Ofisi kuu ya CUF Buguruni kufanyiwa usafi siku ya Jumapili 30th April 2017

deluxelub

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
250
165
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF-CHAMA CHA WANANCHI)
OFFICE OF THE SECRETARY GENERAL

P.O.BOX 3637 ZANZIBAR, TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

• KIKAO CHA JAJI FRANCIS MUTUNGI NA WASHTAKIWA WENZAKE DHIDI YA KATIBU MKUU, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD NA,
• ZOEZI LA USAFI OFISI KUU BUGURUNI SIKU YA JUMAPILI:

Tumepokea simu nyingi kutoka kwa Waandishi wa Habari wakiulizia sababu za kutohudhuria kikao kilichoitishwa na Msajili na kufanyika leo Jijini Dar es Salaam. Tumejulishwa kuwa Msajili wa Vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi na Washtakiwa wenzake katika kesi ya wizi wa Shilingi 369 milioni za Ruzuku ya Chama Cha CUF na Mashauri mengine yaliyopo mahakamani wamekutana bila ya uwepo wetu:
1. Tunapenda kuwajulisha Waandishi wa habari na Watanzania kwa ujumla kuwa si Ofisi ya Katibu Mkuu, Mtendani, Zanzibar na wala Katibu Mkuu Maalim Seif hajapokea/haijapokea taarifa yeyote ya Barua/simu/barua pepe na au kwa njia nyingine yeyote ile wito wa kuhudhuria kikao chochote kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama ya siasa Nchini. CUF Tunaamini kuwa kama kulifanyika kikao hicho itakuwa labda ni katika muendelezo wa vikao vyao ambavyo mara zote tumekuwa tukijulishwa na Intelijensia yetu ya CUF kufanyika kwake wakijadiliana namna ya kujinasua na kesi zinazowakabili Mahakamani na kupanga Njama za kuhujumu CUF na Viongozi wake. Hatujapokea wito wowote wa kikao hicho.

2. Tumeona taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Buguruni imemuandikia barua Mbunge wa Temeke Mhe Abdallah Mtolea ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa CUF-Taifa aliyekusudia pamoja na Viongozi na Wanachama wenzake kwenda kufanya Usafi Ofisi Kuu Buguruni siku ya Jumapili kwamba Jeshi la Polisi limeelekeza kuwa “Kila Mwanachama kufanya usafi katika eneo lake analoishi/Ofisi yake anayofanyia kazi”; Tunapongeza na kuunga mkono maelekezo hayo yaliyotolewa na TARAJA C.CIBE-SSP, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Buguruni kwa kuwa Ofisi hiyo ni mali ya CUF-Chama Cha Wananchi. Na kama ambavyo Jeshi la Polisi lilivyotumika kumsindikiza Lipumba na Genge lake la wahuni kufanya uvamizi katika Ofisi hiyo tarehe 24/9/2016. Ni matarajio yetu kuwa JESHI LA POLISI litatupa ushirikiano kama huo na KUACHA TABIA YA KUZUIA KUFANYIKA KWA SHUGHULI ZOTE ZA CHAMA KWA KUSINGIZIO CHA UVUNJIFU WA AMANI HUKU LIKIMLINDA LIPUMBA NA GENGE LAKE KUFANYA WANAVYOTAKA NA KUSHINDWA KUWACHUKULIA HATUA HATA PALE WANAPOKIRI WENYEWE KWAMBA WAMEHUSIKA NA VITENDO VYA KIHALIFU KAMA WALIVYOFANYA TAREHE 22/4/2017 VINA HOTEL, MABIBO –DAR ES SALAAM.
3. CUF-CHAMA CHA WANANCHI, Tunasema sasa basi imetosha kama Wanachama walivyounga mkono Tamko la Katibu Mkuu alilolitoa katika Hotel ya Ramada Encore Tarehe 9/4/2017. WANACHAMA NA VIONGOZI WOTE TUTAKUTANA BUGURUNI OFISI KUU SIKU YA JUMAPILI KUFANYA USAFI KAMA ILIVYOPANGWA.

HAKI SAWA KWA WOTE

……………………………………..
NASSOR MAZRUI
NAIBU KATIBU MKUU-ZANZIBAR

Imetolewa leo Tarehe 28/4/2017

MAWASILIANO:
MKURUGENZI WA HABARI- SALIM BIMANI 0777 414 112/ 0752 325 227
NAIBU MKURUGNEZI- MAHARAGANDE 0715 062 577/ 0784 001 408
 
Matatizo ya wananchi ni mengi sana kwa sasa. Unga kilo sh 2000, sukari 2500, wengine tushafutwa kazi leo, hayo yote hayatoshi mnataka mkatoke nundu kwa virungu vya polisi.!
 
Kwani tatizo liko wapi wabunge na wanachama kwenda kukutana ofisi kuu ya chama chao.
 
Ni vita ya wanasiasa kati ya Katibu na mwenyekiti. Katibu kajaribu mara kadhaa kumfukiza mwenyekiti, lakini mwenyeti yuko ngangalii hafukuziki. Mwenyekiti akaona atumie hekima amuite mfanya kazi mwenzake, na tukumbike kuwa hawa ni marafiki na ni waumini safi tu wa dini ya mwenyezimungu. Mwenyekiti akaona isiwe tabu ngoja nimtimue maana hana heshma wala hekima. Kamtimua lakini wapii katibu nae kakomaa inaonekana hii vita ni ya Korea na USA sasa wameona wapimane ubavu. Eti wakamsafishe lipumba jpili.dont underestimate the power of lipumba. Ok Ngoja tuone huo usafi unaofanywa hiyo jpili. Usisahau catalyst yetu hapa ni chadema na refaree mutungi na mdhamini Wa pambano ni Ccm. Naomba mechi hii marudio yawe mwezi Wa Ramadhani ili tuone heshma ya hawa watu kweny Dini. Why you? Mbona lowasa na Jpm, hawana bifu za hivyo? We are tired of this, kama MTU angelikua anaishi duniani Mara mbili tungeomba wale waliokufa wakipambana Cuf iingie madarakani waje waone uozo wa viongozi wao....Aibu sana.
 
Usafi uko pale pale
7fa07c1875ab1f129efd6d3b57a46e16.jpg
 
Back
Top Bottom