Ombi: mei mosi mwaka huu tuongeze uhakika wa mshahara wa ile asilimia kubwa wasio na ajira rasmi....

Ame

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
6,194
5,222
Nimefuatilia malumbano ya hoja ITV leo....kuna mdau katoa wazo la busara sana kwamba wakati wengine wetu tunalalamika kuongezewa salary wapo ambao monthly salary yao ni zero....au negative yaani deni....sasa Mh. Rais na watanzania wote tumkumbuke huyu mfanyakazi asiye na kazi rasmi badala ya kuongeza mishahara yetu basi hiyo pesa inayopatikana katika kubana matumizi itumike kurekebisha hayo maisha ya wenzetu yasio kuwa coordinated....

Wenzetu wanatoa non-employment salary kwa wote wasio na mshahara na sisi sasa tuangalie tukianzia na makundi makuu kama wazee, vilema, wangonjwa wa muda mrefu nk....tumesha hakikisha tunazo fedha za kutosha katika mifuko yetu ya jamii hivyo tukiongeza na kiasi kidogo tulichoamua kubana naamini tutaweza. Tukiwekeza kwenye hayo makundi tunalunguza utegemezi ambao utaongeza mapato ya wafanyakazi. Lakini pia kutapunguza matatizo yaambatanayo na maisha magumu na hivyo kupunguza pia matumizi kwenye sector ya afya....etc etc

Lakini pia tuweze kuratibu shughuli ambazo hazijaratibiwa kama kilimo.... Tupo wataalamu serikalini bila kuongezewa mshahara tunaweza kutoa ushauri ambao watawala watakuwa na hiari ya kuupokea au kuuacha.

Inasikitisha kuona tumezungukwa na wimbi kubwa la watu wasioratibiwa lakini wana nguvu kazi ambayo inge ratibiwa au kwa luga ya wenzetu managed ingeweza kuongeza tija na kuwalipa mshahara wa uhakika kila mwezi.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom