikiri from abstract, je , ukishapata umaarufu wa kushangiliwa na machinga ndio umetatua matatizo yao?
Far from it!

Na bahati mbaya machinga siyo kwamba hawana akili, wakisha gundua kwamba umewatapeli kisiasa , suala linakuwa baya zaidi.
Kwa miaka 50 wanatapeliwa kisiasa ndani ya mfumo ule ule, na chama kile kile, watu wale wale, sera zile zile...oops, soory, ni masopakyindi! mtetezi mkubwa wa mfumo fisadi uliowapa vilema vya maisha vijana wetu hadi wakafikia kutafuta hifadhi barabarani, na huko mnawaondoa kwa mabomu na marungu! Wakati wengine wanakwepa kulipa kodi za mabilioni, oops soory, hawakwepi! wanalindwa ndani ya mfumo ule ule, chama kile kile, watu wale wale, sera zile zile ambazo masopakyindi kaapa kuzilinda hata kwa miaka mia, kidumu chama cha wala rushwa!

Kwa kweli inatia kichefuchefu kwani machinga wapo Afrika hadi Marekani, China hadi bara Ulaya, Greenland hadi New Zealand...tofauti ni kwamba huko hakuna aliye juu ya sheria. Marekani naambiwa hata wale "homeless" wana hakika ya kutolala njaa na sasa wanafanyiwa mipango ya kuwajengea sehemu za kuogea na kujisaidia wakiamka asubuhi vibarazani mwa mahekalu! Hapa machinga ni virungu, mafisadi ni escort wasije wakadhurika, majangili ni mamlaka zaidi, wezi na wauaji ni nishani mtindo moja...aah masopakyindi, siku machinga wakizinduka!

Usiku mwema masopakyindi!
 
Last edited by a moderator:
We si una chakula cha kila siku ndio maana unaongea pumba..wengine hawana baba wala mama na serikali ndio hiyo imetupa watu wake,. wasipo kuwa wamachinga watalishwa na nani? au mnataka waingie mtaa wakabe? au waanze kuwavamia majumbani kwenu? unapo andika kitu usikurupuke, kumbuka hii nchi ina classes, sio kila mtu anapata ugali kila siku kama wewe. wengine wanakula mkate tu asubuhi.. wewe mwenye bahati ya kuwa na tarakirishi yenye intaneti unapata bahati ya kuingia jamiiforums kutoa wazo unatakiwa uwafikirie na wao, sio una fikiria kichoyo tu kisa tu wewe una kazi ya maana zaidi..
lingine li53nge linakurupika "wengine wanatembea na visu viwili siku nzima", hivyo visu amenunuliwa na baba ako, au mama ako? kwakuwa mtu yuko kwenye nchi yake na kwakuwa uzembe wa serikali umechangia kwa kiasi kikubwa yeye kuwa na maisha ya chini, kwanini tu msiheshimu anacho kifanya?
 
Mkuu, swala hapa siyo kutetea umachinga. Laiti mfumo wetu wa elimu na mfumo wa uchumi isingekuwa inazalisha wamachinga, basi tatizo la wamachinga lisingekuwepo. Wamachinga wapo kwa sababu umachinga umeletwa na mifumo yetu ya elimu na uchumi. Na kwa kuwa wamachnga ni tokeo la kushindwa kufanya kazi kwa mifumo hiyo miwili, ni lazima jamii iwakubali kwamba ni wenzetu ndani ya hiyo jamii. Wana haki ya kuthaminiwa utu wao, kutetewa na kulindwa.
Safi kabisa mkuu!
Nafikiri tatizo la umachinga lingeanza kufikiriwa na kutatuliwa from the source, hapo tungeweza kulitatua.
This is the sort of thinking ambayo ningetegemea kutoka kwa wakakilishi na viongozi wetu.

Tatizo kubwa ni kugota katika kutafuta suluhisho na kurudi kwenye misingi ya tatizo lenyewe. Sikubaliani na sentensi ya mwisho maana yake ni kukubali kushindwa na kuendejeza unyonyaji wa vijana, wakati fursa ya kuanzisha au kufufua viwanda mikoani ipo.

Kujipanga kiakili nalo linaanza kuwa tatizo la kitaifa hata kwa wakilishi wetu na viongozi.
 
Kwa miaka 50 wanatapeliwa kisiasa ndani ya mfumo ule ule, na chama kile kile, watu wale wale, sera zile zile...oops, soory, ni masopakyindi! mtetezi mkubwa wa mfumo fisadi uliowapa vilema vya maisha vijana wetu hadi wakafikia kutafuta hifadhi barabarani, na huko mnawaondoa kwa mabomu na marungu! Wakati wengine wanakwepa kulipa kodi za mabilioni, oops soory, hawakwepi! wanalindwa ndani ya mfumo ule ule, chama kile kile, watu wale wale, sera zile zile ambazo masopakyindi kaapa kuzilinda hata kwa miaka mia, kidumu chama cha wala rushwa!

Kwa kweli inatia kichefuchefu kwani machinga wapo Afrika hadi Marekani, China hadi bara Ulaya, Greenland hadi New Zealand...tofauti ni kwamba huko hakuna aliye juu ya sheria. Marekani naambiwa hata wale "homeless" wana hakika ya kutolala njaa na sasa wanafanyiwa mipango ya kuwajengea sehemu za kuogea na kujisaidia wakiamka asubuhi vibarazani mwa mahekalu! Hapa machinga ni virungu, mafisadi ni escort wasije wakadhurika, majangili ni mamlaka zaidi, wezi na wauaji ni nishani mtindo moja...aah masopakyindi, siku machinga wakizinduka!

Usiku mwema masopakyindi!

Mkuu sita ingia katika mtego wa kutokuwa objectivy na kupersonalise mada.
Thats low!

Mkuu nilitegemea mawazo mazuri zaidi kutoka kwako wewe uliyeko Marekani, China au bara Ulaya, Greenland na New Zealand.
Hata huko pengine ungeeleza kuwa mtu haamki asubuhi na vitunguu vyake akatandika barabarani ili kujipatia mkate wake.

Umeeleza vizuri kuwa hakuna aliyejuu ya sheria na hujagusia vile vile kuwa hakuna anayesamehewa kodi.

Nashangaa mkuu Mag3 kutetea kutolipa kodi kwa kundi lolote katika jamii, hayo ni mawazo ya utegemezi.

Kila afanyayeshughuli ni lazima iwe controlled ili kipato kipigwe kodi inayostahili.
Hatetewi mtu hapa na kodi ni ile ile whether unauza vitunguu, mitumba au dhahabu, na tunajua wafanyakazi wanalipa kodi kubwa tu.

Kama nilivyosema, kutetea anarchy kwa malengo ya kisiasa ni cheap politics za kuwanyonya hao vijana machinga.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, swala hapa siyo kutetea umachinga. Laiti mfumo wetu wa elimu na mfumo wa uchumi isingekuwa inazalisha wamachinga, basi tatizo la wamachinga lisingekuwepo. Wamachinga wapo kwa sababu umachinga umeletwa na mifumo yetu ya elimu na uchumi. Na kwa kuwa wamachnga ni tokeo la kushindwa kufanya kazi kwa mifumo hiyo miwili, ni lazima jamii iwakubali kwamba ni wenzetu ndani ya hiyo jamii. Wana haki ya kuthaminiwa utu wao, kutetewa na kulindwa.
huu mtindo wa kupotosha uma umeshamili sana nchini.
 
kwa sasa lazima watetewe maana angalau ni njia yao halali ya kujipatia riziki, umaachinga kwa ujumla ni zao la mfumo mbovu wa utawala hasa mfumo wa elimu na mfumo wa uchumi wa nchi, so hawa machinga ni victims tu hivo ni vema walindwe na wakti huo huo utafutwe mkakati wa muda mfupi na mrefu kuondoa tatizo hili.
.... sina uhakika kama sababu ulizotoa (mfumo mbovu wa utawala na hasa mfumo wa uchumi wa nchi) ndio sababu ya tatizo la machinga...dhana ya machinga inakubalika kiuchumi, na machinga wako hata katika nchi zilizoendelea..! tatizo ni tabia yao(baadhi yao) kukiuka taratibu (sheria) zinazoongoza shughuli zao..! sasa wanasiasa wanatetea nini? au kama kawaida yao, wanawatumia kwa ajili ya umaarufu wao wa kisiasa tu?
 
iringa is very fertile, Msigwa could use this advantage to motivate these strong and energetic young men to untite and make something out of farming or agricultural activties.

kuwafanya wana Iringa sawa na wamachinga wa dsm ambako hakuna space for kilimo ni failure kubwa sana kwa mbunge

yet shujaa??
 
