Ombi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mkulima, Oct 31, 2010.

 1. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Wakuu,

  Uchaguzi unaisha leo saa 12.

  Ninawaomba baada ya hapo tupeane habari za uchaguzi kwa amani bila matusi wala jazba. Tujiepushe na zile habari za kuzua na kuwadanganya wana JF.

  Kama mnakumbuka wakati wa uchaguzi wa Kenya, kuna wana JF ambao walituhabarisha vizuri sana. Wao walikuwa wapenzi wa ODM lakini hata pale Kibaki alipokuwa anafanya vizuri walikuwa wanatoa habari. Watu tulikesha tukifuatilia uchaguzi huo.

  Baada ya saa 12 hutamshawishi mtu yeyote akipigie chama chako kura hivyo ukivuruga thread utakuwa unatuudhi bure wana JF.

  Labda tutengeneze threads mbili; moja ya matokeo ya urais na nyingine ya ubunge. Wale wenye info kutoka vituoni na wilaya watujulishe na wengine tupige thanks na kutoa comments zetu fupi fupi.

  Wale watakaojaribu kuvurugu hizo threads wafungiwe mpaka baada ya uchaguzi.

  Moderators inabidi kuwa wakali sana siku ya leo ili tumalize hili zoezi salama.
   
Loading...