Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Kama mwananchi, ninatoa wito wa dhati kutoka katika sakafu ya moyo wangu, tena bila hila yoyote ndani mwangu kwamba CUF halali msiende Buguruni Jumapili. Ninafahamu kwamba Lipumba si halali CUF kwa kuwa alishajivua uongozi, CUF ilisharidhia kujiuzulu kwake na alishavuliwa uanachama wa CUF. Hivyo amejipachika uongozi haramu wa CUF. Ikumbukwe kuwa CUF haramu inabebwa na serikali kwa kupitia Msajili wa Vyama vya siasa. Uvamizi walioufanya CUF haramu kwenye mkutano wa waandishi wa habari ulikuwa na support ya wenye dola. Vingenevyo, CUF haramu wangeshafurushwa Buguruni na kupelekwa kunakohusika- Lupango.
CUF halali wasidhani kwamba aliyekatwa kisigino na wabwana zake wamefurahi. Watakuwa wanatafuta muda muafaka wa ku-strike back. Usafi wa jumapili unaweza kuwa fursa ya CUF haramu na mabwana zao kujibu mapigo, ingawa wao ndio waliovamia kikao. Kwa usalama wa CUF halali, ninawaomba wafute mpango wao. Habari hii imufikie Mtatiro Julius ili awaarifu wanachama wa CUF kuhusu kuachana na usafi wa Jumapili. CUF halali waendelee kutumia njia za kidemokrasia na kisheria za kuwafurusha CUF haramu kwenye ofisi zao. Huu ndiyo ujumbe katika uzi huu, uzingatiwe na hatua zichukuliwe haraka ili kuwalinda wananchi dhidi ya uharamia wa CUF haramu na mabwana zao.