Ndo ujue ni kiasi gani cha umasikini serikali ya ccm imewafikisha. Si kitu cha serikali kujivunia. Kwa hiyo kuwa na visu viwili si kama amependa, nao walipenda wawe na maghorofa kama Rizi-one, walipenda wawe na vituo vya mafuta kama Lake oil na kununua hisa Tanzanite One, ila serikali ya ccm ndiyo iliyowanyima uwezo.

Ukosefu wa Ajira Kenya na TZ,Kenya ni tatizo zaidi,wakati wa mzee mwinyi walisema karibu kila gorofa kariakoo ni ya mama SITTE MWINYI mwisho ukweli ukajulikana si kweli. so hizi siasa za rejareja tuachane nazo.
 
Serikali ya CCM imelifuga hili tatizo, vijana hawana ajira rasmi, wanahitaji kuishi kwa kufanya shughuli zilizopo UMACHINGA ili waishi, Bunge limetega Bil 3 kwenye bajeti hii, vijana wako takribani Mil 16, inamaana ni Tshs 187 kwa kila kijana, kwa mtaji huu unategemea Machinga wasiwepo, unategemea Msigwa asiwatetee wapiga kura wake?
msomi aliyeishia kuwa mlalamikaji badala ya kuwa problem solver. poor you. acheni kujiziba na pamba masikioni hali mnaona hali halisi ya mambo. wamachinga wametengewa mazingira mazuri kwa ajili ya kazi zao lakini wanasiasa wanataka kuwatumia kujitangaza kisiasa.
 
iringa is very fertile, Msigwa could use this advantage to motivate these strong and energetic young men to untite and make something out of farming or agricultural activties.

kuwafanya wana Iringa sawa na wamachinga wa dsm ambako hakuna space for kilimo ni failure kubwa sana kwa mbunge

yet shujaa??

cc.carriculum specialist na wenzako wenye mtindio wa muono
 
Erosion ya thinking katika safu ya wawakilishi wa wananchi sasa inaelekea kubaya-kwa maoni yangu!

Kwa mtu anayeelewa jinsi dhana nzima ya umachinga ilivyo asingeitetea kama mkombozi wa wananchi wasio na uwezo.
Thinking ni kwamba kwa vile barabara zipo, kwa hiyo kuna wateja barabarani, mtu hakodi cha kuweka tumboni.
Cheap thinking just as it is cheap attempt at appeasing political supporters.

Hebu tuichunguze dhana nzima ya umachinga.
Hii ni outlet of goods bila ya record za aina yoyote, kwa wasomi wa siasa ni kama kutetea anarchy, a political status quo ambayo hakuna control ya aina yoyote.

Kuna ukiukwaaji mkubwa wa kodi katika dhana hii ya umachinga, kwa vile records za bidhaa zilizoingizwa nchini, na ufuatiliaji wake wa kodi huwa hakuna.

Sasa kutetea hali hii inaleta wasiwasi kwa jamii yoyote ile.
Ni vema ikajulikana kuwa kama kuna kulipa kodi basi kila mtu asilipe ili iwe survival for the fittest.
Ni wazi kwa mtindo huu taifa linajinyonga lenyewe.

Tutofautishe kati ya wamachinga na dhana ya umachinga.

Wamachinga , originally kutoka Lindi ni kundi la vijana waliokosa kazi ya kuwapa ajira ya maana.

Hivyo basi ni vema wanasiasa wetu wakajikita katika kutatua tatizo la kuwapa vijana wetu matumainio ya maendeleo kwa kukuanzisha miradi yenye tija na manufaa kwa jamii.

Kutetea vijana kukaa vibarazani mwa wahindi au barabarani kuuza njugu na viatu hadi mitumba ni kujipatia umaarufu usio na tija. Ni kama kuvuta bangi ya kisiasana kutegemea matatizo yatapotea yenyewe.
pHakuna shortcut ya kutatua matatizo ya vijan wa nchi hii, na umachinga siyo solution.

wanajua sana ukweli huu lakini wanatafuta umaarufu wa kisiasa. kumbuka 2015 ipo karibu wanasiasa wanaanza kuchagiza kura hivo.

u said every thing, but nakuomba ufanye editing kuna makosa mengi ya kiuandishi kwenye hii taarifa yako.
 
Serikali ya CCM imelifuga hili tatizo, vijana hawana ajira rasmi, wanahitaji kuishi kwa kufanya shughuli zilizopo UMACHINGA ili waishi, Bunge limetega Bil 3 kwenye bajeti hii, vijana wako takribani Mil 16, inamaana ni Tshs 187 kwa kila kijana, kwa mtaji huu unategemea Machinga wasiwepo, unategemea Msigwa asiwatetee wapiga kura wake?
kwa mawazo haya huwezi kuwakomboa wagogo hata siku moja
 
Kama madereva tax na bodaboda wanapaki stendi na kwenye mapito ya watu wengi na hawabuguziwi hata kidogo, kwa nini tu wamachinga ndio wanyanyaswe na wafukuzwe, kama ni biashara wote hao wanafanya hivyo na kama ishu ni mobile basi wote ni hivyo tena Madereva ni wasumbufu kwa wapitao kuliko hata wamachinga, kama ni kodi basi walipe kodi ya maegesho ya mabango yao, tatizo ni ufisadi wa viongozi wetu, mtu akisha pewa hongo ni mfanyabiashara mkubwa anaamua bila kufikiria.
 
Mkiwaondoa machinga mtaanzisha tatizo jingine kubwa kuliko hilo. Kama ni kodi serikari ikachukue kodi hukohuko waliko kama ni kuwaondoa baso serikari iwashike woote waaonunua bodha kwao.Ukla ukashiba hakika utaona wamachinga si kitu ukikulia uswahilini machinga ndo wakombozi ukikulia kule magogoni machinga si kitu. Mbona pale posta mpya karibu na bot wapo je wanunuzi wa pale kina nani. Chanzo cha haya jamani ni CCM miaka hamsini hakuna chochote hakuna ajira elimu mbovu, kukusanya kodi hawawezi ,madini wamewarithisha wakoloni ,sheria zimawahusu wanyonge, shule za madaraja, Some freedom fighters fought for tje right of their people now you your fighting for the right to abbuse. Very sad
 
Wakati flani ambao utakuwa rasmi katika kufanikisha shughuli zao.kwa mfano kuna machinga wapo Arusha Karibu na Impala hotel kwa kweli hata mpangilio wa bidhaa zao unavutia eneo ni safi vitu vimewekwa kwa mpanglio,mfumo kama huo unawafaa lakini serikali haitakiwi kuwafukuza kabla ya kuboresha mazingira ya kufanania na hayo Imagine kama leo wataacha biashara zao maisha yao yatakuwaje
 
iringa is very fertile, Msigwa could use this advantage to motivate these strong and energetic young men to untite and make something out of farming or agricultural activties.

kuwafanya wana Iringa sawa na wamachinga wa dsm ambako hakuna space for kilimo ni failure kubwa sana kwa mbunge

yet shujaa??

Ingekuwa vizuri zaidi ungeeleza huko Iringa hizo fertile land zinagawiwa wapi ili wakapange foleni kuzipata, na kama zinauzwa ungewaeleza pia wapi wakachukue pesa za kununulia hizo fertile land, hapo ungetusaidia kuondoa hili tatizo la umachinga.
 
Erosion ya thinking katika safu ya wawakilishi wa wananchi sasa inaelekea kubaya-kwa maoni yangu!

Wawakilishi wetu wanawakilisha mawazo mbadala ambayo una choice ya kuyaafiki au kutokubaliana nayo lakini yakiwa yamewakilishwa. Mawazo unayoyataka wewe haimkini yamewakilishwa na umeridhika yalivyowakilishwa. "Erosion ya thinking" ina maana mmomonyoko wa fikira nikitafsiri neno kwa neno. Fikra hazimomonyoki ila zinadumaa (conservative), au zinabadilika kuwa bora au kuwa dhaifu ndiyo maana ya fikra mbadala.

Kwa mtu anayeelewa jinsi dhana nzima ya umachinga ilivyo asingeitetea kama mkombozi wa wananchi wasio na uwezo. Thinking ni kwamba kwa vile barabara zipo, kwa hiyo kuna wateja barabarani, mtu hakodi cha kuweka tumboni. Cheap thinking just as it is cheap attempt at appeasing political supporters.

