Ommy Dimpoz zako "collabo" ila single huziwezi usipobadilika mwachie Diamond tu

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
e24f4be3f78f103ef8ea6b714dc0ec29.jpg


Ommy Dimpoz ni miongoni mwa wasanii wanaoimba vizuri sana bongo ukilinganisha na wasanii wengine ananipa jeuri ya kusema kwamba ni miongoni mwa wasanii watano wakubwa katika game ya bongo fleva ambao wanafanya vizuri

kwa sasa nimekuwa nikimfuatilia Mara kwa mara tangu akiwa katika muziki wa band na nimekuwa nikimlinganisha na wasanii mbalimbali lakini nimegundua sababu moja kubwa inayomfanya ashindwe kushindana na aliyekuwa swahiba wake Diamond Platinumz.

Dimpoz ni msanii ambae anashindwa kutamba na nyimbo zake binafsi bali amekuwa akifanya vizuri kupitia migongo ya wasanii wenzake na sababu sio kwamba huwa anatunga nyimbo mbaya sema zinashindwa kufikia hitaji la mashabiki wake

mfano nyimbo alizoimba mwenyewe wanjera [HASHTAG]#ndagushima[/HASHTAG] achiabody ni nyimbo ambazo hazikufanya vizuri ukilinganisha na nyimbo nyingine za kushirikishwa au kushirikisha mfano me&you utamu prokoto mama nainai kajiandae [HASHTAG]#sepa[/HASHTAG] ft Suma mnazalet kwa hiyo inanifanya niamini Dimpoz ni mkali zaidi wa kolabo kuliko akiimba kama Single artist.

Kushindwa kutamba kupitia ngoma zake binafsi kunamfanya kushindwa kushindana na Diamond Platnumz mwenzake kila ngoma anayotoa NI kali iwe kashrikishwa au kashirikisha So nikiambiwa nimshauri Ommy Dimpoz kwa sasa nitamweleza aangalie staili mpya ya utoaji nyimbo hasa anazoimba peke yake ili ashine kama ilivyo kwa [HASHTAG]#kingkiba[/HASHTAG] kila ngoma akitoa NI chuma au kama vipi aache awe anatoa Collabo tu.

Lakini Sio Dimpoz hata Shetta pia braza ukitoa wimbo kama msanii mmoja haushine mfano [HASHTAG]#namjua[/HASHTAG] track kali lakini imepotea lakini cheki ulivotufantia kwenye nidanganye [HASHTAG]#kerewa[/HASHTAG] mdananda nimechokwa shikorobo bongelabwana.

[HASHTAG]#kijanamzalendo[/HASHTAG] [HASHTAG]#ilovetz[/HASHTAG] [HASHTAG]#maoniyangu[/HASHTAG] [HASHTAG]#sangujoseph[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom