Ombi Maalum: Rais Magufuli sasa unda timu huru ya wakemia kuchunguza jambo hili

Jorojik

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,102
7,284
Rais wangu Dr. Magufuli sasa unda timu maalum ili kupata ufumbuzi wa suala hili


Kati ya Mei na Julai mwaka huu kulitokea rapsha kati ya Waziri wa Kilimo, Katibu Mkuu Kilimo na Taasisi inayohusika na Udhibiti wa Matumizi ya Viuatilifu hapa nchini (pesticide management and control in Tanzania). Taasisi hiyo (TPRI) ipo mjini Arusha chini ya Wizara ya Kilimo. Pamoja na majukumu mengine, TPRI kisheria ina jukumu la kuhakiki wa ubora wa viuatilifu (pesticide quality verification) vinavyoingizwa nchini na vile vinavyotengenezwa (formulated) hapa nchini kabla ya kumfikia mkulima na watumiaji wengine. Taasisi pia hushirikiana na wakulima kutatua malalamiko yao kitaalamu kwa yale viuatilifu ambavyo havikufanya kazi kama ilivyotarajiwa. Lengo la Serikali kuwa na Taasisi ya kuhakiki ubora wa viatilifu hapa nchini ni:

· Kuhakikisha viuatilifu visivyokidhi viwango (substandard/fake pesticide products) havimfikii mkulima. Kisheria, ni viuatilifu vinavyokidhi viwango tuu huruhusiwa kuingia nchini ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na kulinda mazingira.

· Kuzuia nchi kutokuwa dampo la viuatilifu hafifu ambavyo mwisho wa siku ni tishio kwa mazingira na binadamu. Ikumbukwe hizi kemikali ni sumu, vile visivyokidhi viwango vikiruhusiwa nchini, definitely wakulima hawatotumia. Hatimaye kutakuwa na piles ya obsolete pesticide products (viuatilifu chakavu) ambavyo ni hatarishi kwa mazingira (hasa maji na udongo. Maji hutumiwa na binadamu, wanyama na viumbe wengine.

· Kuongeza tija na uzalisaji katika mazao ya kilimo hivyo kuongeza pato la mkulima mojamoja na la nchi kwa ujumla.

TPRI huhudumia wafanyabiashara wa viuatilifu nchini, wakulima wakubwa na wadogo, sekta za serikali kama vile Bodi ya pamba na korosho, sekta ya mifugo na sekta ya fya (vuatilifu vya kudhibiti mbu hasa IRS – Indoor Residue Spraying; watu wa kanda ya ziwa na Zanzibar wanafahamu sana haya mambo ya IRS)

Mwaka huu (2017) kampuni ya ETG (Export Trading Company) ilipewa tenda ya kuagiza na kusambaza kiuatilifu aina ya falcon sulphur dust kwa ajili ya zao la korosho. Uagizaji huo ulifanyika kupitia Bodi ya Korosho. Kisheria (Sheria ya Plant Protection, 1997 na TPRI, 1979) kabla kiuatilifu kilichoagizwa kutoka nje ya nchi kusambazwa kwa wakulima ni lazima sampuli za kiuatilifu hicho ziende kwanza TPRI (Arusha) kwa ajili ya kuhakiki ubora wa kiuatilifu hicho. Hivyo basi, shehena ya awali ya falcon sulfur dust ilipoingia nchini mnamo Mei, 2017, sampuli zilipelekwa TPRI kwa ajili uchambuzi wa kimaabara (laboratory analysis). Baada ya uchambuzi wa kimaabara ilionekana falcon sulfur dust kutokidhi viwango katika parameter ya particle size (fines). Kwa kuwa shehena hiyo ya falcon sulfur dust haikukidhi viwango katika kipengele cha fines (particle size) Bodi ya Korosho ilijulishwa kuwa Falcon sulfur haikidhi viwango. Hivyo endapo itatumiwa na wakulima inaweza isiwalete tija.

Note: Parameters nne (4) muhimu zinazochambuliwa (analysed) kwa kiuatilifu aina sulfur dust ni purity, moisture content, acidity na particle size (fines). Na FAO spefications za parameters hizo ni kama ifuatavyo:

i. Sulfur Purity: 99.5% or above

ii. Moisutre content: 0.1% Maximum

iii. Acidity content: 0.03% Maximum

iv. Particle size (fines): to pass by 99.5% or above through 100 mesh number (150µm mesh size).