Umejikita kwenye event ya barabara na tukio la Iringa ambalo hutaki kulitaja. Dhana kiswahili sahihi inanyumbulika kudhania, n.k "Tumekuwa tunadhania kwamba tuna fikra sahihi ya kuendesha nchi yetu kwa fikra za chama cha mapinduzi; sasa tunadhania vyama vya upinzani vinatoa mwelekeo mpya kuhusu maendeleo yetu" Dhana kimsingi ni mawazo tu ambayo yanaweza kuwa sahihi au vinginevyo. Kwa maelezo hayo hakuna dhana ya "umachinga" kwa sababu umachinga ni reality ni ukweli dhahiri. Hapo ndipo pa kuanzia. Unaweza kujitambulisha na kujianisha na wanaoonewa kwa kunyimwa fursa za uchumi au kinyume chake hayo ndiyo matokeo ya fikra na mwelekeo wa kiitikadi na HAIZUILIKI. Kujitambua au kujianisha kutakuweka moja kwa moja na kundi husika. Kwa mfano wamachinga wana wafuasi wengi lakini wapinga wamachinga nao wana wafuasi labda kwa sababu ni waathirika na umachinga. Hizo ndizo zinazo"align political support".

Hebu tuichunguze dhana nzima ya umachinga. Hii ni outlet of goods bila ya record za aina yoyote, kwa wasomi wa siasa ni kama kutetea anarchy, a political status quo ambayo hakuna control ya aina yoyote.

Kuna ukiukwaaji mkubwa wa kodi katika dhana hii ya umachinga, kwa vile records za bidhaa zilizoingizwa nchini, na ufuatiliaji wake wa kodi huwa hakuna.

Sasa kutetea hali hii inaleta wasiwasi kwa jamii yoyote ile.
Ni vema ikajulikana kuwa kama kuna kulipa kodi basi kila mtu asilipe ili iwe survival for the fittest.
Ni wazi kwa mtindo huu taifa linajinyonga lenyewe.

Narudia hakuna dhana ya umachinga, kuna umachinga ambao ni product ya watu kujitafutia fursa za kipato kwa kiwango cha uwezo wao wa mtaji. Pia ni product ya serikali iliyoko madarakani kushindwa (fail) kujipanga kutumia rasilimali watu katika uzalishaji, usamabazaji na utumiaji wa bidhaa zinazohitajika kila siku na malaji.

Si suala la wasomi, watawala tayari wametengeneza mfumo usio na utaratibu "arnachy", udumavu wa mfumo wa siasa zisizo na tija. Hapa umenikuna maana hapo ndicho chanzo cha matatizo yote. Nasikia siku hizo umepewa jina la MFUMO DHAIFU.

Mtazamo wako huo ukiupanua, huna sababu ya kuwalalamikia wamachinga walipe kodi kwa bidhaa ambazo zimeingia nchini bila kodi kutokana na mfumo dhaifu wa utawala. Kodi ya uhakika inayokusanya na serikali yetu ni kutokana na wafanyakazi wake. Mimi nafanya kazi kwenye Kampuni binafsi, mishaharaa mizuri sana, lakini inayolipiwa kodi ni chini ya nusu anacholipwa mfanyakazi. Labda nje ya mada kodi haina maelezo au ushahidi ya jinsi inavyotumika; inasababisha fikra kuwa kodi si wajibu bali ni ulazima unaoweza kuukwepa unapopata nafasi ya kwanza.

Lakini pia tujiulize pamoja na usimamizi mbaya wa ukusanyaji kodi, hawa machinga wanaweza wakachangia kodi kiasi gani ambayo ingeleta tofauti katika makusanyo ya kodi. Hii nalinganisha na ukwepaji wa ulipa kodi wa biashara rasmi.

Habari za uhakika ni kuwa halmashauri zinawatoza kodi machinga lakini hizo kodi hazielekezwi kuwasadia hao machinga walipa kodi.

Tutofautishe kati ya wamachinga na dhana ya umachinga.

Wamachinga , originally kutoka Lindi ni kundi la vijana waliokosa kazi ya kuwapa ajira ya maana.

Hivyo basi ni vema wanasiasa wetu wakajikita katika kutatua tatizo la kuwapa vijana wetu matumainio ya maendeleo kwa kukuanzisha miradi yenye tija na manufaa kwa jamii.

Kutetea vijana kukaa vibarazani mwa wahindi au barabarani kuuza njugu na viatu hadi mitumba ni kujipatia umaarufu usio na tija. Ni kama kuvuta bangi ya kisiasana kutegemea matatizo yatapotea yenyewe.
pHakuna shortcut ya kutatua matatizo ya vijan wa nchi hii, na umachinga siyo solution.

Nashukuru kuwatambua wamachinga tofauti na umacxhinga. Kwa umri wangu na hata baada ya uhuru kulikuwa na watu wakiitwa Guo Guo wahindi fulani weusi waliokuwa wanatembea kwa miguu kuuza(kusambaza) bidhaa zao hadi vijijini. Hii inaipa fursa kuwaita WASAMABAZAJI wa bidhaa sehemu ambazo hazina mfumo rasmi wa maduka ya bidhaa. Wazungu wanaita "distribution chain". Kwetu upareni tulikuwa (sasa imefifia) na masoko (kiete)ambayo ni pamoja na njia wanazopita watu ambazo mtu aliweza kujipatia bidhaa.

Hapa tulipo na umachinga na machinga ni kutokana na kushindwa kwa mfumo wetu rasmi wa kujiongoza kiuchumi kutikana na kushindwa kujipanga na shughuli zetu za uzalishaji na usambazji wa bidhaa. Sitaki kuwahukumu machinga wakati serikali nzima suala la biashara linaendeshwa kimachinga.

Kufupi machinga wapo na umachinga upo unahitaji kutetewa na kuhurumiwa na wenye huruma na wanasiasa shupavu dhidi ya udhaifu mkubwa wa uendeshaji wa utawala.
Kutetea vijana kukaa vibarazani mwa wahindi au barabarani kuuza njugu na viatu hadi mitumba ni kujipatia umaarufu usio na tija. Ni kama kuvuta bangi ya kisiasana kutegemea matatizo yatapotea yenyewe.
Hakuna shortcut ya kutatua matatizo ya vijan wa nchi hii, na umachinga siyo solution.

Vijana lazima watetewe kwa nguvu zote; Mungu kawajalia nguvu, akili na dhamira ya kujituma. Mfumo dhaifu umewazalisha bila nyenzo za kujikimu. Mfumo wetu umetengeneza matabaka ya kiuchumi vijana wakiwa waathirika wakubwa. Kibaya zaidi mfumo uliowatengeneza ndio unawakandamiza kwa nguvu za dola. Suluhu ya tatizo la ajira ipo. Kwanza unahitaji utetezi wa kulitambulisha, pili utetezi uwe shirikishi na mkakati wa muda mfupi wa kati na wa muda mrefu. Mkakati ambao utaingizwa kwenye mahitaji ya mtaji wa kiinchi. Kulianzishwa SIDO na VETA kukabili hili tatizo, sasa hivi hizo ni za wateule si walengwa. Kulikuwa na nyenzo na miundo mbinu ya kilimo vijijini baada ya uhuru, ikauwawa na vijiji vya ujamaa (naviita vijiji vya kukurupuka) maana viliua vijiji vya maendeleo. Hadithi au historia ni ndefu ni kuwa:-

1. Umachinga ni product ya kushindwa mfumo wa elimu katika kuzalisha rasilimali inayohitajika kwenye usambazaji wa bidhaa.

2. Umachinga ni prodcuct ya kutokuwepo mfumo wa uzalisha wa bidhaa ambao umeingiliwa na bidhaa mbadala na rahisi (hazilipiwi kodi) ambazo Wamachinga wana uwezo nazo.

3. Wamachinga wanahitaji moral, political, economic support kutoka kwa watu makini hasa wanasiasa makini wanoelewa uchungu wanaoupata katika dhamira ya kukabiliana na maisha(Kukomaa)

4. Serikali au watawala LAZIMA wabadili mtizamo wawaone machinga kama ni sehemu muhimu ya jamii ambayo inakera na inaiiabisha serikali, ambayo ni mtaji wa kisiasa ukitumiwa ipitasavyo.

On a serious note: kutetea umachinga ni ushujaa kwa sababu mwenye kulia nawe wakati wa dhiki si rafiki tu bali ni zaidi ya shujaa ni mkombozi
 
Mifumo yetu ya uchumi hasa kwa biashara ndogo ndogo haipo katika nchi yetu. Matokeo yake tunaruhusu hata wachina kujazana kariakoo kwa shughuli ambazo zingefanywa na wazalendo!
 
Back
Top Bottom