Ombi: Ukaguzi wa vyeti ufike majeshi yote haraka

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Hivi ni vyombo muhimu sana kwenye taifa letu, hivyo linatakiwa kuongozwa na watu wenye uelewa wa hali ya juu.Nina uhakika kwa utaratibu wa zamani kuna kundi kubwa sana la maaskari ambao hawana vyeti vya shule. Wapo wengine wanatumia vya ndugu zao.


Kuna hofu kua kuna makamishna, majenerali, manaibu kamishna, makanali, maluten, majors, brigedia,masajent,warakibu na vyeo vingine vingi kwenye majeshi haya yote nchi kuanzia JWTZ,POLISI,MAGEREZA,UHAMIAJI, JKT,USALAMA WA TAIFA,ZIMA MOTO nk. Kuna watu wahodhi hivi vyeo bila ya kua na sifa, kama zilivyo taasisi zingine serikalini na kwa nia ya dhati ya serikali ukaguzi huu ufike hadi huko.


Mzee wangu IGP hua nikimsikiliza mzee wangu mmoja ambaye ni mjomba wangu na askari mustaafu akinisimulia jinsi alivyokua akikupatia nafasi ya kwenda kusoma chuo kikuu mlipokua kambi moja yeye akiwa mkuu wa kambi, ukimlilia ukiomba upangwe shift za lindo la usiku tu ili usome mchana,pengine hata usingefika huko kuliko kwa huruma yake hiyo. Kwahiyo sina shaka na shule yako, shughulika na watu wapo wasio na sifa chini yako watakupa shida kwenye utekelezaji.Iwe hivyo na kwa majeshi megine,hawa ni sawa na watumishi hewa tu.

Kama ni kweli serikali imeamua kwa dhati bila kujali cheo cha mtu, ichukue hatua kwa watumishi wote,wasio na sifa wapumzishwe na washtakiwe kwa kuliibia taifa kwa muda wote. Isiwe TRA, Bandarini na sehemu zingine za kiraia lakini pia kwenye majeshi kama taasisi za umma fagio lipite tu.
 
Ukigusa huko kwenye hizo taasisi ni lazima ajira mpya nyingi zitokee na zitatingisha sana usalama. Kwa misingi hii watachukulia hizi sehemu kwa umakini wake hasa wa walio wa rank za juu wa sasa. Walio na umri mdogo up to 30 Years utaratibu wa ajira ulifuata vyeti vyenye uhakika zaidi vya NECTA.
 
We uliyetoa mada hii ni mtusi wewe usiyetutakia amani. We unadhani wanajeshi na Polisi ni sawa na walimu? Leo unaweza ukafukuza walimu laki mbili na hamna shida. Sasa fukuza wanajeshi mia tu uone msala wake. Kama umeshiba makande yako usiwe unapost ujinga.
 
Mtoa mada mbona yuko sahihi sana..maana hata wanajeshi nao ni watumishi wa UMMA na RAIS anataka haki bin haki katika kutawala. Kumbuka hakuna aliye juu ya sheria wala katiba. Ukaguzi wa vyeti ni muhimu kupita maelekezo na lazima ufanyike kwa wafanyakazi wote bila kubagua Idara yeyote. Tunataka kujenga viwanda na kubana matumizi hivyo lazima haki itendeke bhana..:(
 
Back
Top Bottom