Kwa matokeo ya uchambuzi wa kimaabara TPRI, Falcon Sulfur Dust ilikuwa inapita kwa wastani wa 50% tuu kwenye mesh size ya 150µm badala ya 99% kama standard inavyoelekeza hapo juu. Kwa mantiki hiyo falcon sulfur ilikuwa hafifu (substandard) kwa 50% na isingefanya kazi katika mashamba ya korosho kama inavyotakiwa.

Baada ya matokeo hayo, ETG (kampuni ya wahindi) kwa kushirikiana na Katibu Mkuu Kilimo (Mathew Mtigumwe) na Waziri wa sasa wa Kilimo (Charles Tizeba) waligoma kupokea matokeo hayo wakidai sulfur yao ni nzuri. Waziri akalazimisha ifanyike re-analysis nia ikiwa ni kutaka kulazimisha kubadilisha matokeo ya maabara. Uchambuzi ulirudiwa tena, matokeo yakabaki palepale. Walipoona TPRI imegoma kubadili matokeo ya kimaabara vitisho vilianza kila kona kutoka kwa Katibu Mkuu Kilimo, Waziri wa sasa wa Kilimo na ETG wenyewe

Baadaye wakazunguka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali. Mkemia wa Serikali mbele ya mkutano ulioitwa wa wadau wa Korosho ulioitishwa na Waziri Mkuu aliuhakikishia umma kwamba Falcon Sulfur inakidhi ubora unaotakiwa hivyo inafaa kwa matumizi ya korosho. Pale pale Waziri Mkuu alitoa agizo kuwa falcon sulfur dust iende kwa wakulima mara moja kwa mujibu wa matokeo ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Hapo hapo akasema mkanganyiko wa taarifa hizi za kimaabara kati ya Taasisi ya Serikali ya TPRI na Mkemia Mkuu wa Serikali ichunguzwe kujua nini kilitokea. Kuchunguza mkanganyiko wa taarifa ile ya kisayansi maana yake ingekuwa ni kuunda timu ya wataalam huru na kuangalia mchakato mzima wa laboratory analysis na kurudia uchambuzi wa sampuli zile (sampuli bado zipo) kusudi matokeo ya timu hiyo yalinganishwe na yale ya TPRI na ya Mkemia Mkuu wa Serikali kujua mbivu na mbichi.

Hadi leo hakuna tume yoyote ya wataalam wa maabara iliyoundwa na Wizara ya Kilimo kuchunguza sababu ya Taasisi hizi mbili kutoa taarifa tofauti za kiuchambuzi kwa shehena ileile? Badala yake Katibu Mkuu Kilimo (kwa order ya Waziri wa Kilimo bila shaka) akakimbilia kusimamisha wafanyakazi watatu wa TPRI toka Julai 1, 2017 hadi sasa. Wapo tu manyumbani wamekaa tu, hakuna tume yoyote iliyoundwa kuwahoji! Kimyaaaaa! Maana yake ni nini? Miezi minne imepita sasa!

Mhe. Rais tunatambua ni namna gani unachukia watumishi wa umma wanaotumia taaluma yao vibaya tena baada ya kusomeshwa na serikali kwa gharama kubwa. Umekuwa ukitoa mfano wa wale wataalam wa TMAA katika migodi ya dhahabu na almasi. Sasa hawa wa TPRI walisimamia mwanzo mwisho taaluma na ethics ya kazi yao lakini bado wameadhibiwa vikali. Nchi hii inahitaji watu au wataalamu wa aina gani hasa? Mkemia wa Serikali ambaye inaaminika alitoa false report ya falcon sulfur kwa maelekezo ya wanasiasa bado yupo ofisini anakula kiyoyozi. Kwa ripoti yake ile sasa Serikali yako italipa mabilioni ya shilingi za kitanzania kulipia falcon sulfur dust ambayo ni duni na haikutumiwa na wakulima. Sulfur ambayo iliingizwa nchini kwa ghilba kubwa kati ya ETG na Bodi ya Korosho chini ya maelekezo ya Waziri wa Kilimo na Katibu Mkuu Kilimo bila shaka. Tunaomba uwamulike kwa karibu kampuni ya ETG na Bodi ya Korosho katika suala hili. Tunasema hili kwa sababu Bodi ya Korosho baada ya kuona falcon sulfur dust haikubaliki ikaanza kulazimisha wakulima kutumia sulfur ya maji aina ya Devisulfur na Sulfex Gold ambazo zilikuwa zimeisha muda wake wa matumizi (expired). Tunashukuru Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wa wakati ule (Mhe. Halima Dendego) alipambana na hilo hali iliyosababisha Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho (Bw. Jarufu) kuwekwa lock up mara kadhaa kwa attempts zake za kupeleka expired sulfur kwa wakulima.

Waziri wa Kilimo kwa kujua amefanya hila kubwa kwenye falcon sulfur dust, sasa amebaki anapiga siasa juu ya umuhimu wa kutumia sulfur dust bora yenye viwango vinavyokubalika kimataifa katika zao la Korosho. Mfano mzuri ni majuzi alipoulizwa na Sam Mahela (ktk dk 45 ITV, Oktoba 16, 2017) juu ya uvumi wa matumizi ya sulfur duni kwenye zao korosho, akajibu haraka haraka kisiasa ati sulfur haina expire date kwa sababu ni element kama ilivyo copper au zinc. Hapohapo akaachana na sulfur za Korosho akarukia viuatilifu vya pamba na kumwaga uwongo mkubwa. Jamani sulfur dust ikishasharabu (absorb) unyevu wa kutosha aidha kwa utunzani mbovu au kwa sababu yoyote ile lazima igande kama jiwe. Huko ndiko kuexpire kwenyewe. Ndiyo maana ni lazima kuangalia kiwango cha unyevu (moisture content) kwenye maabara kabla ya kupelekwa kwa wakulima. Pia ikishakuwa na kiasi kikubwa cha tindikali (acidity) aidha kwa kusharabu unyevu au kwa oxidation process lazima iharibike. Huko ndiyo kuexpire kwa sulfur za vumbi. Lakini pia ukipitia dossiers (taarifa za kitaalamu kutoka kwa manufacturer) za sulfur dust zote ambazo zimesajiliwa nchini Tanzania, manufacturers wamerecommend shelf life ya miaka 5. Sasa Waziri anaposema sulfur dust haina expire date ana maana gani? Mbona Chumvi ya mezani ambayo ni sodium chloride (elements sawa na zinc, copper etc) zina expire dates? Nazo si zimetengenezwa kwa elements za sodium na chlorine tuu? Waziri Tizeba think twice unapoongea na watanzania hasa kwenye masuala ya taaluma. Ni ajabu kwa Waziri tena wa serikali ya awamu ya tano kuungana na mfanyabiashara binafsi kupinga matokeo ya kisayansi yaliyotolewa na Taasisi ya Serikali huku hataki matokeo hayo yawe verified upya na timu huru ya wakemia tena katika maabara yoyote dunia itakayoonekana inafaa almradi kutanzua kitendawili hiki.

Mhe. Raisi kwa heshima kubwa naomba sasa unda tume huru ya chemical analysts (chemists) ili uchunguzi huru ufanyike juu ya suala hili. Reanalysis ifanyike juu ya kile kipengele cha fines (particle size) ili kujua kati ya Mkemia wa Serikali na TPRI nani alitoa matokea yenye walakin! Baada ya hapo hatua kali ichukuliwe ikigundulika kuna maabara kati ya TPRI na Mkemia wa Serikali ilitoa matokeo yasiyo ya kweli. Waziri wa Kilimo na Katibu Mkuu Kilimo wamulikwe kwa karibu kwa uonevu huu uliopelekea wafanyakazi hao watatu wa TPRI kusimamishwa bila kuundiwa tume ya kuchunguza sakata hilo toka julai hadi sasa. Wafanyakazi hao wameumia kisaikolojia bila shaka huku wakijua hawakutenda kosa lolote kisa tuu waligoma kutii matakwa ya wanasiasa na kusimamia ethics ya taaluma yao. Wafanyakazi hao walikuwa wanalinda maslahi ya wakulima wa Korosho na nchi kwa ujumla kwa kuzuia kiuatilifu hicho hafifu kisiwafikie.


Mhe. Rais nawasilisha haya kwako kwa unyenyekevu mkubwa.
 
Hii mada imenikumbusha enzi za JF ilivyokuwa kwa wadau kama nyie kumwaga nondo kali.

Natumaini wengi wataanza kufunguka tuzidi kufurahia kuwemo humu JamiiForums aka JamboForums yetu ile.
Haya hayakutakiwa kutokea katika kipindi hiki cha JPM. Lakini ndiyo hivyo tena yametokea. Tunaamini Mhe. Magufuli ataliangalia kwa jicho la pekee.
 
Haya hayakutakiwa kutokea katika kipindi hiki cha JPM. Lakini ndiyo hivyo tena yametokea. Tunaamini Mhe. Magufuli ataliangalia kwa jicho la pekee.

Ndio.
Kuna mengi yanaendelea.. naamini na muda ataweza kuyanyakua kwa asilimia kubwa.
Ila kwa sasa nampa sana hongera alipofikia..

Naamini atasoma kwa sababu ni msomaji mzuri wa humu kutokana na anayotamkaga kwenye hotuba zake.
 
Heshima kwako mtoa nondo kali na hii......nimeipenda sana ni somo zuri sana kweli JF n shule kuu kabisaa!!! Kazi kwa aliowaweka kuwachunguza haraka sana maana nasikia PM amebakia kupiga deal kwenye korosho pekeyake
 
Ndio.
Kuna mengi yanaendelea.. naamini na muda ataweza kuyanyakua kwa asilimia kubwa.
Ila kwa sasa nampa sana hongera alipofikia..

Naamini atasoma kwa sababu ni msomaji mzuri wa humu kutokana na anayotamkaga kwenye hotuba zake.
Akishindwa kupita humu kutokana na majukumu mazito ya kitaifa, tunaamini wasaidizi wake watampelekea. Kwa kweli kuna mengi yanaendelea na baadhi ya wafanyakazi wakiumizwa kwa kiasi kikubwa. Rais Magufuli ni muungwana sana, hili jambo atalimaliza na hatimaye uonevu utakwisha.
 
Ndio.
Kuna mengi yanaendelea.. naamini na muda ataweza kuyanyakua kwa asilimia kubwa.
Ila kwa sasa nampa sana hongera alipofikia..

Naamini atasoma kwa sababu ni msomaji mzuri wa humu kutokana na anayotamkaga kwenye hotuba zake.
Akishindwa kupita humu kutokana na majukumu mazito ya kitaifa, tunaamini wasaidizi wake watampelekea. Kwa kweli kuna mengi yanaendelea na baadhi ya wafanyakazi wakiumizwa kwa kiasi kikubwa. Rais Magufuli ni muungwana sana, hili jambo atalimaliza na hatimaye uonevu utakwisha.
 
Heshima kwako mtoa nondo kali na hii......nimeipenda sana ni somo zuri sana kweli JF n shule kuu kabisaa!!! Kazi kwa aliowaweka kuwachunguza haraka sana maana nasikia PM amebakia kupiga deal kwenye korosho pekeyake
Hii nchi ni ngumu mkubwa. Mambo ni mengi na mazito sana
 
Heshima kwako mtoa nondo kali na hii......nimeipenda sana ni somo zuri sana kweli JF n shule kuu kabisaa!!! Kazi kwa aliowaweka kuwachunguza haraka sana maana nasikia PM amebakia kupiga deal kwenye korosho pekeyake
Hii ndio sura niliyokua nayo kuhusu JF miaka kadhaa iliyopita kabda sijajiunga....jamaa amelitendea hali jukwaa
 
Tunajua sana awamu hii Kolomije wanapiga wenyewe tu sasa wenzake nao wanalia njaa.....wameona watokee kwenye korosho....nadhani PM anahaha kusaka chochote maana akishangaa atatoka kapa....Bashite anapiga dealkubwa zote kwa mgongo wa Baba yake....PM amewekwa kando.....na watu wake njaaaa.......sasa wanaharibu sababu njaa......
Hii nchi ni ngumu mkubwa. Mambo ni mengi na mazito sana
 
Akishindwa kupita humu kutokana na majukumu mazito ya kitaifa, tunaamini wasaidizi wake watampelekea. Kwa kweli kuna mengi yanaendelea na baadhi ya wafanyakazi wakiumizwa kwa kiasi kikubwa. Rais Magufuli ni muungwana sana, hili jambo atalimaliza na hatimaye uonevu utakwisha.
Natimaini coco channel atapeleka maana kapita hapa na kauona huu Uzi...Asibaki kupiga ngonjera na mapambio ya kusifia tuuu
 
Hii ndio sura niliyokua nayo kuhusu JF miaka kadhaa iliyopita kabda sijajiunga....jamaa amelitendea hali jukwaa

Hii ilishakatazwa inaitwa UCHOCHEZI, unaifarakanisha serekali na wananchi kw akutoa siri za serekali na sheria ilitungwa, na tangaia hapo ndi mwisho wa Jf hakuna tena siri zinazopatikana huko serekalini.

Sikuhizi hata ripoti za CAG naona ni siri.
 
Back
Top Bottom